Wednesday, 21 May 2014

KUTOKA JF: SHEIKH HASSAN BIN AMIR


  1. #181   Report Post    
    Mag3's Avatar
    JF Tanzanite MemberArray
    Join Date : 31st May 2008
    Posts : 4,338
    Rep Power : 1330305

    Likes Received
    3484

    Likes Given
    3413

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By kilio changu View Post
    Mohamed Said. " Sababu ilikuwa Sheikh Hassan bin Amir alikuwa anataka kujenga Chuo Kikuu "
    kilio changu;


    1. Kwanza, huyo Sheikh Hassan bin Amir hakuwa Mtanganyika...sijui kwa nini hicho chuo Kikuu hakutaka kijengwe kwaoMakunduchi, Zanzibar alikozaliwa mwaka 1880!
    2. Pili, Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Kiongozi wa Jamiatul Islamiya fi Tanganyika kilichoongoza harakati za kupinga ujio waEAMWS mwaka 1945 Jumuiya ya Ismailia ilipotaka kufungua tawi hapa nchini Tanganyika.
    3. Tatu, Kifo cha chama cha siasa cha AMNUT mara tu baada ya uhuru,kilisababisha waliokuwa viongozi wake kukimbilia EAMWS na kuendesha shughuli zao za siasa kupitia mgongo wa Jumuiya hiyo ya Ismailia kinyume cha sheria.
    4. Nne, ni hali hiyo ilisababisha EAMWS ipigwe marufuku na kusababisha Sheikh Hassan bin Amir kufungishwa virago na kurejeshwa kwao Makunduchi, Unguja mwaka 1968
    5. Tano, shughuli za wanajumuiya ya Ismailia chini ya kiongozi wao Aga Khan hazikuwahi kupigwa marufuku na hadi leo shule na hospitali nyingi walizozijenga zipo na zinaendelea kutoa huduma za kijamii.
    6. Mwisho, nazidi kuwatahadharisha wananchi wenzangu; hawa wachochezi na wapuuzi wanaojaribu kupandikiza hizi chuki kwa mgongo wa dini, waogopeni kama ukoma...hawana nia njema.


    cc: RitzMUNGU SI MZUNGUGs-300FaizaFoxyMohamed SaidtofyoIkengya,
    s.crony likes this.

    Its funny how sometimes
    the very people you'd take a bullet for,
    are the ones behind the trigger.
  2. #182   Report Post    
    Abunuas's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 8th April 2011
    Posts : 1,623
    Rep Power : 787

    Likes Received
    208

    Likes Given
    18

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By Kishimbe wa Kishimbe View Post
    Kwenye bao na vijiwe vya kahawa kwani hujui waswahili na uswahili? Mswahili bwana!?
    malipo ya kazi kubwa walioifanya wazee hawa ni matusi na kejeli kutoka kwenu. ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.
  3. #183   Report Post    
    Abunuas's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 8th April 2011
    Posts : 1,623
    Rep Power : 787

    Likes Received
    208

    Likes Given
    18

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By Remote View Post
    wapo umesahau siku kikwete alipoita wazee wa dar nz kuanza kuwaambia walimu sitaki kura zenu.. walikuwa wanamshingilia kwa bashasha na barkashia zao.
    acha dharau bhana, sisi tunaongelea wapigania uhuru ambao bila shaka wengi wao wametangulia mbele ya haki. malipo ya kazi kubwa walioifanya ni matusi na kejeli kama hizi unazoziandika hapa. ama kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni.
  4. #184   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 5,475
    Rep Power : 66147

    Likes Received
    3809

    Likes Given
    223

    Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

    Quote By Mag3 View Post
    kilio changu;


    1. Kwanza, huyo Sheikh Hassan bin Amir hakuwa Mtanganyika...sijui kwa nini hicho chuo Kikuu hakutaka kijengwe kwao Makunduchi, Zanzibar alikozaliwa mwaka 1880!
    2. Pili, Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Kiongozi wa Jamiatul Islamiya fi Tanganyika kilichoongoza harakati za kupinga ujio waEAMWS mwaka 1945 Jumuiya ya Ismailia ilipotaka kufungua tawi hapa nchini Tanganyika.
    3. Tatu, Kifo cha chama cha siasa cha AMNUT mara tu baada ya uhuru,kilisababisha waliokuwa viongozi wake kukimbilia EAMWS na kuendesha shughuli zao za siasa kupitia mgongo wa Jumuiya hiyo ya Ismailia kinyume cha sheria.
    4. Nne, ni hali hiyo ilisababisha EAMWS ipigwe marufuku na kusababisha Sheikh Hassan bin Amir kufungishwa virago na kurejeshwa kwao Makunduchi, Unguja mwaka 1968
    5. Tano, shughuli za wanajumuiya ya Ismailia chini ya kiongozi wao Aga Khan hazikuwahi kupigwa marufuku na hadi leo shule na hospitali nyingi walizozijenga zipo na zinaendelea kutoa huduma za kijamii.
    6. Mwisho, nazidi kuwatahadharisha wananchi wenzangu; hawa wachochezi na wapuuzi wanaojaribu kupandikiza hizi chuki kwa mgongo wa dini, waogopeni kama ukoma...hawana nia njema.


    cc: RitzMUNGU SI MZUNGUGs-300FaizaFoxyMohamed SaidtofyoIkengya,
    Wanajamvi,Hapo chini naweka swali la mleta mada (nyeusi) na jibu lake (buluu).

