Kabla msomaji hujasoma kisa hicho hapo chini hebu jiulize.
Lakini kabla hujasoma kisa hiki au baada ya kusoma kisa hiki itakuwa vizuri ukaijua historia ya Maaskofu na Kanisa wakati Waislam wanapigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950 ili kuaondoa dhulma na kuleta haki na usawa kwa wananachi wote.
Sasa soma kisa hiki kama kinavyotujia baada ya nusu karne ya uhuru::
Inaweza kutokea siku sheikh akapiga simu polisi kudai kuwa Muhammad (SAW) anatukanwa kanisani na hapo hapo polisi wavamie kanisa na kuanza kuwapiga Wakristo kisha kuwafungulia mashtaka mahakamani ya uchochezi na mahakama ikazuia dhamana yao?
Achilia mbali kuwa katika kipigo hicho wapo Wakristo wanakojoa damu na wengine hawawezi hata kutembea?
Lakini kubwa...
Magazeti yote yasiandike kuhusu tukio hilo?
Waislamu tufanye nini katika hali hii iliyopo nchini kwetu wakati vyombo vyote vya dola vinapojigeuza kuwa watumishi watiifu wa Kanisa.
Lakini masheikh wana dhima mbele ya Allah kuwapa fatwa Waislam nini kinachotakiwa kifanywe dhulma inapotamalaki dhidi ya umma wa Kiislam.
Hivi sasa tuna kesi ya Sheikh Ponda, Sheikh Chambuso na kadhia nzima ya mauaji ya Waislam Kilindi na inaelekea hakuna dalili za kupungua kwa dhulma hii.
Nini Waislam tufanye?
Waislamu tufanye nini katika hali hii iliyopo nchini kwetu wakati vyombo vyote vya dola vinapojigeuza kuwa watumishi watiifu wa Kanisa.
Lakini masheikh wana dhima mbele ya Allah kuwapa fatwa Waislam nini kinachotakiwa kifanywe dhulma inapotamalaki dhidi ya umma wa Kiislam.
Hivi sasa tuna kesi ya Sheikh Ponda, Sheikh Chambuso na kadhia nzima ya mauaji ya Waislam Kilindi na inaelekea hakuna dalili za kupungua kwa dhulma hii.
Nini Waislam tufanye?
Je Waislam warejee katika Azimio la Tungi?
Jibu utakuwanalo mwenyewe ndugu Muislam.
Lakini kabla hujasoma kisa hiki au baada ya kusoma kisa hiki itakuwa vizuri ukaijua historia ya Maaskofu na Kanisa wakati Waislam wanapigania uhuru wa Tanganyika katika miaka ya 1950 ili kuaondoa dhulma na kuleta haki na usawa kwa wananachi wote.
Nimekuwekea historia nzima ya Kanisa na Ukoloni angalia hapa:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/tanu-ilivyovunja-ngome-ya-kanisa-kanisa.html
Sasa soma kisa hiki kama kinavyotujia baada ya nusu karne ya uhuru::
Askofu aleta balaa kwa Waislamu wa Masasi
![]() |
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Zelotte Steven |
Kwa mtindo ule ule wa Mwembechai, Polisi wamevamia Waislamu msikitini, kutoa kipigo k i k a l i n a ku watupa rumande baada ya kuwajeruhi vibaya.Walifanya hivyo baada ya kupelekewa taarifa na Askofu mmoja nao kuchukua hatua bila kuchunguza wala kuhoji.
Askofu huyo alidai kuwa Yesu alikuwa akitukanwa katika msikiti mmoja ambapo kulikuwa kukifanyika muhadhara. Hata hivyo, hapakuwa na muhadhara, bali Waislamu waliokuwa wamekusanyika kufanya fikra juu ya kuweka umeme katika msikiti wao.
Wakati shughuli zikiendelea wa kawa wameweka CD ya mdahalo uliokuwa umefanyika ka ti ka ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. Hata hivyo, Polisi hawakutka kuuliza wala kuchunguza madai ya Askofu, bali kwa mtindo ule ule uliotumika Mwembechai wakavamia Waislamu kuwapiga na kuwatia mbaroni.
Mpaka sasa Waislamu saba wapo rumande baada ya dhamana zao kufungwa, huku mmoja wao akiwa amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Masasi Mkomaindo, kutokana na kipigo cha Polisi hao. A w a l i k a b l a y a kukamatwa Jumamosi ya wiki iliyopita, ilidaiwa kuwa Polisi hao walivamiana kuingia ndani ya Msikiti wa Kijiji cha Mwembe na kuwapiga Waislamu waliokuwepo msikitini hapo na kuwajeruhi na kisha kuwakamata na kuwapeleka katika kituo cha Polisi Wilayani Masasi. Imeelezwa kwamba katika uvamizi huo ndani ya Msikiti, Polisi pia wamedaiwa kuchukua Amplifier, pesa tasilim kiasi cha shilingi 522,000 pamoja na kuharibu miundo mbinu ya umeme na kuvunja kisanduku cha pesa za sadaka na kutoweka nazo.
Waislamu hao walifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi Jumatatu wiki hii na kusomewa mashitaka ya uchochez i, huku dhamana yao ikizuiwa na kurudishwa rumande hadi Aprili, 14, 2014, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Mwandishi wa habari hizi alipowasiliana na Kamanda wa Polisi Mkoani Mtwara, Kamanda Zelothe Steven, ili kutolea ufafanuzi madai hayo, alisema kwamba kesi ipo Mahakamani na kumtaka mwandishi aenda akaulize huko. “ Nadhani tayari nimeshakujibu kwamba kesi hiyo tayari ipo Mahakamani, mimi sina cha kusema, asante nimeshakujibu.” Alijibu Kamanda Steven na kukata simu.
Akielezea tukio hilo kutoka Masasi, Katibu wa Habari wa Jukwaa la Vijana Masasi, Ustadhi Hussein M c h o m o l o , a l i s e m a Waislamu wamesikitishwa na hatua ya Jeshi la Polisi, k u f u a t a m a e l e k e z o kiongozi wa Kikristo bila kuyafanyia uchunguzi. Alisema katika tukio hilo lililotokea katika kijiji cha Mwenge, Waislamu walikuwa katika kikao Msikiti wa Mwenge kujadili kufanyia ukarabati mfumo wa umeme (wiring) katika Msikiti huo.
Kabla ya kutokea tukio hilo, Ust. Mchomolo, alisema wakati wanasubiriana ili waanze kikao hicho majira ya kuelekea Alasir, waliweka mkanda (CD) ya mdahalo baina ya Waislamu na Wakristo uliofanyika Jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa Diamond, wakawa wanasikiliza.“Walikuwa wamefika Waislamu nane, sasa wakati wanawasubiri wenzao ilibidi waweke kanda ya mdahalo wa muhadhara baina ya Waislamu na Wakristo, wakawa wanasikiliza.” Alisema Ust. Mchomolo.
Alisema wakati Waislamu wakiendelea kusikiliza mdahalo huo, Mchungaji mmoja aliwapigia simu Polisi na kuwaeleza kwamba ku na Waislamu wanafanya Mhadhara na wanamtukana Yesu. Ust. Mchomolo, alisema kufuatia taarifa hizo, Polisi walifika Msikitini hapo na bila kuuliza waliingia ndani ya Msikiti na viatu vyao kisha wakaanza kutembeza kipigo kwa Waislamu hao wanane waliokuwa ndani ya msikiti. “Waliingia mle ndani waliwakuta Waislamu wanane tu, kati yao mmoja alikuwa fundi umeme na alikuwa ameshaanza kufanya matengenezo ya mfumo wa umeme ndani ya Msikiti huo”. Alibainisha Ust. Mchomolo.
Alisem a baada ya Polisi kuingia, mmoja wa Waislamu hao alihoji kwamba kun a tatizo gani, na kuwaeleza kama kuna tatizo ingekuwa vizuri wangewaita nje ili wawaeleze kuliko kuingia na viatu kama kwamba wamegoma kutii amri. “Badala ya kutoa majibu maafande hao walianza kutoa kipigo kwa Muislamu huyo kisha kuwajumuisha katika kipigo na wale wengine waliokuwemo humo ndani. Baada ya kuwajeruhi waliwatoa na kuwaingiza katika gari lao na kuwapeleka kituo cha Polisi”. Alisema Ust. Mchomolo.
Alisem a baada ya Polisi kuingia, mmoja wa Waislamu hao alihoji kwamba kun a tatizo gani, na kuwaeleza kama kuna tatizo ingekuwa vizuri wangewaita nje ili wawaeleze kuliko kuingia na viatu kama kwamba wamegoma kutii amri. “Badala ya kutoa majibu maafande hao walianza kutoa kipigo kwa Muislamu huyo kisha kuwajumuisha katika kipigo na wale wengine waliokuwemo humo ndani. Baada ya kuwajeruhi waliwatoa na kuwaingiza katika gari lao na kuwapeleka kituo cha Polisi”. Alisema Ust. Mchomolo.
