Tewa Said Tewa 1924 1998
Mmoja wa Waasisi wa TANU
Aliyesimama wa pili kutoka kulia ni Tewa Said Tewa akiwa katika Baraza la Mawaziri wa serikali ya kwanza 1961 |
Waliosimama kushoto kwenda kulia: Abduliwahid Sykes, Tewa Said Tewa Waliokaa wa mwisho kulia Chief Abdallah Said Fundikira Wakiwa Makka Hijja 1964 |
Uncle Saleh with the East Africa Muslim Welfare delegation. Saleh bin
Madhi hosted them when they came to Saudi Arabia. In the same trip,
uncle Saleh and the delegation met with the Saudi king to gain his
support. The king offered his complete support. Nyerere fearing the
rise and influence of the Muslim association promptly broke it up. In
the picture, uncle Saleh is seated next to Chief Fundikira of Tabora,
the chief of the Nyamwezi tribe, who also served as the Minister of
Justice for Tanzania. In the top left, Abdulwahid Sykes who fought for
Tanzania's independence and was pegged to be the first president of
Tanzania. He chose his friend Nyerere to be the first president and
provided all the moral and financial support for it to become a
reality. The others in the photograph are ministers who were serving
as delegates.
Baada ya kishindo kile Tewa
sasa akajikita katika kuhakikisha kuwa anafanikisha ujenzi wa Chuo KIkuu Cha
Waislam. Lakini hakufanikiwa kwani ghafla akajikuta yuko katikakati ya kile
kilichokujajulikana kama “mgogoro wa EAMWS wa mwaka 1968” mgogoro ambao
ulidumu kwa takriban miezi mitatu na mwishowe serikali ikakipiga chama kile marufuku
na Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa usiku wa manane kurudishwa kwao Unguja na
BAKWATA ikaundwa kushika nafasi ya EAMWS. Ujenzi wa Chuo Kikuu na mradi wa
kujenga shule za msingi na upili ambazo Tewa alikuwa akizisimamia chini ya
EAMWS vyote vikafa. Kwa kipindi kirefu kuanzia mwaka 1968 Mzee Tewa aliishi
maisha ya upweke hadi miaka ya 1990 kwa sababu ya mwelekeo mpya wa siasa Mzee
Tewa alianzisha taasisi iliyokuja kujulikana kama Muzdaliffa Muslim Academy
iliyokuwa na makao yake makuu Msikiti wa Manyema, Dar es Salaam.
6 Oktoba 2011
Madhi hosted them when they came to Saudi Arabia. In the same trip,
uncle Saleh and the delegation met with the Saudi king to gain his
support. The king offered his complete support. Nyerere fearing the
rise and influence of the Muslim association promptly broke it up. In
the picture, uncle Saleh is seated next to Chief Fundikira of Tabora,
the chief of the Nyamwezi tribe, who also served as the Minister of
Justice for Tanzania. In the top left, Abdulwahid Sykes who fought for
Tanzania's independence and was pegged to be the first president of
Tanzania. He chose his friend Nyerere to be the first president and
provided all the moral and financial support for it to become a
reality. The others in the photograph are ministers who were serving
as delegates.
Tewa Said Tewa ni mtoto wa
Dar es Salaam. Mimi nimekuwa nikimuona toka utoto wangu na kumbukumbu zangu za
awali kabisa za Tewa Said Tewa ni kumuona Mtaa wa Pemba akiwa ndani ya gari
lake la Kiwaziri Humber nyeusi. Nilikuja kumfahamu vizuri sasa mimi nishakuwa
mtu mzima na nikawa karibunae sana kiasi alinieleza historia yake yote ya
maisha yake katika siasa kuanzia kuupigania uhuru hadi alipokuwa waziri na
mwisho wa kuangushwa kwake kutoka uongozi. Mzee Tewa akawa mwalimu wangu katika
kuzijua siasa za Dar es Salaam ya mwaka 1950 wakati wa kudai uhuru na siasa
zilizokuja kutamalaki baada ya uhuru kupatikana. Tewa Said alikuwa na umbo la
kupendenza na sura jamil. Tewa Said alikuwa mvazi mzuri. Tulikuwa tukikaa
kwenye veranda yake nyumbani kwake Magomeni Mikumi akinifungulia album yenye
picha zake akiwa kijana wakati waziri wa serikali, balozi China na Rais wa East
African Muslim Welfare Society (EAMWS). Nilipendezwa na zile suti zake.
Picha zake kwa jumla zikimwonyesha katika baraza la kwanza la mawaziri na picha
nyingine akiwa katika shughuli tofauti. Hakika ukItazama picha zile utasema ule
ulikuwa wakati wa enzi zake.
