Wednesday, 21 May 2014

KUTOKA JF: JIBU LA MTU ALIYENITUKANIA WAZEE NA WALIMU WANGU


 Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

Quote By Buchanan View Post
Wazee wenyewe wa vibaraghashia washike kalamu mwenyewe na kujiandikia hiyo "historia mpya!"

Buchanan,
Inaelekea wewe uwelewa wako uko chini sana.
Hata adabu yako vilevile iko chini sana nasikitika kusema.

Uvaaji wa barghashia unakuudhi nini wewe kiasi una tukejeli sisi wavaaji na na wazee wetu waliotufunza kujisitiri hivyo ndugu yangu?

Huu ni utamaduni wetu watu wa pwani kama vile unavyotuona tunavaa kanzu za dariz na makubadhi.

Mimi sikucheki wewe unapoingia msalani na karatasi ukajifutanazo ilhali maji yapo.


Sikubezi na kukunyayapaa kuwa hujui ''hygiene.''

Nafanya staha kwa kuwa najua huo ni utamaduni wako.
Wala sikucheki kuwa hujui tohara.

Sana sana ninakutamania ujue mambo haya ili unufaike kama ninavyonufaika mimi na hali ya usafi wa kiwiliwili changu.

''Mohamed nataka nguo za mume wangu zinukie kama kanzu yako nifanyeje?’’
Dada wa Kikristo ananambia siku moja.

Salamu hizi nikazifikisha kwa mke wangu.
Mke wangu akanunua chetezo na udi akampelekea zawadi yule dada.

Mke wangu ananihadithia, anasema wakajifungia ‘’bedroom ya huyu dada wakafukiza udi chumba kizima kisha akamwambia sasa lete
mashati na suti za bwana tumkomeshe leo.

Sitaki kukueleza furaha ya yule bwana alivyoingia chumbani kulala alipopigwa na harufu nzuri ya shuka zilizofukizwa udi.

Usiku kanipigia simu, ''Mohamed old boy, you owe me one tomorrow let us have dinner the four of us aisee nyinyi Waswahili kweli mnafaidi...''

Niangalie picha nyingi mimi nimevaa bargashia.
Ninazo vilevile designer suit za Yves Saint Laurent na Gucci kukutajia chache.



Angalia kwa Makini Nimevaa Bargashia Designer Shirt na Designer Jeans
Katika Mfuko wa Shati Nimechomeka Kalamu ya Cross Huo Mkoba
una Lap Top (State of the Art) Niko Maulidini Lamu

Buchanan,
Jifunze adab.

Si vizuri kudharau mila na tamaduni za watu wengine hata kama wewe unahisi utamaduni wa kuigwa ni ule wa Wazungu.

Turudi kwenye mada.

Unaona hiki kitabu cha Abdul Sykes:



Kuna baadhi mimi nimesomeshwa na wavaa bargashia nitakupa majina yao – Sheikh Ali bin Abbas, Bilali Rehani Waikela, Yusuf Chembera, Salum Mpunga na akina mama wavaa mabaibui – Bi. Mwamvua Masha, Mwalimu Sakina bint Arab na wengine wengi.

Nimesomeshwa historia na watu mimi nikiwa nimekaa kwenye jamvi namuelekea mwalimu wangu na mwalimu wangu anazungumza (lecture style).

Wengi wa hawa watu hawakusoma, ''secular edcation,'' lakini walikuwa wajuzi wa kile walichosoma.

Nikija siku ya pili mwalimu wangu ananiuliza, ''Ehe, jana tuliishia wapi?''

Nami namwambia mathalan, ''Sheikh Hassan bin Amir alivyompokea Nyerere katika madras yake pale Mtaa wa Amani mwaka 1954.''

''Taib, basi ikawa Sheikh...'' Mwalimu wangu anendelea.

Mimi nimesomeshwa na watu hawa na leo unaniona hapa elimu ile niliyoteka kwao naitoa kwa wengine humu Jamii Forums na kote ninakoalikwa dunia nzima.

Maalim Haruna ndiyo aliyenifunza ''the art of debating,'' namtaja sana hapa nikitegemea na nyinyi mfaidike na ilm ile muache matusi na kebehi.

Wapi.
Sikio la kufa.

Buchanan,(Nilipata kukuambia kuwa jina lako linanikumbusha kituo changu cha treni Glasgow).

Hata ukinitazama katika video au unanisikiliza katika audio hivyo ninavyozungumza ndiyo nilivyowasikia walimu wangu wavaa bargashia wakizungumza.

(Sikiliza hapa mwalimu wangu Sheikh Ali bin Abbas alivyonifunza kutoa darsa kama Sheikh Hassan bin Amir alivyokuwa akifanya naiga style na utulivu katika kutamka maneno: http://www.mohammedsaid.com/2014/05/...nia-uhuru.html)

Muone mwalimu wangu hapa chini Sheikh Ali bin Abbas mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Hassan bin Amir:




Niko na mwalimu wangu Sheikh Ali bin Abbas miaka michache
kabla ya kifo Chake 2014



Professor wa African History James Brenan kutoka Marekani
Anateka Ilm Kutoka kwa Sheikh Ali bin Abbas

Buchanan,
Nadhani ujumbe umekufikia sawia.
Last edited by Mohamed Said; Today at 19:37.
Edit / Delete

No comments: