By
Kubwajinga
Hii article imejaa uongo na uchochezi mwingi. Mwandishi ametumia porojo za gengeni na kuzifanya kuwa ni facts. Hili la EAMWS ni moja ya uongo na uchochezi uliozagaa mitaani. EAMWS ilikufa kutoana na migogoro ya ndani hasa ule wa Bukoba kulikokuwa na mgongano kati ya wahindi/waarabu (mabepari) vs waislamu wazawa waliokuwa wana-support ujamaa (TANU & ASP). TANU hawakuanzisha mgogoro wa EAMWS ingawa viongozi wake wa kiislamu walishiriki kwenye usuluhishi. Tuachane na fitina/uchochezi kwani hata maandiko nayo yanakemea fitna.
Kubwajinga,
Hayo ulosema ya migogoro ya ndani katika EAMWS ndiyo ''official
version,'' iliyotengenezwa na Usalama wa Taifa na ndiyo iliyodumu
kwa miaka yote.
Marehemu Rashid Kayugwa aliyekuwa Usalama wa Taifa ndiye
aliyepewa jukumu la kuongoza propaganda hizi.
Mwisho wa maisha yake alieleza yote na Kayugwa alijuta sana
alitubia na kuomba msamaha kwa Allah amsamehe.
Lakini nitakuongezea jingine labda hulijui katika sakata ile ya EAMWS.
Uongo ulitengenezwa kuwa Sheikh Hassan bin Amir alikuwa anataka
kupindua serikali ya
Nyerere.
Haya yalidumu kwa kipindi kirefu hadi pale nilipofanya utafiti na baadae
kuandika ''paper,''
''Islam and Politics in Tanzania,'' (Al Haq Interna
tional (Karachi) Vol. 1 No. 3 August- December 1993).
Lakini kabla ya kuchapwa kwa hii ''paper,'' Pakistan mwaka 1993, niliitoa
kwenye mkutano wa East Africa Study Circle, Nairobi mwaka 1989.
Kwa mara ya kwanza ikawa kisa cha mgogoro wa EAMWS kinaelezwa
na upande wa pili na mkono wa Nyerere na Kanisa Katoliki ukawa kwa
mara ya kwanza umewekwa kweupe.
Huu ndiyo ukweli ambao Waislam leo wanaujua.
Vitabu vilivyofuatia vya P van Bergen na John Sivalon kuonyesha
fitna za Kanisa dhidi ya Uislam Tanzania ikawa kama vimekuja kwa nia
ya kunisadikisha yale ambayo nilikuwa nimeandika siku nyingi.
Hayo si uchochezi wala si fitna ni ukweli mtupu wa yale yaliyotukumba
Waislam na yanaendelea kututaabisha hadi leo.
Kubwajinga,
Umeniita mie muongo.
Nakuthibitishia kuwa yote niliyosema ni kweli na kama una uwezo
fanya utafiti wako yote nilliyosema yatakudhihirikia.
Zentrum Moderner Orient (ZMO) ni taasisi kubwa ya utafiti wa
historia duniani iko Berlin.
Walinialika hapo kwa mwezi mmoja na tulielezana mengi katika
maandishi yangu na utafiti nilokwishafanya.
Kama wewe na wao walikuwa na shaka na baadhi ya mambo.
Hadi hivi sasa nimepokea watafiti watatu kutoka Ujerumani na USA
na wote hao wanatafiti kile nilichoandika wakiakisi yale nilohadhiri
Ujerumani.
In Sha Allah tusubiri matokeo ya tafiti hizo.
|
Ofisini Zentrum Moderner Orient (ZMO), BERLIN, GERMANY |
No comments:
Post a Comment