Wednesday, 30 April 2014

''KUNO KUNO KUNO,'' MREJEE JAMVINI KWA SHEIKH JONGO...

Ndugu Msomaji,

''Kuno, kuno, kuno,'' ni mwito wa watu kuitana mara nyingi kwa jambo zuri la kufurahisha. Hii ni lugha ya Kibandari. Ukisikia kuli anapiga kelele, ''Kuno kuno kuno,'' basi jua zimefika taarifa kuwa labda siku ile ofisi ya Bwana Fedha kunatoka ''advanzi,'' au kunatoka ''bogi,'' au kunatoka mshahara. Ikiwa hivyo hapo wanapangiana zamu kuacha ''mzigo,'' kupandisha kwa Bwana Fedha kwenda kupokea. Hii  ''KUNO, KUNO,'' ni lugha ya makuli. Makuli hawa sasa hawapo. Kazi ya ukuli siku hizi si ya watu wa pwani tena kama zamani miaka ya 1940 na 1950 hadi 1970 ikawa kazi yenyewe imachangwanywa na mila na misemo ya pwani ya Wamatumbi, Wandengereko, Wazaramo, Wangindo, Warufiji, Wamakonde wa Lindi nk. Bandari za sasa hakuna, ''Kuno kuno,'' asilani.

Nawapigia ''kuno kuno,'' ndugu zangu ili kama ulishapita kwa Sheikh Jongo In Sha Allah urudi tena jamvini usome upya. 

Nimeongeza maanjumati...

No comments: