1. Amour Muhammed Al Barwani
2. Muhammed Abdulla Al Ghassany (marehemu Baba)
3. Saleh ( Baba yake alikuwa akiuza Haluwa)
4. Muhammed Abdulla Salim Al Barwani
5. Unknown
6. Saleh Awadh Al Hadhramy
7. Unknown
8. Muhammed Amran ( From Pemba)
9. Muhammed Muhammed Othman
10. Unknown
Waliokaa kwenye viti kutoka kulia1. Eisa Muhammed Said Al Barwani
2. Ahmed Rashad Ali Bakashmar (marehemu Mzee Rashadi)
3. Hussein Gahtan
4. Maalim Hilal Al Barwani
5. Ali Muhsin Al Barwani (marehemu Sheikh Ali Muhsin)
6. Ali Khalifa Al Miskry
7. Ali Said
Waliokaa Chini kwenye ardhi kutoka kulia
1. Muhammed Ali Ameir Al Marhoubi
2. Suleiman Said Al Kharusy
Majina yote ameyapata Sheikh Taha Baharoon (wa Dubai) kutoka kwa Bwana Amour Muhammed Al Barwani aliyopo Muscat.
Tutakuwekeeani hapa maisha ya Ahmed Rashad Ali na katika maisha yake lau kwa mukhtahsari tutamtaja Ali Muhsin Barwani. Wote hawa wawili ni watu ambao historia ya ukombozi wa Zanzibar haiwezi kukamilika bila kuwataja.
Ahmad Rashad Ali alikuja kuwa mcheza mpira maarufu India wakati akiwa mwanafunzi na kisha kuwa mchezaji maarufu na nahodha wa timu ya Zanzibar katika mashindano ya Gossage Cup katika miaka 1940 hadi 1950. Ali Muhsin alifahamika kwa kuwa hodari vilevile katika mpira utotoni lakini zaidi kwa uhidari wa masoma darasani kiasi cha kwenda kusoma Makerere College, Uganda. Lakini Ali Muhsin atakachokumbukwa sana kwa siku zile ni kuongoza harakati za siasa chini ya Zanzibar Nationalist Party (ZNP) au kwa jina lingine Hizbu L' Watan. Ali Muhsin alikuwa katika serikali ya kwanza ya Zanzibar iliyopinduliwa mwaka 1964 na yeye akawekwa kifungoni Tanzania Bara kwa amri ya Nyerere kwa miaka 10.
Vuteni subra tunatayarisha mahanjumati...
Ahmed Rashad Ali Bingwa wa Propaganda za Ukombozi wa Afrika
Ahmed Rashad Ali |
Ahmed Rashad Ali na Sidney Poitier Uwanja wa Ndege Dar es Salaam 1973 |
Mwishoni
mwa kwama wa 1950 kilichipuka chama cha siri Zanzibar ,
Haki za binaadamuí chama hiki kinaweza kuchukuliwa kama
chama cha kwanza kilichokuwa na chembechembe za siasa. Waliosababisha mwamko
huu mpya walikuwa Ahmed Rashad Ali Ahmed Said Kharus maarufu kwa jina la
Bamanga au “Guy.” Ahmed Rashad Ali alikuwa na ngozi nyeusi na kwa kumwangalia usingedhani
kuwa ni Mwarabu. Bamanga alikuwa Mwarabu. Kumekuwapo na kuoana kati ya Waarabu
na Waafrika kiasi cha kupoteza kabisa damu ya Kiarabu iliyokuwa haina mchanganyiko.
Kwa ajili ya utambulisho mtu atatambuliwa kuwa ni Mwarabu kama
atakuwa na ngozi nyeupe. Unaweza kwa hiyo kumpata Mwarabu mwenye ngozi nyeusi
akatambulika kama Mwafrika. Kitu cha kuangalia
katika kuwatambua watu na hadhi zao ilikuwa hali ya maisha katika jamii na si
rangi zao. Kulikuwa na uvumi kuwa Bamanga alipokuwa Kenya alipata kujitia katika Mau
Mau na kwa ajili hii akapewa jina la utani, Aterere
neno la Kikuyu lenye maana ‘njoo hapa.’ Bamanga alikuwa anatoka kwenye ukoo
wenye kujiweza wa Kiarabu. Baba yake alikuwa District Commissioner. Ahmed Said
Kharus au kama alivyozoeleka kwa jina lake la kupanga Bamanga alikuwa akisikika
mara nyingi akiwalaumu Waarabu kwa mateso mengi yaliyokuwa yakiwafika Waafrika kama
vile yeye hakuwa Mwarabu. Katika nyakati zake za kupumzika Bamanga alikuwa
mpiganaji masumbwi na kwa kuwa alikuwa na jumbo kubwa mchezo huu ulimfaa sana .
Aliyesimama wa pili kulia Ahmed Said Abdullah Alkharusi (Bamanga) |
Rafiki
yake Ahmed Rashad Ali, yeye alikuwa mweusi na ingekuwa taabu sana kwake yeye kujinasibu na Urabu ingawa damu
ya Kiarabu ilikuwa ikitembea ndani ya mishipa yake. Tofauti na Kharus, Rashad
alikuwa msomi kwa kiasi chake alikuwa amepata elimu yake ya mwanzo Zainzibar na
India
kati ya mwaka wa 1937 – 1947. Alikwenda India akiwa na umri wa miaka
ishirini. Rashad kama alivyokuwa rafiki
yake Kharus alikuwa anatoka kwenye ukoo wenye kujiweza. Bamanga na Ahmed Rashad
walikutanisha fikra zao zilizojaa yake waliyoyaona Kenya
na India na wakaamua
kuanzisha vuguvugu la siasa kama lile kwa wakati ule lililokuwa Kenya na India . Haukupita muda Bamanga na
Rashad wakawa wamepata wafuasi. Hii kwao haikuwa vigumu kwa kuwa wote wawili
walikuwa wanamichezo maarufu. Bamanga mwana-masumbwi na Rashad alikuwa mcheza
kriketi wa sifa na vilevile alicheza mpira wa kulipwa Bombay
na akawa nahodha wa timu ya Zanzibar
kwa miaka saba. Hawa vijana wawili wakaonekana na wale ambao walikutananao kama vijana wa maendeleo waliokuwa na maslahi ya wananchi
katika nyoyo zao. Akiwa India Rashad alishuhudia jinsi Mohamed Ali Jinnah na
Mahatma Ghandi walivyokuwa wakiwahamasisha watu dhidi ya ukoloni wa Waingereza.
Bamanga alivyokuwa Kenya
alishuhudia uadui ambao wananchi walikuwa wanaonyesha kwa Waingereza lakini hali
ya siasa Zanzibar
ilikuwa kidogo tofauti. Zanzibar
madaraka ya serikali yalikuwa yamejigawanya kati ya Sultan na serikali ya
Uingereza. Lakini kwa hakika hasa madaraka halisi alikuwanayo British Resident
wakati Sultan alikuwa tu pale akionaekana kama
mfano wa utawala akiwa hana madaraka yoyote ilhali utawala wa nchi ulikuwa
chini ya Mwingereza. HK ilikuwa na malalamiko ya kiuchumi dhidi ya wamiliki wa
ardhi. Hiki chama kilichokuwa kikichipuka kilikuwa kikiwaeleza wakulima wajione
kuwa wao tabaka maalum lililokuwa likinyonywa na matajri. Wakati ule watu wengi
wa tabaka la chini walikuwa wameajiriwa kama vibarau katika mashamba ya karafuu
na minazi yaliyozagaa Zanzibar .
Kazi
ya kuchuma karafuu visiwani ilikuwa kama
kiwanda hasa kinachoajiri kwa kuwa karafuu ilikuwa inatoa ajira kwa Waafrika
walio wengi na hivyo kuwawezesha watu kujikumu.
Ikawa
wakulima wanafahmishwa kwa lugha nyepesi sana
vipi wanadhulumiwa. Walikuwa wakieleza kwa. Waingereza wakawa wameachwa pembeni
kwa kuonekana wao walikuwa ni watawala, hawamiliki chochote katika mali zilizokuwa
visiwani. Ikawa kwa njia hii Waingereza kupitia kwa British Resident wakawa
hawaonekani kama wanatishia ustawi wa walio wengi.
Viongozi
wa HK wakawa wanawauliza wakulima wajiulize hivi mali yote ile wanayoifanyika
kazi inakwenda wapi mpaka lini wao watendelea kukaa kimya huku wananyonywa.
Ikawa watu wanaona shida zao katika ule utajiri uliokuwa katika mitaa ya Zanzibar ikawa sasa Waarabu wanaonekana kama
wahamiaji na wanyonyaji badala majirani
mtaani.
Baada
ya kuungwa mkono Rashad na Kharusi wakatunga shairi kuonesha jinsi wananchi
walivyokuwa wakinyonywa na shairi likachapwa katika tayari kwa kusambazwa.
Shairi lilionyesha kwa mizania ya kazi inayofanywa na kile kipato cha
wafanyakazi. Mantiki ilikuwa kuonyesha kiasi cha unyonyaji uliokuwa ukifanyika.
