Wednesday, 30 April 2014
WASEMAVYO KUHUSU SHEIKH ALI MUHSIN BARWANI
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Introduction Below is a cut and paste from Wikipedia. Please compare and contrast between Ton Ton Macoute of Haiti and Zombies of Zanzi...
1. Kupiga vita Uislamu kwa kuvunja mashikamano baina ya Kiswahili na Kiarabu na kubadilisha maandishi yetu asilia kuyafanya kwa harufi za Kizungu. Kwa kufanya hili imewatenga Waswahili na misingi ya dini yao. Hayo pia yamefanywa kwa Maturuki, Maindonesia na wengineo.
2. Kuvamiwa Zanzibar mwaka 1964 na kuondosha serikali ya kidimokrasia na kuimeza Zanzibar kwa jina la muungano wa Tanzania. Hili limefanywa tokea hapo mwanzo wa kuunda huo muungano kwa makusudi aliyo yasema majuzi Mheshimiwa William Lukuvi Waziri ya serikali ya Tanzania kwamba “hatuiachii Zanzibar yenye Waislamu 95% kuwa nchi kwa sababu wataleta serikali ya Kiislamu”.
3. Serekali za baada ya kutoka wakoloni ziliwashinda wakoloni kuzuia uhuru wa kuabudu na kuingilia wafuasi wa dini kufuata sharia zao. Haya yamefanzwa kwa jina la kuhifadhi ati usalama wa dola na wa nchi. Hapo ikavunjwa kila haki za mwananchi na ikawa usalama wa mwananchi umetanguliwa na usalama wa watawala. Mabaraza ya wananchi ya kidini yakavunjwa na serekali ikawaundia wananchi vyama vya dini vya serikali. Dini ikapotezwa.
Huyu Sheikh Ali Muhsin tokea ujana wake alipinga ugozi na chuki za kikabila na alifanya kila juhudi kuunganisha watu wake Wazanzibari wawe wamoja. Juhudi zake amezipiga vita mtawala mkoloni na vibaraka vyake na yakatokea yaliyo tokea. Hapana alie weza kuwaunganisha Wazanzibari ila Rais Amani Karume na Maalim Seif Sharif walipo unda serikali ya Muwafaka. Watawala wa leo wanafuata mbinu za wakoloni kuwagawanisha watu waweze kuendela kuwatawala kwa miaka 50 mengine. Ulimwengu wa leo sio wa 1964. Watu waTanzania nzima wameamka si Muislamu wala si Mkristo, wote wanajua nani mfitinaji na hawakubali kuatawliwa kwa mabavu.