Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
salam alykum: sheikh Mohammed bin Said. Natabaruk kidogo hapa jamvini kwa kuuliza zile harakati zote zilofanywa na Nyerere na kuivamia jan 1964ZNZ kwa kudhulumu roho za maelfu za watu wasokua na hatia yeyote hawa wazee wetu waliomzunguka Nyerere kwa kila harakati za Tanganyika walikua hawajiliona hilo?
Mimi nitakupa fikra zangu binafsi kuhusu jambo hili.
Ziko dalili nyingi sana kuwa wazee wetu waliokuwa katikati ya siasa
wakati ule walijua mpango wa kupindua serikali ya Sheikh Mohamed
Shamte.
Lile ambalo hawakulijua ni kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki Sakura
na Kipumbwi iliyokuwa imetayarishwa pale ili kuvamia Zanzibar.
Wazee wetu walikujapata na mshtuko pale iliowadhihirikia kuwa kuna
mauaji mengi sana yametendeka bila sababu na mauaji hayo ni baada
ya serikali ikiwa imeshaanguka.
Ndiyo maana mtu kama Ali Mwinyi Tambwe katika maisha yake
yote hakutaka kunasibishwa na mapinduzi ya Zanzibar ingawa yeye
alikuwa katika ya mipango ile.
Nimelitaja jina la Ali Mwinyi Tambwe kwa kuwa lilikuja kuwa dhahir
katika kitabu cha Dk. Harith Ghassany na katika kuadhimisha miaka
50 ya mapinduzi kapewa nishani.
Lakini wako wazee wetu wengine bado wahai na waliujua mpango
wote wa mapinduzi na inajulikana kuwa walihusika lakini hadi leo
wamepiga kimya.
Hivi juzi tu nimepokea nakala ya barua kutoka kwa sahib yangu aliyeko
Northwestern University, Marekani barua inayotoka kwa Abdulwahid
Sykes kwenda kwa Aboud Jumbe.
Huyu sahib wangu tulifahamiana nilipokwenda kuzungumza Northwestern
University na nilimpa nakala ya kitabu cha Sykes.
Kwa kujua utafiti nilokwushafanya kuhusu maisha ya Abdul Sykes
ndiyo akaniletea barua hii.
Barua hii imeandikwa mwaka 1967.
Ukisoma barua hii inaonyesha ule ukaribu waliokuwanao hawa watu
wawili.
Hii inaonyesha kuwa udugu wao una historia ndefu kwa hiyo wana
mengi.
Issa bin Nasser Al-Ismaily alipata kumuuliza Abdul Sykes miaka
mingi baada ya yale mauaji kutokea kuwa ilikuwaje ikawa vile.
Jibu la Abdul Sykes ni kuwa alimsihi Sheikh Issa wasizungumze
habari za Zanzibar kwani huenda zikavunja udugu wao.
Kisa hiki Sheikh Issa kakieleza katika kitabu chake ''Zanzibar:
Kinyan'ganyiro na Utumwa.''
Dk. Ghassany halikadhalika kutokana na umuhimu wake na yeye
kakitaja katika kitabu chake.
Sasa swali la kujiuliza ni hili, kwa nini Abdul Sykes alijibu vile?
Nini alikuwa anatakakuficha na hakupenda Sheikh Issa akijue?
Alipokufa David Kimche magazeti mengi Ulaya yaliandika taazia
yake.
Ukitaka kumjua Kimche ni nani ''google,'' sina uwezo wa kumueleza
mtu huyu.
Kwa ufupi huyu alikuwa Mossad na akifahamiana na mmoja wa wazee
wetu kipindi kile cha kupanga mapinduzi ya Zanzibar.
Hivi sasa si siri tena kuwa Waisraeli pia walihusika katika mapinduzi
ya Zanzibar
Huyu mzee wangu inajulikana ingawa yeye mwenyewe anaficha kuwa
alihusika katika mipango ya mapinduzi na alikuwa karibu sana na
Wayahudi.
Baada ya kusalimiana nikamwambia kuwa Kimche amefariki.
Jibu lake, ''Ala! sikuwa na habari.''
Alionyesha kushangaa lakini nadhani kwa kunijua akajua ''I was in
the know,'' kama wasemavyo Waingereza hakuniliza kitu zaidi.
Nyerere mwenyewe hakutaka ijulikane kuwa alihusika katika njama
zile.
Hii ndiyo hali ilivyo.
Kubwa la hawa wote nilioeleza habari zao ni kuwa hawakutaka
wahusishwe na mapinduzi ya Zanzibar kwa sababu ya yale mauaji
yaliyotokea na inasadikiwa mauaji mengi yalifanywa na Wamakonde
kutoka katika Mashamba yale ya mkonge ya Sakura.
Ilimchukua Victor Mkello takriban miaka mitatu hadi siku moja
alipoamua kutoa yake ya moyoni kuhusu mchango wake katika
mapinduzi ya Zanzibar na hapo ndipo alipomweleza Dk. Ghassany
nini kilipitika.
Dk. Ghassany akienda Muscat na kurudi Tanga kwa subira kubwa
akisubiri siku Mkello atakapofunguka.
Ingawa mmoja wa washirika wake Mzee Mohamed Omar Mkwawa
tayari alikuwa keshaeleza mpango mzima lakini kauli ya Mkello kutoka
kinywani kwake mwenyewe ilikuwa muhimu kusadikisha lile tayari
lililokuwa wazi.
Baada ya mapinduzi yale kufanikiwa si Nyerere wala Karume sasa
walikuwa hata kwa chembe wanawahitajia hawa wazee wetu kwa
hiyo Karume alifanya hayo yote aliyofanya bila ya kuwepo mtu hata
mmoja wa kumzindua au kumshika mkono kumtanabaisha hata kwa
mbali na kumwambia, ''Muogope Allah.''
Kwa kukhitimisha ni kuwa hili jambo la roho za watu waliodhulumiwa bure
halitakwisha na litakuwa linaturejea miaka nenda miaka rudi mpaka pale
tutakapokubali ukweli kuwa limetokea na yalikuwa ni makosa, watu wakaa
wakalizungumza wakataka msamaha kwa Allah na ikapigwa fatha.
Hanga kabla hajafa alijuta kwa yale yalotokea katika mapinduzi na akataka
msamaha kwa Allah na kaacha usia khasa kuhusu hatari ya ubaguzi.
Atakae kujua zaidi kuhusu habari hizi na akisome kitabu cha Dk. Ghassany
mimi nimepita mle mle alimopita yeye.
Mzee Mohamed Omari Mkwawa akikisoma kitabu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru,'' Nyumbani Kwangu Tanga Mwaka 2010 Kilipotoka
Wakati wa Utafiti nikiwa pwani ya Kipumbwi ambako majahazi ya mamluki wa Kimakonde yalipokuwa yanaondokea
kulekea Zanzibar kushiriki katika mapinduzi hii ilikuwa mwaka 2003
Victor Mkello Kama Alivyokuwa mwaka 2003Last edited by Mohamed Said; Today at 08:07.
Wednesday, 28 May 2014
KUTOKA JF: ILIKUWAJE MAUAJI YAKATOKEA ZANZIBAR NA NYERERE NA WALIOKUWA KARIBU NA YEYE WAKAWA KIMYA?
Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment