Zanzibar |
Zanzibar ni nchi ya Kiislam.
Tanzania Bara Waislam ni wengi lakini si watawala wa nchi.
Dola Tanzania iko mikononi mwa Kanisa.
Na Waislam hawapendezi sana kila kukicha ni taarifa za kutisha
zaWaislam kupigwa na vyombo vya dola na viongozi wao waliokataa kuwa
vibaraka wa serikali kusimamishwa mahakamani kwa kesi hii au ile.
Hapa ndipo swali linapokuja.
Hii dola ya Bara inawapendea nini Waislam wa Zanzibar na
inawachukia kwa lipi Waislam wa Bara?
Swali jingine.
Tujaalie kuna mapenzi ya kweli baina ya Dola ya Bara na Zanzibar...
Kipi kilichoudhi Bara wakati Zanzibar ilipojiunga na Organisation
of Islamic Conference (OIC) mwaka 1993 kiasi cha Mwalimu Nyerere
kulazimisha lazima Zanzibar ijitoe OIC?
Tafadhali ingia hapa usome sakata la Zanzibar na OIC:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/zanzibar-membership-to-organisation-of.html
Ukiweza kujibu maswali haya utaweza kujua kwa nini kuna vurugu
Bunge Maalum la Katiba na kwa nini bunge la Tanzania linalohodhiwa na
Kanisa limejiimarisha zaidi kwa kujiongezea wafuasi zaidi katika bunge
hilo?
Bunge la Katiba lina uiano katika nyanja zote isipokuwa ya dini.
Katika dini Waislam lazima kama ada wawe wachache na Wakristo wawe
wengi.
Haya yote ni kutaka na kutafuta nini?
Hebu ingia hapa uone upogo huo wa dini:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/uteuzi-wa-baraza-la-katiba.html
Sasa kwa kuhitimisha ili picha ikae sawa ukutani ingia hapa chini
ujikumbushe wapi Zanzibar imetoka katika kutafuta uhuru wake katika
historia ya miaka ya hivi karibuni:

NB: Makala zote hizo hapo juu zinapatikana hapa hapa katika
website hii.
No comments:
Post a Comment