Thursday, 17 April 2014

WILLIAM LUKUVI NA HOFU YA UISLAM


#126   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert MemberArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,290
Rep Power : 66105
















Likes Received
3478
















Likes Given
217

Default Re: Lukuvi: Nina Hofu na Uislaam aka "Islamophobia".

Quote By FaizaFoxy View Post
Kabla ya kutoka bungeni baadhi ya wabunge wa UKAWA jana, Professor Lipumba aliweka wazi aliyoyaongea kanisani waziri mmoja wa Serikali ya Muungano. Lipumba alisema kuna waziri kaenda kuhutubia kanisani kuwa "ikiwa Zanzibar itapewa mamlaka kamili basi mjuwe itaanzisha dola ya Kiislam".

Jana nikauliza ni waziri gani huyo? sikupata jibu humu JF.

Lakini kwa kuwa Mungu hamfichi mnafik, huyo waziri kajitokeza mwenyewe bungeni leo hii na kwanza kukiri kuwa katumwa na Waziri Mkuu na kusema kuwa hiyo ni hofu, "phobia" yake na akaendelea kusema "hakuna yeyote wa kunizuia hofu yangu hii".

Akazunguka wee na maneno lakini akashindwa kukisema kile alichokieleza Lipumba.

Kwa uchache, Lukuvi ameudhihirishia umma kuwa ana "Islamophobia" au hofu ya Uislaam.

Kiongozi unaefikia kutangaza Kanisani na Bungeni kuwa hutaki kuwapa mamlaka kamili Zanzibar kwa ajili ya dini yao, kweli hiyo si Serikali ya Mfumo Kristo tunayoilalamikia siku zote humu?

Na leo Lukuvi kahitimisha kwa kuniunga mkono yale ninayoyasema humu kila siku kuwa huu Muungano upo kwa ajili ya Kanisa. Na unaongozwa na Kanisa. Huwa mnajifanya hamnielewi lakini leo yamebainika bayana.

Wanaonisikitisha zaidi ni wale Wazanzibari waliobaki kuipigia makofi hoja hii ya Lukuvi, halafu wanajiita wao Waislaam. Waislaam mnaambiwa hampewi nchi yenu kwa kuwa Lukuvi ana hofu mkipewa mtaifanya dola ya Kiislaam na nyinyi mnashangilia? Yaani Lukuvi anawaambia kinaga ubaga kuwa mtabaki ndani ya mfuko Kristo mkitaka msitake na mkikataa basi ni bora nchi hii ishikwe na jeshi na akafikia mpaka kuwapa mfano wa Islamic Brotherhood ya Egypt.

Kinachonishangaza hii hofu yanini kwa Lukuvi? ikiwa nchi anayoiongelea ni Zanzibar na Wazanzibari 99% ni Waislaam ikiwa wataamuwa nchi yao kuwa ya Kiislaam yeye anapatwa na hofu ya nini?

cc Ritzgombesugu kahtaan
Moderator tafadhali usiiunganishe hii na nyuzi nyingine hii maudhui yake inajitegemea.
FaizaFoxy,
Mara tu lilipodhihiri tatizo la serikali mbili au tatu niliweka mada kadhaa katika
website yangu na katika nyingine mbili nikisema kuwa hapatawezekana kamwe
mtu yeyote kuweza kufanya tafakuri ya maana na kuweza kuchangia katika
mada hiyo bila ya kujua historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar.

Ukishajua historia ya kweli ya mapinduzi ya Zanzibar hapo mtu anaweza kuwa
katika hali ya siyo tu kuchangia bali hata kujua kwa nini kwanza, hii leo historia
ya mapinduzi imetiwa mkono na kubadilishwa.

Pili atajua kwa nini hao mashujaa khasa wa mapinduzi yenyewe hawatajwi; na
tatu kutokakana na kujua hayo mawili yalotajwa ataelewa kwa nini Zanzibar leo
haitakiwi kuwa huru.

Katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi zimetolewa medali kadhaa
kwa wale mashujaa wa mapinduzi.

Ikiwa unaijua historia ya kweli ya mapinduzi utashangazwa kwa kukosekaaa majina
ya wapangaji wa mapinduzi.

Na hakika kuna wengi wameshangaa mbona kinara wa mapinduzi Abdallah Kassim
Hanga hakuenziwa?


Hanga kafutwa katika historia ya Zanzibar.

Ukimsikia Hanga anatajwa basi atatajwa na wale ambao wameumizwa jinsi
alivyouliwa kishenzi mwaka 1967 au 1968 hakuna mwenye uhakika ni lini aliuliwa.

Mbona Oscar Kambona hakuenziwa? Mbona Victor Mkello hakuenziwa?

Mbona Aboud Mmasai hakuenziwa? Mbona Omar Mohamed Mkwawa hakuenziwa?

Vipi kuhusu John Okello? Vipi Mwalimu Nyerere aliyetoa msaada mkubwa kutoka
Tangayika, msaada wa fedha na ''logistics'' hatajwi popote wala hakuenziwa?

Wako wengi waliostahili medali hawakupewa medali.

Mbona halitajwi jeshi la mamluki wa Kimakonde kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura
na Kipumbwi waliokuwa chini ya Victor Mkello na kuvushwa kuja Zanzibar na Mzee Mkwawa,
mamluki ambao ndiyo waliua watu wengi katika mapinduzi yale?

Hebu tuanze na kujiuliza kwa nini mambo yako hivi?

Hapa kinafichwa kitu gani?

Kwa wenye kujua historia ya kweli ya Zanzibar na kwa nini serikali ya Sheikh
Mohammed Shamte ilipinduliwa hawashangai kusikia William Lukuvi kenda

kanisani kusema aliyosema kuwa kuna hofu Zanzibar itaimarisha Uislam ikiwa
itaachiwa kuwa huru.

Kwa sasa nitaishia hapa niwaache wana jamvi wahangaishe akili na fikra zao.
Last edited by Mohamed Said; Today at 17:12.


Kassim Hanga aliyekaa chini mwenye miwani na hii ndiyo ilikuwa mara yake
ya mwisho kuonekana baada ya siku hii alirudishwa Zanzibar na huko aliuawa
Photo
Victor Mkello Akiwa Katika Siku Zake za Mwisho
Hapa Yuko Kwenye Kitanda Chake cha Umauti Mwaka 2003
Mzee Mkwawa Akisoma Kitabu Kilichoandikwa na
Dk. Harith Ghassany ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' Karume alimpa jina
 la utani, ''Tindo,'' kwa mchango wake katika Mapinduzi ya Zanibar



Manamba wa Kimakonde Katika Shamba la Mkonge Tanga
Hawa Ndiyo Waliovushwa Kwenda Kusaidia Mapinduzi Zanzibar

2 comments:

ric said...

unapotosha watu kwani tumemsikia hakumaanisha hivyo.Kazi yako uchonganishi.

Unknown said...

Hakuna kilichopotoshwa hapo,jitahid kufuatilia mambo kwa undani bila kuegemea upande wowote,