Ikutumiwa lugha nyepesi shairi
lilionyesha mkwezi anaeajiriwa kuangua nazi inabidi apande mnazi ambao ni mrefu
kwa mita kadhaa kazi ambayo ni ya hatari kwa hali yoyote ile. Mshahara wa mtu
huyo ni kiduchu, senti tano ukiinganisha na fedha atakazopata tajiri baada ya
kuuza nazi au mbata. Shairi vilevile likasisitiza ukweli kuwa mfanyakazi hana
kinga endapo atakufa au kuumia kazini. Shairi likahitimishwa kwa kibwagizo kuwa
endapo madai ya wananchi hayatatekelezwa serikali isiwalaumu watu wa Zanzibar kwa kile
watakachofanya.
Kwa
hali yoyote ile kama siasa zilivyokuwa
Zainzibar kwa wakti ule karatasi ile ilikuwa ni ya uchochezi. Namna jinsi
makaratasi yake yalivyosambazwa ilitoa hisia kuwa chama kile cha siri kilikuwa
kimejipanga vyema na kimeenea kikigusa kila upande wa kisiwa. Ilikuwa
inashangaza kuwa waliopokea makaratasi yale hawakuweza kuwatambua waliowapa.
Jambo hili likazidi kuongoza mshangao katika kadhia ile ya makaratasi. Ili kuongeza mshawasha katika usambazaji wa makaratasi
wale waliochaguliwa kugawa makaratasi wakajibadili tokea mavazi hadi sura.
Kuhakikisha kuwa hakutakuwa na uwezekano wa kutambulika mwanaharakati wa Mwera
alikwenda kugawa Tunguu, wa kutoka Tumbatu alikwenda kugawa Mjini na wa Mjini
alikwenda Vikokotoni, Kizimkazi, Makunduchi na kwengineko. Namna hii ikawa
vigumu kuweza kuwatambua wale waliogawa
makaratasi yale. Baadhi ya makaratasi yalikuwa yametumbukizwa katika madirisha
ya magari ya Wazungu waliokuwa wakifanya kazi katika idara mbalimbali na
nyingine zilitumbukizwa katika madirisha ya nyumba. Lakini ili Ahmed Rashad na
Bamanga wajikinge ili wasihisiwe kuwa ndiyo wao waliofanya mambo yale kuepuka
kukamatwa ilibidi wapate ushahidi utakaowatoa katika dhima ile.
Mwingireza
mmoja aliyeitwa Money alikuwa afisa mstaafu. Baada ya kufanya kazi katika
serikali ya Zanzibar
alistaafu na kuamua kulowea kisiwani.
Money au Mr. Money kama watu walivyozoea
kumwita alikuwa shushushu – mpashaji habari wa serikali. Alikuwa akijichanganya
na Waafrika na alikuwa akitembea sehemu nyingi wanapokutanika watu. Mr Money
akiwajua Rashad na Bamanga. Usiku wa
siku ile ya Jumamosi siku waliyopanga kutawanya yale makaratasi iliamuliwa kuwa
Rashad na Bamanga waende nyumbani kwa Mr. Money kwa mazungumzo na kuburudika.
Huu ndiyo itakuwa kinga yao .
Rashad akamsubiri Bamanga lakini Bamanga hakutokea kama
walivyoahidiana. Alipotokea alikuwa na kikapu kimejaa makaratasi tele. Siku ile
wote walikuwa na mwambo hivyo hawakuwa na fedha kwa ajili ya matumizi ya jioni
ile. Rashad akatoa wazo kuwa waende kwa ndugu yake Rashad mama mmoja Prince
Sayyid Soud wakachukue fedha.
Walipofika
nyumbani kwa Sayyid Soud nyumba ilikuwa ya ghorofa, Rashad akamwita ndugu yake akiwa
chini ngazini. Sayyid Soud akamwambia apande juu. Bamanga alibaki chini
kajificha gizani. Kulikuwa na sababu hakutaka mwana wa mfalme amuone. Kulikuwa
na uadui kati ya koo zao. Vijana wane kutoka ukoo wa Kharusi walimpiga Sayyid
Soud na hii ikasababisha uhasama baina ya koo hizo mbili. Sayyid Soud akataka
kujua Rashad kafuatana na nani aliyemwacha chini. Rashad akamwambia ni Bamanga.
Sayyid Soud akakasirikia Rashad akamkumbusha ndugu yake kuwa akina Kharusi ni
adui zao. Rashad akamtuliza ndugu yake akamwambia kuwa alipogombana na akina
Kharusi Bamanga alikuwa Nairobi
na hakuhusika kwa namna yoyote na ugomvi ule. Akamweleza kuwa Bamanga
alisikitishwa na ugomvi ule na itakuwa si haki kumuhusisha. Bamanga akapanda
juu na kikapu chake kimejaa makaratasi. Sayyid Soud alikiona lakini hakuuliza
kitu.
Kushoto kwenda kulia Ahmed Rashad Ali, Dk. Harith Ghassany na Mohamed Said nyumbani kwa Mzee Rashad Upanga |
No comments:
Post a Comment