Wednesday, 14 May 2014

TV IMAAN KUPITIA STARTIMES DAR ES SALAAM: FUATILIA ''WALIOACHA ALAMA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA''



TV IMAAN IKO HEWANI 

Kwenye King'amuzi cha Startimes
Ingia Default Settings
Bonyeza Yes
Itakupeleka Kwenye Automatic Search
Ingia Channel 110

TV Imaan kituo cha televisheni chini ya Islamic Foundation, Morogoro hii leo In Sha Allah kitaanza kurusha matangazo yake kupitia Startimes kwa Mkoa wa Dar es Salaam.

Fuatilia kipindi ''Walioacha Alama Katika Historia ya Tanzania,'' ambamo Mohamed Said atafanya mahojiano na wale waliosukuma gurudumu la historia ya Tanzania....


Vijana wa TV Imaan Wakiwa Kazini Bwawani Hotel Zanzibar
Abbas Sykes Akihojiwa na TV Imaan Kuhusu Harakati za Kupigania
Uhuru wa Tanganyika
Salim Rashid Akihojiwa na TV Imaan  Kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano
Ishaka Kihemba Akimhoji Mzee Hassan Nassoro Moyo Hoteli
ya Bwawani Kuhusu Maridhiano Zanzibar

Mtoto wa Sheikh Mohamed Shamte Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Zanzibar
Baraka Shamte Akihojiwa na TV Imaan kuhusu baba yake na Msimamo wake
Yeye Baraka Shamte Kuhusu Mapinduzi
Mzee Kitwana Selemani Kondo
Akihojiwa Nyumbani Kwake na TV Imaan


Vilevile vipo vipindi vingine vingi vya kuuelewa Uislam kwa watazamaji wa kila rika vipindi ambavyo vinaelimisha, kuburudisha, kutuliza akili ya mja na kumjengea uwezo mkubwa wa kuijua dini yake kwa wepesi na kumjua Allah Subhana wa Taala.

Fuatilia...

No comments: