Monday, 13 January 2014

Mauaji ya Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wa Kijiji cha Madina - Simulizi ya Maziko Yao

11 Mfungo Sita 1435

Fatilia kwa makini ukurasa huu In Sha Allah...
Tunatengeneza...

Allah SW katufunza anasema: ''Msidhulumu wala msikubali kudhulumiwa.''
Haya ndiyo mafunzo ya Uislam.

Mtume SAW katuambia: ''Dhulma haidumu na ikidumu huangamiza.''

Mtume SAW anasema, ''Iogope dua ya aliyedhulumiwa kwani haina pazia.''

Mauaji ya Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wa Kijiji cha Madina 

Tarehe 25 Oktoba 2013 siku ya Ijumaa Waislam katika kujiji cha Madina walishambuliwa  na askari na Waislam wawili waliuawa kwa kupigwa risasi.

Waislam hao ni Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir.

Hamisi Ramadhani amezikwa Handeni katika makaburi ya hospitali maiti ilipokuwa imehifadiwa.

Abu Zubeir maiti yake ilihamishwa kutoka Handeni kwa kuwa hospitali haikuwa na chumba cha barafu cha kuhifadhi maiti ikapelekwa Korogwe.

Ndugu zake Abu Zubeir waliogopa kujitokeza kuchukua maiti yake kwa kuwa askari walikuwa wakimkamata kila aliyefika hospitali kuuliza taarifa za maiti hao.

Haijulikani nani wamemzika Abu Zubeir na hadi sasa ndugu zake hawajajitokeza kujua ndugu yao kazikwa wapi kwa hofu ya kukamatwa.

Sheikh Waziri anasema yeye na wenzake walikabidhiwa maiti ya Hamisi Ramadhani siku ya Jumapili na siku hiyo hiyo walimzika katika makaburi ya hospitali sanda yake ikiwa shuka ile iliyofunika maiti yake.

Sheikh Waziri anasema juu ya kuwa maiti zile zilikuwa hazikuhifadhiwa katika baridi hali ya maiti ilikuwa nzuri kabisa.

Mashuhuda wa kifo cha Hamisi Ramadhani wanasema alipopigwa risasi Hamisi Ramadhani alishahadia kwa sauti na kila mtu alisikia shahada ile.

Allah awalaze mahali pema peponi.
Amin.

Maelezo Mafupi ya Sheikh Waziri Shuza

Siku ile ya mashambulizi tarehe 25 Oktoba 2013 Sheikh Waziri akiwa kama kiongozi wa Waislam alipigiwa simu yeye akiwa Mkata katika shughuli za biashara kujulishwa kuwa kuna watu wameuawa kwa hiyo akaombwa aende Hospitali ya Wilaya Handeni akaagalie waliouawa na majeruhi.

Taarifa zilizomfikia alipofika Handeni jioni ile zilikuwa taarifa za kuogofya.

Hali pale hospitali ilikuwa ya kutia hofu palikuwa na ulinzi mkali hospitali nzima imezungukwa na maaskari. Kwa ajili hii Sheikh Waziri hakuweza kwenda hospitali siku hiyo na hata siku ya pili yaani Jumamosi hakuweza kwenda.

Waislam walibakia majumbani kwao wakisubiri na kuomba dua.

Sheikh Waziri akiwa kiongozi wa alipiga marufuku shura ya aina yoyote msikitini kuhusu mauaji yale kutafuta salama.

Waislam walikuwa wanakuja kuswali na wakimaliza wanaondoka kurudi majumbani kwao.

Lakini Sheikh Waziri akawa na wasiwasi kuwa ikiwa hatafanya jambo kuna hatari ya wale marehemu kutozikwa Kiislam.

Sheikh Waziri ilipofika Jumapili ikamjia fikra ya kumpigia diwani Mushashi. Alimweleza diwani huyu kuwa Waislam wangeshukuru kama serikali wangeruhusu maiti zile wapewe ili wazizike.

Haukupita muda diwani akamfahamisha Sheikh Zuberi kuwa anaweza kwenda hospitali na kuonana na Mganga Mkuu kwa ajili ya kupewa zile maiti mbili.

Lakini Mganga Mkuu akasema kuwa amri aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Bi. Chiku Galawa ni kuwa maiti zile zipelekwe Tanga kwa mazishi ikiwa ndugu zao hawajajitokeza na huko maiti hizo zitachangwanywa na maiti nyingine za wasio na ndugu na zitazikwa na serikali.

Ikawa sasa lazima Mkuu wa Mkoa asubiriwe ili abatilishe amri yake ya awali na endapo ruksa itatoka Waislam wa Handeni watazizika maiti hizo.

Sheikh Hamisi akaondoka kusubiri amri ya Mkuu wa Mkoa.

Mwishowe maiti ilitolewa kwa Sheikh Waziri baada ya mazungumzo marefu kati ya Mganga Mkuu na Sheikh Waziri ikizingatiwa kuwa kwa siku tatu hakuna ndugu wa marehemu aliyejitokeza kuchukua maiti.

Sheikh Waziri alifunuliwa maiti ya Hamisi Ramadhani na Mganga Mkuu mbele ya askari.akaonyeshwa jeraha la mguuni alipopigwa risasi.

Shuka haikufunuliwa kuoneshwa majeraha mengine...
Sheikh Waziri hakuwa na haja ya kutaka mengi lililomshughulisha ilikuwa ni kupata maiti ili waisiitiri.

Sheikh Waziri  anasema ilikuwa wazi kuwa Polisi na Mganga Mkuu walikuwa wameshakubaliana nini cha kufanya wakati watakapoonyesha maiti kwa ndugu zao.

Mganga Mkuu alionyesha jeraha la risasi mguuni akisema kuwa hapo ndipo zilipotoka damu nyingi kusababisha kifo cha Hamisi Ramadhani.

Lakini wao walikuwa na habari kamili kutoka kwa mke wa marehemu na jamaa wengine kuwa ndugu yao alikuwa amepigwa risasi katika kibofu cha mkojo na kwa hakika sehemu ile ingawa ilikuwa imefunikwa na shuka palikuwa na uvimbe mkubwa.

Sheikh Waziri na Waislam wachache walimzika ndugu yao usiku katika makaburi hapo hospitalini.

Insha Allah Sheikh Waziri atasikika kwa kauli yake akieleza msiba huu...
Fatilia hapa hapa:
Photo
Moja ya Nyumba Zilizovunjwa  Negelo
Photo
Add caption

Mwandishi akimhoji Sheikh Waziri Shuza Kiongozi wa
Ansar Handeni Kuhusu Kushiriki Kwake Katika Kumzika
Waziri Ramadhani aliyeuawa Madina Wakati Askari Waliposhambulia
Waislam Msikitini



Msikiti wa Ansar Handeni

Alfajr Maulid Day 12 Mfungo Sita 1435
Kituo cha Mabasi Ngamiani Tanga
Mwandishi akielekea Handeni


Ingia Kwenye Gallery Usikilize Simulizi za Maziko ya Waislam Waliouawa Madina


No comments: