Thursday, 1 May 2014

MAUWAJI YA MSIKITI WA MWEMBECHAI 1998

Sajenti Rashid Zahaki Kijana wa Kiislam Aliyefukuzwa Kazi
Jeshi la Polisi kwa Kusikitishwa na Mauaji ya Msikti wa
Mwembechai Mwaka 1998

Kliki hapo chini uangalie video ya Mauwaji ya Msikiti wa Mwembechai:

Sikupata kabla kumjua Rashid Zahaki hadi aliponipigia simu nikiwa Tanga na hapo ndipo tulipofahamiana. Kwa ufupi aliniambia kuwa ana habari muhimu kuhusu kuuliwa kwa Waislam Mwembecha ambazo angependa kunifahamisha. Tukapanga miadi kuwa nikija Dar es Salaam nitampigia simu tuonane na anipe hicho kisa. Mauaji ya Mwembechai yalikuwa mashuhuri na ni moja katika matokea ya kusikitisha na kuhuzinisha katika historia ya Waislam wa Tanzania. Hakika nilimkaribisha Rashid Zahaki nyumbani kwangu na akanielza mkasa mzima wa nini kilikuwa kimepangwa hadi yakatokea mauaji yale. Wakati ule yeye Rashid Zahaki alikuwa katika Jeshi la Polisi. Kanda ile niliyorekodi nilimpa Dk. Hamza Mustafa Njozi na yeye kufuatia umuhimu wa taarifa ile alitumia mazungumzo yangu kwenye moja ya kitabu chake,''Muslims and the State in Tanzania.'' Kabla ya kukutana na mimi kwa muda mrefu alipita katika vyombo vya habari tofauti akijaribu kuwaeleza ukweli wa kile kilichotokea Mwembechai na kusababisha mauaji lakini hakuna hata mhariri mmoja aliyekuwa tayari kumsikiliza na kuchapa taarifa yake. Kipindi kile alinieleza Zahaki kuwa kilikuwa kipindi kigumu sana katika maisha yake licha ya kuwa hana tena njia ya kuendesha maisha yake bali aliona kwa dhahiri yake nguvu ya Mfumokristo katika Tanzania. Ndipo hapo baadhi ya watu wakamuelekeza kukutana na mimi labda ningeweza kusikiliza kisa chake na kukiweka bayana kwa Waislam kukifahamu. Wakati namsikiliza Rashid Zahaki ilinijia picha katika kitabu cha Muhammad Ali ''The Greatest My Own Story,'' ambacho kuna sura inayoeleza kuwa siku moja katika miaka ya 1970 baada ya Ali kushinda kesi ya kufungiwa kupigana, muda mchache kabla hajapanda ulingoni aliletwa kijana wa Kinegro ambae Klu Klux Klan walikuwa wamemhasi, yaani wamemkata sehemu zake za siri na kuzinyofoa kabisa kwa chuki ya rangi. Yule kijana kwa muda mrefu alikuwa anatafuta nafasi ili amuone Ali na kumwelezea kisa chake akiamini Ali alikuwa na uwezo na ujasiri wa kueleza dunia mkasa wake. Zahaki tukiwa nyumbani kwangu sauti iliyokuwa ikinijia ilikuwa ya kinasa sauti changu kikizunguka na sauti ya upole ya Zahaki akieleza chuki iliyokubuhu katika jeshi la polisi dhidi ya Waislam. Hii ilikuwa zaidi ya miaka 10 iliyopita. Muongo mmoja. Hali ikoje hivi sasa?

Nilimfananisha Zahaki na yule kijana wa Kinegro aliyefika mbele ya Ali kumueleza dhulma aliyofanyiwa na Wazungu wabaguzi wa rangi.

Kisa kizima cha Sajenti Rashid Zahaki kimo humu ndani:
http://www.mohammedsaid.com/2014/02/rashid-zahaki-na-mauaji-ya-mwembechai.html

Hali ikoje kutoka mwaka 1998 hadi leo mwaka 2014?
Angalia picha hii ya Waislam wakitoka mahakamani Morogoro ambako Sheikh Ponda amenyimwa tena dhamana:


Waislam Wakitoka Mahakamani Morogoro kwa Maandamano Walipokwenda
Kusikiliza Kesi ya Sheikh Ponda
Mwananchi 1 May 2014

No comments: