Monday, 28 April 2014

CANON R M GIBBONS MZUNGU ALIYEWAWAKILISHA WAAFRIKA KATIKA BARAZA LA KUTUNGA SHERIA (LEGISLATIVE ASSEMBLY)

Msomaji nilikuwa nimemsindikiza mtu katika ofisi wa mtu mkubwa sana katika historia ya Tanzania. Huyu bwana sasa hivi ni mstaafu baada ya kushika nafasi ambazo hakuna Mtanzania ambae kwa kweli anaweza kuzifikia kwa hivi karibuni. Mwenzangu akaingia ndani ya ofisi ya huyu bwana kwa mazungumzo na mimi nikabaki mapokezi ambako niliona kitabu kuhusu Ukoo wa Karimjee (bahati mbaya sikukumbuka kuchukua jina la hiki kitabu) lakini kitabu hiki kinaeleza historia yao yote toka walipotoka India kuja Tanganyika. Picha hiyo hapo chini  ni kutoka kitabu hicho. Picha hii imenivutia kwa kumkuta Padri Gibbons ndani ya mjumuiko huo.

Nakusihi ndugu msomaji teremka hadi chini umsome Father Gibbons kama alivyoelezwa na Kleist Sykes kwa maelezo aliyomueleza mwanae Abdulwahid Kleist Sykes na Abdulwahid akamueleza binti yake Daisy Aisha Sykes na Daisy akaandika maisha ya babu yake katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe, ''Modern Tanzanians.'' Nimekuwekea ukurasa kutoka kitabu hicho ili usome nini Daisy ameandika kutoka kumbukumbu za babu yake.




Ukurasa Kutoka Kitabu,, ''Modern Tanzanians,'' Kilichohaririwa
na John Iliffe
Maneno Katika Ukurasa Yameandikwa na Daisy Sykes Buruku:
The Townsman: Kleist Sykes 

No comments: