Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
e: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
''Kumbukumbu za Abbas Kleist Sykes''(Picha kwa Hisani ya TV Imaan)Akihojiwa na Mohamed SaidKipindi cha Walioacha Alama Katika HistoriaWanajamvi,Inaelekea mnakasha unaelekea ukingoni.Kwa kweli mjadala wa maneno pamoja na picha, hii ya picha ni staili mpyaimeongeza sana raha kwa wasikilizaji.Picha hizi ni adimu sana.Ni picha ambazo ungetegemea kuzikuta zimepamba kuta za ofisi ndogo yaCCM pale Lumumba.Bahati mbaya picha hizi ilivyo pale hazitakiwi kwa kuwa zitapingana na yaleyaliyomo katika historia rasmi ya Chuo Cha Kivukoni.Waislam wamekuwa wengi mno katika harakati za kudai uhuru.Mjadala unelekea kugota maana naona hoja jamaa zimewaishia kwa hiyo sasawanapanda ile pembea maarufu ya ''merry go round.''Ukweli ni kuwa historia ya TANU kama ilivyo kwa ukweli wake lazima iwatishebaadhi ya watu kwa sababu ambazo sasa ziko wazi.Kisa cha Abdul Sykes ni kisa cha kipekee katika wanasiasa wote waliopitakatika nchi yetu.Nyerere mwenyewe hakupitia yale aliyopitia Abdul Sykes kuanzia kuzaliwakatika nyumba ya siasa hadi kuja kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazihadi kuwa kiongozi katika TAA na mwisho kuwa mmoja wa watu waliofadhiliharakati za uhuru akiwa na wadogo zake wawili Ally na Abbas.Ukimleta Abdul Sykes katika historia ya TANU lazima uje na miaka zaidi ya20 ya historia na katika miaka hiyo 20 utakutana na wazalendo wengi sanapamoja na baba yake na rafiki wa baba yake kama Mzee bin Sudi.
- Nimemleta Mzee bin Sudi kwa makusudi kutaka kuonyesha jinsi siasa zaDar es Salaam zilivyokuwa katika miaka ya 1930.Sijamleta kwa kuwa ni Mmanyema.Katika miaka hiyo 1930 Mzee bin Sudi alikuwa Rais wa African Associationna Kleist alikuwa Katibu.Katika miaka hiyo 1930 Mzee bin Sudi alikuwa Rais wa Al Jamiatul Islamiyyana Kleist alikuwa Katibu.Vyama vyote hivyo viwili vilikuwa vinaongozwa na hawa watu wawili katikauongozi wake wa juu.Ukimfuta Abdul Sykes katika historia hii ya vyama ndiyo umemtoa na babayake na hao wazalendo wengine.Vilevile utakuwa umekosa kuijua historia ya karibu miaka 25.Si hilo tu kuna wengine utawakosa katika vijana walioleta mwamko mpya wasiasa baada ya Vita Kuu ya Dunia (1938 - 1945).Utamkosa Hamza Kibwana Mwapachu, utamkosa Dk. Vedasto Kyaruzi nakweli ukimkosa Dk. Kyaruzi hutoweza hata kwa mbali kueleza mchango wamadaktari wenzake wanasiasa 5 pamoja na Dk. Kyaruzi waliofanya makubwakatika TAA.Sasa vipi utamueleza Nyerere katika TAA bila ya kumtaja kwanza HamzaMwapachu na kisha Abdul Sykes?Ikiwa Abdul Sykes utamkwepa asitokee katika historia vipi utaeleza juhudiza kubadili uongozi wa TAA mwaka 1950?Juhudi ambazo kuanzia pale TAA mwaka wa 1950 kikawa chama cha siasakupitia TAA Political Subcommmitee?Vipi utamleta Chief Kidaha Makwaia katika kutafuta uongozi alioukataa 1950hadi 1952 na badala yake ukachukuliwa na Nyerere mwaka 1953?Vipi utamleta Schneider Abdillah Plantan na kaka yake Mwalimu Sauti
Thomas Plantan ambae ndiye aliyekuwa anataka kuondolewa katika nafasiya urais wa TAA bila ya kueleza chanzo cha mabadilo yale?Sasa ukiwatoa hawa katika historia vipi utamfikia mdogo wao RamadhaniMashado Plantan ambae gazeti lake la Zuhra ndilo lilikuwa la kwanza katikaTanganyika mwaka 1954 kumtangaza Nyerere kwa watu na watu wakamjua?Kumbuka hili ndilo lililokuwa gazeti pekee la Waafrika wakati ule lililokuwalikiandika siasa.Ikiwa mtafiti atataka kumpachika Nyerere kwenye TAA kisha kwenye TANUkwa kuwaondoa wazalendo hawa sasa hii itakuwa historia gani?Ikiwa mtafiti atataka kumweleza Nyerere katika harakati za kudai uhuru bilaya kuwataja wale waliokuwa huko katika majimbo ambao walimuunga mkonohii itakuwa historia gani?Wanajamvi,Nadhani kwa haya tunaweza sasa tukaufunga mjadala huu ikiwa mmeridhia.Uamuzi ni wenu ndugu zangu.Last edited by Mohamed Said; Today at 20:38.
