Wednesday, 8 January 2014

Madina Yakatazwa Kuwa Sehemu ya Makazi Kwa Amri ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa



Sheikh Deep Throat

Nyaraka Kutoka Madina

Nyaraka zimefika Dar es Salaam zinazoonyesha kuwa wakazi wa Madina kijiji kilichovamiwa kwa kisingizio kuwa kilikuwa na uhusiano na Al Shabab wamelazimishwa kuweka sahihi makubaliano kati yao na uongozi wa kata ya Negero kuhama eneo hilo kwa kuwa haparuhusiwi kuishi watu. 

Kutokana na nyaraka hizo amri hiyo imetoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Galawa. 

Nyaraka inaonyesha kuwa waliotilishwa sahihi amri hiyo ya kuondoshwa Madina ni Muhamadi Mwandalo na Salimu Mwalimu na viongozi waliotia sahihi kwa niaba ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Negero ni Paul A. Mnyeke na Ramadhani A. Mwamilinga. 

Nyaraka ina muhuri wa Afisa Mtendaji Kata Negero.

Makubaliano hayo yanasema wanakijiji hao wamepewa siku 10 kuishi Madina kuanzia tarehe 19 hadi 24 Desemba 2013 wawe wameshaondoka Madina na wamevunja nyumba zao na kuondoa vifaa vyao.

Makubaliano hayo yanataka nyumba ziwe zimevunjwa ingawa nyumba zilishavunjwa siku nyingi na vifaa vya wanakijiji hao kupotea katika uvamizi ule.

Makubaliano hayo nyaraka inaonesha yalifanywa tarehe 17 Desemba 2013.

Manazi wa Kijerumani waliwafanyia dhulma mfano wa hii Wayahudi wakati wa Vita Kuu Vya Dunia.

Wanasheria wanaweza kusaidia katika dhulma hii.

Kuna wanavijiji waliondoka Madina zamani kwa sababu mbalimbali.

Kijiji kiliposhambuliwa na kesi kufunguliwa dhidi ya Waislam Mahakama ya Handeni wakazi hawa waliohama walikuwa kimya na walipozungumza walitoa  picha iliyokuwa wakati mwingine inamtisha msikilizaji.

Taratibu baada ya kusikia kuwa nyumba zimevunjwa na kuchoma moto na ardhi zao sasa wananyang'anywa wameanza kuhaha kutaka kujua kulikoni.

Wanazungumza kuhusu mali zao na mashamba yao na viwanja vyao na ardhi zao.

Kubwa sana na hili wengi hawakuwa wanalijua wanazungumza kuhusu machimbo ya dhahabu huko Madina...waliyokuwa wakimiliki kihalali na nyaraza za umiliki wanazo...

Halikadhalika tumepokea hapa ujumbe mkali kuwa hawa Waislam wa Madina hawastahili kuhurumiwa na kutetewa...

Jibu limekuwa wanastahili kuhurumiwa na kutetewa kwani hata kama tujaaliwe walikuwa katika makosa hapakuwa na sababu ya kuuliwa na nyumba na misikiti yao kuchomwa moto.

Ilikuwa hawa ''wakosaji'' wakamatwe wapelekwe mahakamani.

Anaetaka kujua zaidi kuhusu hili na atembelee Ubao.

Ukurasa huu uko wazi kusikiliza yanayoanza kujitokeza kutoka Madina.

Unaweza kufatilia sakata ya Madina katika ''SHEIKH OMAR MOHAMED AZUNGUMZIA MAUAJI YALIYOTOKEA HANDENI.'' (Gallery)

PS:
'The one who got away...''
Huko ndiko kunakotoka taarifa hizi kwa staili ile ya ''Deep Throat.''

Huyu Deep Throat ndiye aliyekuwa anatoa taarifa za siri katika kashfa ya Watergate.

Nadhani mmenielewa.

PS: Deep Throat amekufa kama miezi miwili iliyopita.


1 comment:

Heri Hatibu said...

Maa shaa Allahu, tunakushukuru sheikh kwa kutujuza mambo muhimu na mazito yanayojiri ndani ya nchi yrtu.