''The Torch on Kilimanjaro'' Kitabu Kilichofitiniwa Kisiingizwe Katika Mtaala wa Shule za Msingi za Tanzania![]() Aliyesimama juu ya boneti ya Land Rover akihutubia wananchi ni Mwalimu Nyerere na picha ya pembeni ni Nyerere na Kenyatta. ![]() Mwandishi akitoa maelezo kuhusu kitabu The Torch on Kilimanjaro ![]() |
| Mohamed Seif Khatib katika Uzinduzi wa Kitabu, ''The Torch on Kilimanjaro'' Kilimanjaro Kempinski Hotel kulia kwake ni Sheikh Abdillah Nassir |
Mwalimu akikiangalia kitabu
![]() ![]() ![]() ![]() Kitabu hiki kilikuwa katika mradi wa kuchapa vitabu kwa ajili ya shule za msingi madhumuni yakiwa ni kumsomesha mwanafunzi lugha ya Kiingereza na wakati huo huo ajifunze na historia ya nchi yake ili kujenga uzalendo. Waandishi kutoka Afrika ya Mashariki waliandika vitabu kiasi ya 15 isipokuwa Tanzania. OUP walimfuata mwandishi na kumuomba aandike kitabu kimoja ili angalu Tanzania na wao wawemo katika orodha ya nchi zilizoshiriki katika mradi ule wa kusomesha lugha ya Kiingereza Afrika ya Mashariki. Mwandishi akapeleka mswada Nairobi. Baada ya muda alikwenda Nairobi kuonana na mhariri ili kurekebisha mswada. Mhariri akasafiri hadi Dar es Salaam baada ya kupata marekebisho na kazi ikakamilika. Kitabu kikachapwa. OUP wakafanya dhifa kubwa sana ya kukizindua kitabu Kilimanjaro Kempinski Hotel ambako wakuu wa Wizara ya Elimu walikaribishwa pamoja na vyombo vya habari. Mgeni wa heshima alikuwa Mohamed Seif Khatib. Waalikwa wote walipewa nakala moja ya kitabu na mwandishi alikieleza kitabu mbele ya hadhira ile. Kwa upande wao OUP walikisifia kitabu kile kuwa kitachangia katika watoto wa shule za msingi kujifunza Kiingereza na historia ya nchi yao hususan historia ya Mwalimu Nyerere alipoanza kudai uhuru wa Tanganyika mwaka 1954 hadi uhuru ulipopatikana mwaka 1961. Aliposhuka tu kutoka kwenye jukwaa watu wa televisheni na magazeti wakamzunguka kumhoji kuhusu kitabu kile. Tanzania kitu chochote kinachomuhusu Nyerere kinauzika. Mwandishi na mchapaji OUP walitegemea makubwa kutoka kitabu kile. Haikuwa hivyo. Kitabu hiki kimepigwa chenga kuanzia mwaka 2007 licha ya juhudi nyingi za OUP kuwaandikia Wizara ya Elimu kuwaomba wakiingize katika mtaala wa kusomesha lugha ya Kiingereza. OUP walimweleza mwandishi kuwa wao hawajui kwa nini kitabu hiki chenye historia ya Mwalimu Nyerere hakitakiwi wakati kule Kenya kitabu cha Jomo Kenyatta ''The Kapenguria Six'' kilicho katika mradi huu kipo katika mtaala wa shule za msingi na kinasomeshwa.
The Kapenguria Six
Muswada mpya 'The School Trip'' ambao mwandishi aliwapa OUP na wakaupokea kwa ajili ya uchapaji baada ya kuona uzuri wa kitabu kile cha kwanza, OUP wameghairi kukichapa kitabu na maelezo ni kuwa mwandishi hauziki nchini kwake lau kama ana kipaji cha uandishi wa hadithi za watoto. Hata hivyo OUP walimshirikisha mwandishi katika mradi mwingine kwa ajili ya vitabu Afrika ''The Mermaid of Msambweni and Other Stories'' (2007) kitabu cha mkusanyiko wa waandishi kutoka nchi tofauti za Afrika Tanzania ikiwakilishwa na mwandishi huyu. OUP wala hawakushughulika kukitangaza kitabu hiki hapa Tanzania. Huu mfumo inasemekana una watu wake unaowapenda na kuwatumikia. Je, Wizara ya Elimu ni moja ya taasisi zinazoongozwa na ''Mfumokristo?'' |







No comments:
Post a Comment