Ust. Mchomolo, alisema mbali ya kutoa kipigo kwa Waislamu hao na kuwajeruhi, lakini pia walifanya uharibifu ndani ya Msikiti huo na kutoweka na baadhi ya vitu.Alifafanua uharibifu waliofanya Polisi hao ndani ya Msikiti huo kuwa ni kufumua miundombinu yote ya waya ambayo fundi alikuwa tayari ameshaanza kufanyia mateng e n e z o , k i s h a kukata nyaya zilizokuwa zinatoka katika Amplifier kwenda katika spika. Hawakuishia hapo, Ust. Mchomolo, alidai kwamba Polisi hao walidiriki hata kuvunja kisanduku cha pesa za sadaka za Waislamu na kuchukua pesa zote zilizokuwemo humo ambapo haijajulikani ni kiasi gani. Zaidi Ust. Mchomolo, alivitaja baadhi ya vitu vilivyotoweka na Polisi hao kuwa ni Amplifier, betrii ya gari (Yuasa) na pesa kiasi cha shilingi 522,000/ - ambazo Waislamu walikuwa wamepanga kumlipa fundi wao, zikijumuisha na gharama za nyaya za umeme.
I l i e l e z w a k u w a Muislamu mmoja ambaye ni fundi umeme, Polisi w a l i m k a b i d h i k w a ndugu zake baada ya kupoteza fahamu kufuatia kipigo walichompiga, wakiwataka wampeleke hospitalini.“Fundi alipigwa zaidi hadi kupoteza fahamu, Polisi walichofanya ni kuwaruhusu ndugu zake kumchukua ili wampeleke hospitalini, kwani hali yake ilikuwa ni mbaya sana.” Alisema Ust. Mchomolo. Ust. Mchomolo, alisema kuwa siku ya Jumapili (iliyopita) Waislamu walifika kituo cha Polisi, lakini wa lishindwa kutoa msaada wowote kufuatia Polisi kituoni hapo kuwataka kwanza wawasiliane na RCO, aliyetajwa kwa jina la Afande Meela. Hat a hivyo, Ust. Mchomolo , a m b a y e anafuatilia kwa karibu suala hilo, alisema tangu kukamatwa kwa Waislamu hao (Jumamosi) wamekuwa wakimpigia RCO kufuatia maelekezo ya Polisi kituoni hapo bila mafanikio yoyote. Alisema wamekuwa wakilazimika kufika kituoni hapo tangu kukamat wa kwa Waislamu hao kwa lengo la kuwawekea dhamana na kujua utaratibu wa kuwapatia matibabu kwa kuwa watuhumiwa wamedaiwa kuwa hawajiwezi hata kutembea kutokana na kipigo cha Polisi waliowakamata.
Kibaya zaidi kati ya hao waliopo rumande mmoja anadaiwa kukojoa damu. Ust. Mchomolo, alisema hali hiyo wameibaini siku ya Jumatatu baada ya kufika kituoni hapo kufatilia taratibu za dhamana na kuwajulia hali ndipo walipoelezwa kuwa kuna jamaa yao mmaja anakojoa damu. “Tulipofika mmoja wa askari alituambia kuna Muislamu mmoja hivi sasa anakojoa damu na akatuambia kutokana na hali yake hiyo, anunuliwe dawa aanze kumeza na ni kweli baada ya kufanikiwa kuwaona walituthibitishia kuwa mmoja wao yupo katika hali hiyo. “Tayari tumefanya utaratibu wa kumpatia dawa, lakini mpaka sasa tupo hapa Polisi tunasubiri wapelekwe Mahakamani, wanadaiwa wamefanya uchochezi.” Alisema Ust. Mchomolo. Waislamu hao walifikishwa na kusomewa shitaka hilo Jumatatu wiki hii katika Mahakama ya Wilaya ya Masasi. Aliwataja Waislamu h a o k u wa n i J a f a r i Said, aliyelazwa katika Hospitali ya Mkomaindo, w e n g i n e ni Ahmad Daud, Salum Swalehe, Bakari Ismail, Hija Aphat, Mohammed Hamimu, Abbasi Mabweha, pamoja na Bashiru Hamisi. Watano kati ya hao, walionekana kushindwa kutembea w a k a t i wakiletwa na kutoka Mahakamani.
***
Allah Subhana Wataala Forbid! They will do this once too often and then...the stalk which broke the camel's back...Bang!
Difficult to reverse...the country will burn before our very eyes...Allah tuepushe na balaa hilo. Amin.
Allah Subhana Wataala Forbid! They will do this once too often and then...the stalk which broke the camel's back...Bang!
Difficult to reverse...the country will burn before our very eyes...Allah tuepushe na balaa hilo. Amin.
Mufti wa BAKWATA Sheikh Shaaban Simba |
1 comment:
Innaa lillahi wa innaa ilaihi rajiuun
Lini nusra ya Allah itakuja kwa waislam tumekosea wapinhadi tunapata adhabu hii ili tujirekebishe
Wallahu mustaan
Post a Comment