Sunday 31 December 2017

BABU YANGU SALUM ABDALLAH











Nanren,
Aliyewekwa kizuizini si baba yangu.
Aliyewekwa kizuizini ni babu yangu Salum Abdallah.

Hakuwekwa kwa ajili ya dini.

Yeye alikuwa Mwenyekiti wa Tanganyika Railway African Union (TRAU)
chama alichokiasisi na kuwa mwenyekiti wake mwaka wa 1955 Kasanga
Tumbo akiwa katibu.

TRAU ilipigana bega kwa bega katika uhuru wa Tanganyika na babu yangu
ni katika wanachama wa mwanzo wa TANU Tabora.

Yeye alikuwa katika kamati ya siri iliyokuwa ikifanya mikutano mjini hapo
kwa matayarisho ya kuundwa TANU.

Salum Abdallah alipigana kwa hali na mali katika kupambana na ukoloni.
Mwaka wa 1947 aliongoza General Strike halikadhalika mwaka wa 1949.

Mwaka wa 1960 aliongoza mgomo wa Railway uliodumu siku 82 kuvunja
rekodi ya mgomo wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh Kenya.

Salum Abdallah alikamatwa na kuwekwa kizuizini baada ya maasi ya KAR 
ya mwaka wa 1964 pamoja na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi.

Lakini kesi ile ya waasi ilipokwenda mahakamani hawa viongozi wa vyama vya 
wafanyakazi hawakushitakiwa kwa uasi.

Kuwekwa kwao ndani ilikuwa Mwalimu Nyerere anatafuta nafasi ya kuunda 
chama kimoja cha wafanyakazi kitakachowekwa chini ya TANU.

Ule mgomo wa mwaka wa 1960 ndiyo uliomtia hofu Mwalimu Nyerere kwa 
kudhihirikiwa kuwa kulikuwa na viongozi wa watu kama yeye ambao walikuwa 
wakisikilizwa na wananchi.

Mara tu baada ya uhuru mwaka wa 1962 Nyerere aliitisha mkutano Moshi wa 
viongozi wa wafanyakazi agenda ikiwa kuwa na chama kimoja chini ya TANU.

Babu yangu alikuwa mmoja wa watu waliompinga katika wazo hilo kwa hoja nzito.

Nyerere hakufurahishwa na yeye.

Babu yangu alipotoka kizuizini alijitoa katika siasa na kujikita katika biashara na 
kilimo cha tumbuku Urambo.

Alipokufa mwaka wa 1974 TANU ilifika mazikoni na walisoma taazia ya kumsifia
wakisema kuwa Salum Abdallah aliweka mfuko wake wazi kwa TANU wakati
wa kupigania uhuru.

Babu yangu hakupata kujiunga na AMNUT yeye alikuwa TANU hadi alipohisi usaliti
ndani ya chama uliosababisha yeye kuwekwa kizuizini kwa shutuma za uongo.

Bahati mbaya sana umekuwa ukiamini kuwa babu yangu aliwekwa ndani kwa ajili
ya Uislam.

Naamini kuanzia sasa unampa babu yangu heshima anayostahili kama mpigania
haki na uhuru wa Tanganyika.

Itapendeza kama ndugu zangu mkajizuia kuandika mambo ambayo hamyajui.

Hiyo unayoita ''chokochoko,'' ukiwa unataka kuelewa historia yake fungua uzi In 
Shaallah nitakuja na nitatoa darsa.


Hii nyaraka hapo chini ambayo inasema kuwa viongozi wa wafanyakazi akiwamo 
babu yangu walihusika katika maasi, kesi ilipofikishwa mahakamani hakuna hata
kiongozi mmoja wa wafanyakazi alishtakiwa.

Viongozi hawa walibakia wameshikiliwa katika jela tofauti kisha wakaachiwa bila
ya mashtaka.



No comments: