Platozoom,
Najua na niko hadhir sana ninalofanya.
Wala isikupitikie kuwa mimi au siye ni watu wa kuletewa hizo unazoita, ''stori.''
Mimi si ''mwandishi,'' kwa maana iliyozoeleka niko mbele sana ya hapo.
Mengine hatuyaandiki kwa kutafuta salama ya nchi yetu.
Ninalofanya hapa ni kuitahadharisha serikali ijue kuwa uko mfumo ndani ya serikali
ambao uko dhidi ya Uislam.
Kwani hili ni siri tena...
Waislam wametembea nchi nzima wakifanya mihadhara ya wazi kuhusu Mfumokristo.
Hili ndilo tunalosema.
Ipo kheri nyingi sana katika haya ninayoandika na ndiyo maana unaiona sijajificha niko
hapa kwa jina langu kamili na picha zangu ziko humu nyingi tu.
Mimi nimesimama kwenye ukweli na huu ukweli utakapofuatiliwa ndipo kheri itapatikana.
Vinginevyo tutakujajuta sote.
Soma hapo chini habari kutoka Lalago, Handeni.
Unadhani huu ni utani kuwa watu wanashukiwa wameua na hawajakamatwa?
BREAKING NEWS!
Insha Allah kesho Jumatatu 19 May 2014
Baba yake mzazi Rajab Omar Mtana, Mzee Omar Mtana akifuatana na Amir (Kiongozi) wa Waislam wa kijiji cha Lulago Sheikh Salim Kisailo watakwenda kuonana na Uongozi wa Juu wa Polisi Mkoa wa Tanga kutaka kujua iweje wale waliompiga mwanae Rajab Omar Mtana ambae hadi leo hajaonekana (na inasadikiwa ameuawa) hawajakamatwa licha ya taarifa kufikishwa polisi na jalada SON/RB346/2014 kufunguliwa.
No comments:
Post a Comment