Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Jakaya Mrisho Kikwete |
Fuatilia hapa In Sha Allah tutajitahidi kuweka mambo yanayosibu nchi
yetu toka tupate uhuru mwaka 1961...
Ninaandika kitabu kuhusu siasa za Tanzania na jinsi dini inavyotawala
hisia za watawala walio madarakani. Katika sura moja ninaeleza namna Jakaya
Mrisho Kikwete alivyoweza kufanya kampeni kwa miaka kumi na hatimae akaweza
kuchaguliwa kuwa rais...lakini haikuwa kazi nyepesi kwa mara ya kwanza 1995
alipojaribu juhudi zake zilipata upinzani wa chinichini..
Nakuwekea hapa msomaji yale niliyoandika katika mswada wangu.
Nia ni kuangalia ni kweli Mwalimu Nyerere aliacha taifa lisilo na udini,
lenye mshikamano wa kweli na umoja?:
''But before the conference Kikwete went
on record to complain that the secretary of the party Dr. Lawrence
Mtazama Gama, a Catholic, and hailing from the south like Mkapa was
undermining his campaign on religious grounds. Nyerere who
had earlier and eloquently promised him that he would take care of religious
sentiments for Kikwete, was suddenly dead silent. For a time
it seemed as if the party was to engulf into a religious crisis involving its
own top leadership. Religion was a sensitive issue and CCM had always
maintained that the party did not discriminate its members on religious
grounds. The conflict between Kikwete and Gama was
an embarrassment to the party. In a strange turn of reconciliation
effort CCM issued a statement that Gama had apologised
to Kikwete. It is a pity that Kikwete did not
reveal what religious issue became the source of conflict that the party
had Gama to apologise. The thought of Gama apologising
to Kikwete was a humiliation to Gama not only
because of his seniority but because of other factors...''
Hii ndiyo hali ilikuwapo wakati Kikwete na Mkapa wanaelekea
Dodoma kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM itakaochagua mgombea wa CCM.
Hapa Khalfan Mrisho Kikwete, Muislam alikuwa anakwenda kupambana
na Benjamin William Mkapa Mkatoliki mfuasi wa kanisa lenye
nguvu kupita kiasi Tanzania...
Fatilia ukarasa huu kwa
mengine In Sha Allah...
''Mkapa was forced to pick his campaign
committee from people outside the inner circle of the party. Two
newspapers publishers were in his committee Damian Ruhinda and Jenerali
Ulimwengu. The special NEC Conference convened to elect one CCM member
to stand for presidential candidate elected Jakaya Mrisho Kikwete in
the first round with Mkapa coming close second and Msuya was
last. But since he had not commanded an absolute majority voting had to be
repeated. There was tension in the conference hall as CCM delegates voted to
choose between Kikwete and Mkapa. Christians were
heard to whisper to each other that they should not again allow a Muslim to
govern the country, never again they whispered to each other.
And when Mkapa won hymns were
sung.''
Huu ndiyo ukweli wa siasa za
Tanzania... dini haichezi mbali.
Lakini ili ndugu mfuatiliaji
upate picha halisi ya nini kilikuwa kinafanyika nyuma ya pazia itabidi nimlete
mgombea mwingine aliyekuwa mwanachama wa CCM...
Prof. Kighoma
Abdallah Ali Malima...
''The difference between Prof.
Malima and Kikwete was that, while Kikwete really
believed that he was a serious candidate for Nyerere, Prof.
Malima knew Kikwete was thrown into the race by the
Christian lobby to block him. The rule of the game was to play a Muslim against
a Muslim. But Kikwete was too naive to understand that. His
background had not prepared him to understand the intricacies of politics in Tanzania as it relates to dealing with Islam and Muslims. If he had taken
some time to think long and hard he would have realised that if experienced
people like Malecela, Msuya and Kolimba were
not seen as fit to rule the country despite of their long service to the
country which span more than three decades how possible could he supersede them
and be a better candidate than those old guards?''
Marehemu Malima alikuwa
akihadithia mkasa huu wa mkutano wa Dodoma wa kuwafanyia usaili wagombea hakika
akinitoa machozi kwa kucheka. Si kama yale aliyokuwa anahadithia yanachekesha
hivyo bali kwa vile mtu unavyoweza kushangaa inakuwaje watu wazima wakachezewa
vile na Nyerere na wao wasijijue kama wanachezewa. Malima alikuwa
akinichekesha pale alipokuwa anasema yeye alipoingia kuhojiwa kamkuta Nyerere
yuko ubavuni kwa Mwinyi utadhani wamekaa kiti kimoja. Ilikuwa
lazima Kikwete aletwe kugombea vinginevyo wagombea wote
wangekuwa Wakristo ukimtoa marehemu Prof. Malima. Hali ingelikuwa
vile ingekuwa lazima Prof. Malima wamchague ama sivyo Waislam
wangelikuwa hawamo katika mbio za kwenda Ikulu. Sasa Nyerere hakuweza
kucheza na shilingi chooni. Prof. Malima na Mkapa washindane...hakuweza
kutabiri matokeo kwani Prof. Malima akipendeza sana kwa umma
wa Waislam...sababu za kupendeza huko ni kuwa Prof. Malima allijtolea
kuiasa serikali kuwa kuna ubaguzi wa kidini dhidi ya Waislam nchini petu.
Turudi mwanzo
tulikoanzia...
Rais Kikwete anasema, ''Mzee
Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye
amani na mshikamano...'' (Mwananchi Ijumaa, Aprili 18, 2014).
Hiyo hapo juu ni picha ya ya
nchi yenye amani na mshikamano?
Jibu utakuwanalo wewe msomaji.
Waislam bila kificho
wametembea nchi nzima kuwaeleza wananchi kuwa Tanzania inaendeshwa na Mfumo
Kristo na Waislam wanabaguliwa toka uhuru upatikane. Kwa kauli hiyo hapo
juu ya Rais Kikwete ni kuwa kapuuza kilio cha Waislam.Kwake
yeye hakuna dhulma na Waislam ni waongo kwani wao na Wakristo wote wana fursa
sawa. Kanisa linatumia vyombo vya ulinzi kama jeshi lake
binafsi. Waislam wanapigwa ndani ya misikiti na kufunguliwa kesi za
kubambika. Kovu la Mwembechai la mwaka 1998 bado halijapona. Waislam
wamesingiziwa kuwa ni magaidi na askari wemeingia katika vijiji vyao kuwapiga
na kuwaua na misikiti yao kuchomwa moto. Haya yametokea Kilindi na jambo
la kusikitisha vyombo vyote vya habari vimekataa kuandika habari
hizi. Binafsi nimezungumza na vyombo vya habari vya kimataifa na kuwapa
picha za video kuonyesha unyama waliofanyiwa Waislam. Wamekiri kuwa hakika
dhulma imetendeka lakini hakuna hata chombo kimoja kilichokuwa na ujasiri wa
kufanya kitu. Majuma mawili yaliyopita Masasi Waislam wameingiliwa msikitini
baada ya sala ya Ijumaa na kupigwa kwa kusingiziwa ati wamemtukana Yesu. Baada
ya kipigo hicho wamfunguliwa kesi ya uchochezi. Swali la kujiuliza ni hili kwa nini Waislam hawapelekwi mahakamani ila sisi ni kupigwa kisha ndiyo tunafikishwa mbele ya vyombo vya sheria?
Ndugu msomaji hii ndiyo amani
aliyotuachia chembelecho Rais Kikwete, Mzee Nyerere? Hili
ndilo taifa moja, lililoungana, lenye umoja, lenye amani na
mshikamano? Rais Kikwete kipi kinamfanya ajifanye kuwa haujui
ukweli?
Ali Hassan Mwinyi na Mama Maria Nyerere wakiangalia Nyerere Akicheza Bao |
No comments:
Post a Comment