[QUOTE=WildCard;9664661]Thread umeianza mwenyewe Ritz.
Haukuweka picha za enzi za TAA chama ambacho hakikuwa
cha SIASA( ukweli huu mchungu kwa baadhi yenu). Tanganyika
haikuwahi kuwa na chama cha siasa kikiitwa AA wala TAA.
Mwalimu alikuwa KIONGOZI MKUU wa harakati hizi. Hakuwa kila
kitu hata kama angejaribu kuwa hivo. Akawa Rais wa KWANZA
wa TANU na wa mwisho, akawa Rais wa KWANZA wa Tanganyika
huru na wa mwisho, akawa Rais wa KWANZA wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, akawa Mwenyekiti wa KWANZA wa CCM.
Kwa nini asionekane hivo?[/QUOTE]
WildCard,
Yako mengi sana lakini nadhani haya yanakutosha katika kueleza historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ni kweli TAA hakikuwa chama cha siasa lakini wewe unadhani mwaka 1929 akina Kleist wangepeleka maombi ya kusajili chama cha siasa wangekubaliwa na Waingereza?TAA hakikuwa chama cha siasa lakini kilifanya siasa kuanzia mwaka 1950 pale akina Abdul Sykes na Hamza Mwapachu walipouondoa kwa nguvu uongozi wa Mwalimu Thomas Plantan akiwa rais na Clement Mohamed Mtamila akiwa katibu. Kuanzia hapo TAA ikawa na TAA Political Subcommittee kamati ambamo ndani yake walikuwapo Sheikh Hassan bin Amir, Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Stephen Mhando, John Rupia na Said Chaurembo.
Thomas Soudt Plantan |
Kamati hii ndiyo iliyokuja kuunda TANU na ndiyo iliyotoa uamuzi wa kuwapekeka Japhet Kirilo, Saadan Abdu Kandoro na Abbas Sykes nchi nzima kuwaeleza watu madhila ya ukoloni. Hii ni baada ya Kirilo na Earle Seaton kurejea UNO walikokwenda kueleza dhulma ya ardhi ya Wameru. Huyu Earle Seaton alikuwa rafiki yake Abdul Sykes na alikuwa mwanasheria Moshi. Sasa Abdul alimleta katika ile TAA Political Subcommittee awashauri kuhusu sheria katika ''Mandate Territories.''
Earle Seaton Nyerere |
Earle Seaton |
Nakurudisha nyuma nikufahamishe kuwa katika kuiandika ile katiba kama Gavana alivyowataka Waafrika wafanye mwaka 1949 chini ya Constitutional Development Committee, Seaton alitoa msaada mkubwa sana. Wajumbe wa TAA katika kuandika hii katiba ni wale wajumbe hapo juu wa TAA Political Subcommittee. Kipindi hiki ndicho kipindi Abdul Sykes alikwenda kuonana na Kenyatta Nairobi. Hii ilikuwa 1950. Ally Sykes na Denis Phombeah wakaalikwa na Keneth Kaunda mwaka 1953 kuhudhuria mkutano wa wapigania uhuru wa Afrika Chini ya Jangwa la Sahara. Mkutano ulikuwa ufanyike Lusaka.
Katika haya yote ikiwa WildCard huoni siasa unaona starehe hii kwa kweli ni bahati mbaya sana kwetu sote. Waingereza wao waliona hii ni siasa na TAA ilikuwa imekiuka sheria. Ndipo walipotoa Sekula Na. 5 1953 na wakafatisha na nyingine mwaka huo huo Sekula Na. 6 ikiwaonya watumishi wa serikali kujiingiza katika siasa.
Yako mengi sana lakini nadhani haya yanakutosha katika kueleza historia ya wazee wangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
No comments:
Post a Comment