    Kwanza, huyo Sheikh Hassan bin Amir hakuwa Mtanganyika...sijui kwa nini hicho chuo Kikuu hakutaka kijengwe kwao Makunduchi, Zanzibar alikozaliwa mwaka 1880!

    Hoja ya kwanini chuo hakikujengwa ''kwao'' Sheikh Hassan bin Amir ni kuwa Uislam hauna mipaka, Waislam wote ni ndugu. Ukitia ukabila, eneo, katika Uislam au rangi basi jua umetoka katika mafunzo ya Allah. Naona mweka mada kahamaki zinakuja lugha za ''huyo Sheikh Hassan...'' na ''kwao.'' Sisi hapa tuna Wamishionari Wazungu wa kila nchi toka miaka ya 1800 na hatujawaambia warudi kwao au hizo shule na hospitali wakajenge kwao. Hamaki kwa hakika hupoteza uwezo wa kufikiri.
    Pili, Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Kiongozi wa Jamiatul Islamiya fi Tanganyika kilichoongoza harakati za kupinga ujio wa EAMWSmwaka 1945 Jumuiya ya Ismailia ilipotaka kufungua tawi hapa nchini Tanganyika.

    Sheikh Hassan bin Amir hakuwa kiongozi wa Al Ajamiatul Islamiyya fi Tanganyika. Sheikh Hassan alikuwa kiongozi wa Daawat Islamiyya na hii ilikuwa baada ya uhuru. Sheikh Hassan bin Amir alikuwa Mufti. Hakuna taasisi yoyote iliyopinga EAMWS. Mweka mada ajifunze historia ya Waislam kwanza kabla ya kuandika hii itarahisisha mjadala
    Tatu, Kifo cha chama cha siasa cha AMNUT mara tu baada ya uhuru,kilisababisha waliokuwa viongozi wake kukimbilia EAMWS na kuendesha shughuli zao za siasa kupitia mgongo wa Jumuiya hiyo ya Ismailia kinyume cha sheria.

    AMNUT haikupata kuwa na nguvu yoyote katika jamii ya Waislam Tanganyika na hata Zanzibar hakikuungwa mkono. Katibu wake SheikhAbdulkarim Abdulwahid alijitahidi sana lakini hakufanikiwa kuungwa mkono na Waislam.
    Nne, ni hali hiyo ilisababisha EAMWS ipigwe marufuku na kusababisha Sheikh Hassan bin Amir kufungishwa virago na kurejeshwa kwao Makunduchi, Unguja mwaka 1968
    Hapa jibu linapatikana kwa majibu niliyotoa hapo juu. Naona umehamaki maana lugha ya kiungwana haipo tena inakuja hasira na lugha ya ''kufungishwa virago...'' Inaelekea huijui historia ya Sheikh Hassan bin Amir. Kipo kitabu kimeandikwa na Dr. Issa Ziddi kuhusu maisha ya Sheikh Hassan bin Amir kitafute ukisosome. Mimi nimetoa muhadhara wa Sheikh Hassan bin Amir Zanzibar University mwaka 2004 ukipenda unaweza kusoma hiyo paper hapo chini: MUFTI SHEIKH HASSAN BIN AMEIR (1880 - 1979) - Mohamed SaidSheikh Hassan bin Amir alifukuzwa nchini na EAMWS kwa sababu alitaka kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam. Hayo usemayo ni maarufu kwa Waislam na waliokuwa wakieneza propaganda hizo pia wanafahamika kwa majina yao.

    Tano, shughuli za wanajumuiya ya Ismailia chini ya kiongozi wao Aga Khan hazikuwahi kupigwa marufuku na hadi leo shule na hospitali nyingi walizozijenga zipo na zinaendelea kutoa huduma za kijamii.

    Inaelekea mweka mada hajui tofauti kati ya shughuli za Aga Khan na EAMWS akisoma hiyo paper hapo juu itamfungua macho.
    Mwisho, nazidi kuwatahadharisha wananchi wenzangu; hawa wachochezi na wapuuzi wanaojaribu kupandikiza hizi chuki kwa mgongo wa dini, waogopeni kama ukoma...hawana nia njema.

    Naona mweka mada kahamaki tena na lugha zisizofaa kwenye mjadala zinatokeza za ''wachochezi na wapuuzi.'' Nami namtoa hofu kuwa hakuna anae chochea chochote hapa ila kinachofanyika au ninachokifanya ni kueleza ukweli wa mambo baada ya Waislam na Uislam kupakwa matope kwa miaka mingi na propaganda. Kwa ajili hii basi hapana haja yoyote ya kuwatahadharisha watu lolote. Tujadiliane tu ili umma ujue ukweli wa mambo.

    Mweka mada alipata kuwatahadharisha watu kuwa wasinisome kwa kuwa mimi ni mtu wa ''kijiweni.'' Nilimpa jibu. Hakunijibu kakaa kimya hadi leo.





No comments: