Friday, 3 January 2014

UBAO WA YANAYOJIRI, SALAAM, UKUMBUSHO NA YATOKANAYO

''Naanza Audhu Billahi, kumlaani shetani.
Napiga na Bismillahi, Kumuomba Rahmani.
Iwe njema asubuhi,
na siku yenye amani. Ulitakalo uwahi,
Ili uwe furahani.
Kwa Radhi za Mursali, Mtume wetu Amini. Ung'are wako wajihi, akhera na duniani.
Ameen ya Rabb,
JUMA'A MUBARAK''


Nadir Mahfoudh Mkurugenzi Mkuu Al Noor Charitable Agency, Zanzibar



Sheikh Omar Wazir alikuwa anapita njia akawakuta ndugu zake wanajenga Msikiti.
Na yeye akaingia ili zisimpite. Huyo aliyepiganae picha ndiyo Imam.
 Picha kwa hisani ya Sheikh Omar


Sheikh Omar Wazir: 


A Alaykum, 

Tacloban ni kisiwa kimoja kati ya vingi vilioko katika nchi ya Philippines. 

Kwa bakhti mbaya ndicho kilichoathirika zaidi na Typhoon Yolanda . maelfu ya wakaazi wa kisiwa hiki wamepoteza maisha yao na wengi kukosa makaazi ya kudumu. 

Nimebakhtika kuwa nipo katika team ya wanaoshughulikia misaada ya namna mbali mbali kusaidia walioathirika na kimbunga hicho. 

Nikiwa narudi kazini hii ni wiki yangu ya pili kuweko hapa ,ambako wiki za kabla nilikuwa visiwa vyengine nakutana na Waislamu ambao wanaujenga msikiti wao ambao umebomoka wote kwa njia ya harambe. 

Nilikuwa na mwenzangu mwenye asli ya Kipalestine ambae hisia zake zilikuwa na juu zaidi tulipokutana na haya Mungu amjaze khair na imani zaidi kwa alioyafanya.

Mola awape imani na uwezo ndugu zetu hawa kuweza kuyakabil yaliomazito kwao hasa kwa vile nchi hii imezungukwa na wenye imani ya Kimishini kwa nguvu sana.

Wabillahi Taufik 


Kutoka kwa Sheikh Haidar Haidar 

Tunaheshimu sana juhudi kubwa zinazofanywa ndugu yetu mzee Mohammed Said  katika harakati muhimu za kutetea Uislamu na waislamu, Allah amlipe kwa juhudi hizo ila wakati huo huo tunampa angalizo katika harakati hizo ajitahidi sana kuandika habari zenye utafiti wa kutosha ili kubainisha ukweli halisi na kuepuka uchochezi.
Katika e mail kadhaa masiku ya  karibunili amejitahidi kuandika kadhia inayohusu vikundi vya waislamu wa huko kilindi na Madina wilayani Handeni  tunaamini lengo ni zuri katika kutetea Waislamu wa maeneo hayo lakini kwa kiasi amekosa taarifa za kutosha kuhusiana na vikundi hivyo ikiwemo misimamo na aqida zao.

Walikotokea
Vijana wengi wa kijiji cha  Madina wametokea jijini Dar es salaam Masjid Haq Buguruni na hawa wa Kilindi wanatokea Mabibo jijini Dar wengi wao walikuwa ni wafanyabishara wa soko la ndizi kule mabibo na walikuwa wakiswali Masjid Othman msikiti wa chuo cha taifa cha usafirishaji[NIT]chini ya Imamu Sheikh Jadu Rafii Mcheni walikuwa wakisoma darsa la awali pale...

Mauwaji na Uvunjaji wa Misikiti
Mzee Mohammed Said ni vyema uende ukamtembelee...



Photo
Baadhi ya Matofali Yaliyotoka Katika
Msingi wa Msikiti

Msingi wa Msikti Uliovunjwa Lwande na matofali yake kupelekwa kujenga
hospitali ya serikali



Bwana Chambuso
Mzee Mohammed Said umeandika habari za bwana mdogo Chambuso... Mzee Mohammed Said zingatia maelekezo ya Uislamu usipoteze muda wako...

Wabillah Tawfiiq
Ujumbe ulioletwa kwangu hapo juu kutoka kwa Sheikh Haidar ni mkali na ndiyo maana sikuwa na moyo wa kuuchapa hapa Waislam wakausoma.
Nimeweka hapa vipande vidogo tu vya ujumbe huo ili wasomaji waone lau kwa uchache kile kilichokusudiwa na Sheikh Haidar Haidar.



Asalaam Aleikum,

Sheikh Haidar nimekusoma kwa makini na nimeelewa yote 
uloandika.

Mimi nanwatetea hawa Waislam kwa kuwa tujaalie ni wakosa hapakuwa
na haki ya kuwaua na kuchoma nyumba na misikiti yao.

Makatoliki wana Wanamaombi lakini hawajapigwa wala kuchomewa nyumba.
Na kama kungekuwa na lolote ilikuwa wakamatwe wapelekwe mahakamani.

MS



  1. Kutoka kwa Mwalimu Hashim Saiboko

Assalaam Aleykum.

Nadhani haya yakuvunja haki za Waislamu yako sawa kwa mujibu wa sheria ya ugaidi.

Hii ni sheria tuliyoipinga kwa msingi kwamba kwa kutumia sheria hii askari anaweza kumuua  'gaidi' yaani Muislamu na asichukuliwe hatua yoyote. 

Bw. Muhammed Said msiba huu msingi wake ni huo. 

Na katika mapambano yetu tulenge pia kurudisha hadhi ya Waislamu kuwa nao ni binadamu na kuwa wanastahili kupewa heshima na haki wapewazo watu wengine.

***


Assalaam aleykum,

Nadhani haya yakuvunja haki za Waislamu yako sawa kwa mujibu wa sheria ya ugaidi. 

Hii ni sheria tuliyoipinga kwa msingi kwamba kwa kutumia sheria hii askari anaweza kumuua  'gaidi' yaani Muislamu na asichukuliwe hatua yoyote. 

Bw. Muhammed Said msiba huu msingi wake ni huo.

Na katika mapambano yetu tulenge pia kurudisha hadhi ya Waislamu kuwa nao ni binadamu na kuwa wanastahili kupewa heshima na haki wapewazo watu wengine.

***

Mohamed Said na Sheikh Chambuso

***


Elimu Bila Mipaka
Radio Imaan


Kipindi Cha Mwangaza Kwa Jamii
Kipindi cha Kila Jumapili Asubuhi

Mahojiano na  Aljazeera 2007
Chole Road Masaki, Dar es Salaam





Mbaya Kirilo alikuwa amesafiri amekwenda Nairobi

Aljazeera Producer |Amir
Voice of America, Washington DC, 2011


Tarehe 11 January 2014


Maulid ya Wanafunzi wa Al Marhum
Sheikh Ramadhani Abbas



Aljazeera Interview, Tanga 2008
Add caption

Mohamed Vaal wa Aljazeera Akimhoji Mwandishi
Nyumbani Kwake Bombo Tanga 2008


Mwandishi na Abdulwahid Sykes Nyumbani kwa Japhet Kirilo Usa River 1989
Wakati ule Mwandishi Alikuwa Akitafiti Historia ya Uhuru wa Tanganyika Bahati


1 comment:

omar said...

A Alaykum,
Tacloban ni kisiwa kimoja kati ya vingi vilioko katika nchi ya Philippines.
kwa bakhti mbaya ndicho kilichoathirika zaidi na Typhoon Yolanda .
maelfu ya wakaazi wa kisiwa hiki wamepoteza maisha yao na wengi kukosa makaazi ya kudumu .
Nimebakhtika kuwa nipo katika team ya wanaoshughulikia misaada ya namna mbali mbali kusaidia walioathirika na kimbunga hicho.
nikiwa narudi kazini hii ni wiki yangu ya pili kuweko hapa ,ambako wiki za kabla nilikuwa visiwa vyengine nakutana na waislamu ambao wanaujenga msikiti wao ambao umebomoka wote kwa anjia ya harambe .
nilikuwa na mwenzangu mwenye asli ya kipalestine ambae hisia zake zilikuwa na juu zaidi tulipokutana na haya mungu amjaze khair na imani zaidi kwa alioyafanya .
Mola awape imani na uwezo ndugu zetu hawa kuweza kuyakabil yaliomazito kwao hasa kwa vile nchi hii imezungukwa na wenye imani ya kimishini kwa nguvu sana .
wabillahi Taufik .