Tewa Said Tewa Katika Mkutano wa Kimataifa (Picha Kwa Hisani ya Mwanae Said Tewa) |
Alipofariki dunia mwaka 1998
mimi sikuwapo Dar es Salaam nilikuwa nje ya nchi kwa hiyo sikuhudhuria maziko
yake. Kitu cha kushangaza ni kuwa kwa kile kipndi cha takriban mwezi mmoja
nilipokuwa sipo Tanzania watu maarufu watatu waliopigania wa Tanganyika walifariki
kwa kufuatana mmoja baada ya mwingine, Dossa Aziz, Zuberi Mtemvu na Tewa Said
Tewa. Kwa haraka niliporejea nchini nilipitia magazeti kuangalia taazia
zilizoandikwa kuhusu watu hawa. Nilisikitika sana kwani hapakuwa na taazia
yoyote ya maana na aliyeandikiwa taazia alikuwa mmoja tu nae ni Dossa Aziz na
walioandika taazia ile ilioenesha walikuwa hawamjui Dossa. Zuberi Mtemvu na
Tewa Said hawakuandikiwa taazia yoyote. Nilinyanyua kalamu na kuwaandikia
taazia stahili yao hao wote na zote zilichapwa katika magazeti. Hawa wote
walikuwa wazee wangu wakinifahamu si mimi tu bali hata wazazi wangu.
Tewa ni mmoja katika wale
wazalendo 17 walioasisi TANU lakini katika picha ile maarufu ya waasisi wa TANU
yeye na Ally Sykes hawamo. Sababu ya kutokuwepo kwao ni kuwa wao walikuwa
wanyakazi wa serikali na kuna na Government Circular No. 5 ya serikali ya
kikoloni hawakuwa na ruhusa ya kujiingiza katika siasa. Tewa ni kati ya watu wa
mwanzo kumpokea Nyerere na kufahamiana na Nyerere alipokuja Dar es Salaam mwaka
wa 1952. Tewa alikuwa mwanachama wa kikundi kilichojiita Wednesday Tea Club
ambacho kiliwajumuisha vijana wa wakati ule waliokuwa katika TAA na kazi kubwa
ya kikundi hiki ilikuwa kukutana nyumbani kwa Abdulahid au Dossa kila siku ya
Jumatano kunywa chai pamoja na kupiga siasa. Kwa ajili hii Tewa alishuhudia
yote katika harakati za kudai uhuru kwa macho yake si kama mtazamaji bali kama
mchezaji wa kikosi cha kwanza.
Mzee Tewa akinihadithia
habari za Julius Nyerere anasema kuwa alifuatwa na Abdulwahid Sykes usiku
nyumbani kwake Mtaa wa Pemba siku moja kabla ya kufanya uchaguzi mkuu wa TAA wa
mwaka 1953 uliomwingiza Nyerere katika uongozi wa TAA. Tewa anasema Abdulwahid
alikwenda kwake kwa minajili ya kuzungumza kuhusu uchaguzi ule ambao yeye
Abdulwahid Sykes alikuwa anapambana na Nyerere. Jinsi mipango ilivyokuwa
imepangwa uchaguzi ule ilikuwa sawa na kukamilisha ratiba ya mkutano tu kwani
viongozi wa juu wa TAA, yeye mwenyewe Abdulwahid, Ally, Dossa na John Rupia
walikuwa wamekubaliana kuwa Nyerere apewe nafasi ile kwa Abdulwahid
kumpisha kiti. Mara nyingi sana Mzee Tewa kila tukizungumza habari za Nyerere
na TANU alikuwa akikirudia kisa hili kama vile kasahau kuwa alinishanieleza.
Tewa anasema, “Abdulwahid alikuja kwangu usiku na akaniambia kuwa Tewa, kesho
tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii. Kuanzia
hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya kumnyang’anya
madaraka tuliyompa. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu
kitakwenda sawa.” Mzee Tewa alikuwa akisema kuwa, “Abdulwahid ndiye
aliyechelewesha kuundwa kwa TANU. Ilikuwa TANU tuiunde toka 1950 na tungefanya
vile Nyerere asingetuwahi angekuwa keshachelewa lakini Abdu kwa miaka minne
mfulululizo alikataa kuitisha mkutano wa TAA hadi 1954. Kila tukimwambia habari
ya mkutano anasema tusubiri mambo bado.”
Mzee Tewa alikuwa mwalimu
wangu na hivi niandikapo ni kama vile namuona na mimi kama mwanafunzi anaetaka
kuonekana hodari sikuacha kumvurumishia maswali. Nilimuuliza,“Hivi baba
inawezekanaje mtu mmoja akasimamisha kuitishwa kwa mkutano wa chama?” Mzee Tewa
alinijibu kwa kusema, “Abdu alikuwa na akili sana na sisi sote tukimtegemea
yeye katika uendeshaji wa chama lakini kikubwa zaidi ni kuwa tukimtegemea zaidi
katika kufadhili mambo mengi ya chama. Sasa yeye akisema tusubiri ilibidi iwe
hivyo. Hawa akina Sykes katika TAA na TANU walikuwa na nguvu sana maana licha
kuwa viongozi walitoa fedha zao kupambana na Waingereza na hilo toka enzi ya
baba yao.
Tewa Said baada ya kupatikana
uhuru mwaka wa 1961 na sasa akiwa waziri wa serikali, mwaka wa 1962
alishiriki katika kuitisha mkutano uliokujajulikana kama Muslim Congress. Tewa
Said alihusika sana katika kufanikisha mkutano huu. Mkutano huu ulihudhuriwa na
jumuia zote za Kiislam zilizokuwapo wakati ule kama East African Muslim Welfare
Society (EAMWS), Daawat Islamiyya, Jamiatul Islamiya fi Tanganyika na Muslim
Education Union. Mkutano huu uliamua pamoja na mambo mengine kuanzisha idara ya
elimu chini ya EAMWS. Mkutano huu ulitayarisha mipango ya kujenga shule Tanganyika
nzima na mwishowe kujenga Chuo Kikuu cha kwanza kwa Waislam katika Afrika ya
Mashariki. Mkutano ule ukamchagua Tewa Said Tewa kuwa mwenyekiti wa EAMWS kwa
upande wa Tanganyika. Kwa kitendo hiki nyota ya Tewa ikazidi kung’ara si
Tanganyika tu bali Afrika ya Mashariki nzima. Wenzake katika harakati hizi
maarufu sana alikuwa Badru Kakunguru wa Uganda na Prince karim Aga Khan. Lakini
Mzee Tewa alinieleza ushindi ule wake na usuhuba wake na watu mashuhuri kama
hawa ukaja kumsababishia matatizo makubwa baadae.
Nakumbuka kama jana vile siku
Mzee Tewa aliponieleza kisa hiki. Alinyanyuka pale tukipokuwa tumekaa akaingia
chumbani kwake akatoka na jalada akanikabidhi akisema, “Mohamed haya
niliyoandika humu sijamwonyesha yeyote wewe utakuwa mtu wa kwanza kusoma maisha
yangu ya siasa. Tafadhali nenda na jalada hili kasome kisha unirudishie.” Iko
siku kaja mtu kwangu akanambia, “Mohamed, Mzee Tewa anasema anakupenda sana na
akashangaa anasema hayo mapenzi yake kwako ni maajabu ya Mwenyezi Mungu kwani
yeye na baba yako hawakuwa na mkabala mwema toka utoto wao lakini ajabu wewe
mwanae umekuja kuwa rafiki yake.” Maneno haya aliyasema Mzee Tewa
alipofikishiwa habari za kifo cha baba yangu na huyu mpashaji habari wangu.”
Nilisoma lile jalada na kwa kweli niliyokuta mle yalinikosesha raha sana.
Nilianza kumtazama Mzee Tewa sasa kwa sura nyingine kabisa na mapenzi
yangu kwake yakazidi kupita kiasi.Ikawa sasa nimepata tafsriri halisi ya
maneno, “siasa ni mc mchezo mchafu.” Mzee wangu Ahmed Rashad Ali yeye akiongeza
akisema,”Jinsi unavyokuwa mchafu zaidi ndiyo unavyokuwa bingwa.” Insha Allah iko siku nitakuja andika
na kuyaweka wazi kwa ajili ya faida ya kizazi kijacho mengi alonambia Mzee Tewa
na yale niliyosoma katika lile jalada lake alilonipa.
Mwaka 1964 Tewa Said Tewa
aliongoza ujumbe wa EAMWS akifuatana na Mufti wa Tanganyika na Unguja Sheikh
Hassan Bin Amir na Sheikh Said Omar Abdallah, maarufu kwa jina la Mwinyibaraka
(Mwinyibaraka alikuwa msomi wa Chuo Cha Oxford, Uingereza), Aziz Khaki na
wengineo wakafanya ziara ya nchi za Kiislam na walionana na Gamal Abdi Nasser
ambae aliwapa msaada wa kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam, Tanzania. Huyu Aziz
Khaki alikuwa mtu muhimu sana katika EAMWS yeye alikuwa katibu lakini zaidi
alikuwa kama mwakilishi wa Aga Khan ndani ya jumuia hiyo. Mwalimu Nyerere
alialikwa katika sherehe ya kuweka jiwe la msingi la Chuo Kikuu na yeye kwa
mkono wake ndiye aliweka jiwe lile akiwa katika ya Tewa Said Tewa na Sheikh
Hassan bin Amir. Sherehe ilikuwa kubwa na mabalozi wa nchi zote za Kiislam walihudhuria
sherehe ile. Haukupita muda Tewa Said Tewa Nyerere akamtoa Tewa katika baraza
la mawaziri na kumfanya balozi wa Tanzania China. Hii ilikuwa mwaka 1965.
Tewa
inaelekea hakuipenda nafasi ile akajiuzulu na kurudi nyumbani kushiriki katika
uchaguzi mkuu wa mwaka ule. Katika uchaguzi ule wa mwaka 1965 ambao Bibi Titi aligombea wote Bi Titi
na Tewa walianguka tena kwa kushindwa na watu ambao wala hawakuwa maarufu wala
hawakuwa na nguvu yoyote ya siasa. Bibi
Titit alibwagwa na mtu mmoja
akijulikana kama A. M. Mtanga na Tewa akaangushwa na mtu aliyeitwa na Ramadhani Dollah. Huyu Dolla alikuwa
mbunge kwa kipindi kimoja uchaguzi wa 1970 aliangushwa na mwisho aliishia jela.
Tewa Said Tewa na Mwenyekiti Mao Tse Tung wa China (Picha Kwa Hisani ya Mwanae Said Tewa) |
Kushoto: Tewa Said Tewa, Gamal Abdel Nasser na Chief Abdallah Said Fundkira (Picha Kwa Hisani ya Mwanae Said Tewa) |
Kipindi cha miaka ya 1990
kilikuwa kipindi kigumu kwa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi kuliibuka
migogoro mingi ya kidini. Sasa watu waliopata kuwa viongozi katika taasisi za
dini walijaribu sana kutoa michango jinsi ya kuyaendea haya matatizo. Mzee Tewa
alijitokeza sana katika kutoa mchango wake. Mwaka
1991 Kanisa Katoliki katika kuadhimisha miaka 25 ya “World Peace Day”
walifikisha salamu zilizotoka kwa Papa na aliyezfikisha salamu zile kwa Waislam
wa Tanzania alikuwa Balozi wa Papa Tanzania, Monseigneur Agostino Machetto
akifuatana na Secretary of the Apostolic, Father Gabriele Gaccia na Father
Peter Smith. Tewa Said Tewa ndiye aliyepokea salamu hizi kwa niaba ya
Waislam wa Tanzania. Picha za sherehe hii ilipamba magazeti yote. Inaelekea
Tewa Said Tewa hakuwa na bahati na uongozi mara zikatokea vurugu za kuvunjwa
mabucha ya nguruwe mjini Dar es Salaam na serikali ikapiga marufuku taasisi
zote za Kiislam isipokuwa BAKWATA na Tewa akarudia tena maisha yake ya upweke.
Mara nyingi nilipokwenda
nyumbani kwake kumsalimia nilimkuta mnyonge na mwenye fikra lakini hakuacha
kuniombea dua na kunihimiza nisiwache kumtembelea. Akiwa katika hali kama hii
siku moja akanipa jalada lingine nikasome. Ilipigwa na butwaa. Mzee Tewa
alikuwa amefasiri kutoka kwa Kiingereza kuja Kiswahili “Homer” na “Ulysses.”
Mzee wangu Tewa Said Tewa alipofariki nilikuwa niko nje ya Tanzania na habari
za kifo chake kilifikia kwa wakati. Nilisikitika sana hasa nikikumbuka nyakati
nilizokuwanae faragha pale nyumbani kwake Mikumi akinisomesha siasa za nchi
yetu na kunihadithia madhila yaliyomkuta kwa ajili ya kuutumikia umma kwa
uadilifu. Miaka miwili iliyopita nilikuwa naandika kitabu na nikahitaji picha.
Nilipokwenda kuwaona watoto na wajukuu wa Mzee Tewa kuomba picha hakuna aliyekuwa
anajua maktaba ya mzee wao iko wapi. Nilionyeshwa picha moja tu ya Tewa
iliyotundikwa ukutani iliyopigwa Makka mwaka wa 1964 wakati Tewa alipokwenda
hija. Nilijaribu kuwaongelesha kuhusu mzee wao na kwa masikitiko makubwa
nilikuja kubaini kuwa vijana wale hawakuwa wanajua chochote kuhusu huyu shujaa
wa uhuru wa Tanganyika.
Mohamed Said
1 comment:
Mwenyeezi Mungu amlaze pahali pema peponi. Baba yetu mpenzi Tewa Said Tewa . Ameen
Na hao waliodhani wataishi milele duniani Mwenyeezi Mungu atawa............
Post a Comment