FaizaFoxy namfahamu huyu Mzee tunaswali nae sana hapa usijali zimefika salam zako.''Kumbukumbu za Abbas Kleist Sykes''(Picha kwa Hisani ya TV Imaan)Akihojiwa na Mohamed SaidKipindi cha Walioacha Alama Katika Historia
Wanajamvi,
Inaelekea mnakasha unaelekea ukingoni.
Kwa kweli mjadala wa maneno pamoja na picha, hii ya picha ni staili mpya
imeongeza sana raha kwa wasikilizaji.
Picha hizi ni adimu sana.
Ni picha ambazo ungetegemea kuzikuta zimepamba kuta za ofisi ndogo ya
CCM pale Lumumba.
Bahati mbaya picha hizi ilivyo pale hazitakiwi kwa kuwa zitapingana na yale
yaliyomo katika historia rasmi ya Chuo Cha Kivukoni.
Waislam wamekuwa wengi mno katika harakati za kudai uhuru.
Mjadala unelekea kugota maana naona hoja jamaa zimewaishia kwa hiyo sasa
wanapanda ile pembea maarufu ya ''merry go round.''
Ukweli ni kuwa historia ya TANU kama ilivyo kwa ukweli wake lazima iwatishe
baadhi ya watu kwa sababu ambazo sasa ziko wazi.
Kisa cha Abdul Sykes ni kisa cha kipekee katika wanasiasa wote waliopita
katika nchi yetu.
Nyerere mwenyewe hakupitia yale aliyopitia Abdul Sykes kuanzia kuzaliwa
katika nyumba ya siasa hadi kuja kuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi
hadi kuwa kiongozi katika TAA na mwisho kuwa mmoja wa watu waliofadhili
harakati za uhuru akiwa na wadogo zake wawili Ally na Abbas.
Ukimleta Abdul Sykes katika historia ya TANU lazima uje na miaka zaidi ya
20 ya historia na katika miaka hiyo 20 utakutana na wazalendo wengi sana
pamoja na baba yake na rafiki wa baba yake kama Mzee bin Sudi.Nimemleta Mzee bin Sudi kwa makusudi kutaka kuonyesha jinsi siasa za
Dar es Salaam zilivyokuwa katika miaka ya 1930.
Sijamleta kwa kuwa ni Mmanyema.
Katika miaka hiyo 1930 Mzee bin Sudi alikuwa Rais wa African Association
na Kleist alikuwa Katibu.
Katika miaka hiyo 1930 Mzee bin Sudi alikuwa Rais wa Al Jamiatul Islamiyya
na Kleist alikuwa Katibu.
Vyama vyote hivyo viwili vilikuwa vinaongozwa na hawa watu wawili katika
uongozi wake wa juu.
Ukimfuta Abdul Sykes katika historia hii ya vyama ndiyo umemtoa na baba
yake na hao wazalendo wengine.
Vilevile utakuwa umekosa kuijua historia ya karibu miaka 25.
Si hilo tu kuna wengine utawakosa katika vijana walioleta mwamko mpya wa
siasa baada ya Vita Kuu ya Dunia (1938 - 1942).
Utamkosa Hamza Kibwana Mwapachu, utamkosa Dk. Vedasto Kyaruzi na
kweli ukimkosa Dk. Kyaruzi hutoweza hata kwa mbali kueleza mchango wa
madaktari wenzake wanasiasa 5 pamoja na Dk. Kyaruzi waliofanya makubwa
katika TAA.
Sasa vipi utamueleza Nyerere katika TAA bila ya kumtaja kwanza Hamza
Mwapachu na kisha Abdul Sykes?
Ikiwa Abdul Sykes utamkwepa asitokee katika historia vipi utaeleza juhudi
za kubadili uongozi wa TAA mwaka 1950?
Juhudi ambazo kuanzia pale TAA mwaka wa 1950 kikawa chama cha siasa
kupitia TAA Political Subcommmitee?
Vipi utamleta Chief Kidaha Makwaia katika kutafuta uongozi alioukataa 1950
hadi 1952 na badala yake ukachukuliwa na Nyerere mwaka 1953?
Vipi utamleta Schneider Abdillah Plantan na kaka yake Mwalimu Sauti
Thomas Plantan ambae ndiye aliyekuwa anataka kuondolewa katika nafasi
ya urais wa TAA bila ya kueleza chanzo cha mabadilo yale?
Sasa ukiwatoa hawa katika historia vipi utamfikia mdogo wao Ramadhani
Mashado Plantan ambae gazeti lake la Zuhra ndilo lilikuwa la kwanza katika
Tanganyika mwaka 1954 kumtangaza Nyerere kwa watu na watu wakamjua?
Kumbuka hili ndilo lililokuwa gazeti pekee la Waafrika wakati ule lililokuwa
likiandika siasa.
Ikiwa mtafiti atataka kumpachika Nyerere kwenye TAA kisha kwenye TANU
kwa kuwaondoa wazalendo hawa sasa hii itakuwa historia gani?
Ikiwa mtafiti atataka kumweleza Nyerere katika harakati za kudai uhuru bila
ya kuwataja wale waliokuwa huko katika majimbo ambao walimuunga mkono
hii itakuwa historia gani?
Wanajamvi,
Nadhani kwa haya tunaweza sasa tukaufunga mjadala huu ikiwa mmeridhia.
Uamuzi ni wenu ndugu zangu.Last edited by Mohamed Said; Today at 20:38.
By FaizaFoxy
Utatuwacha wapweke na tumenyong'onyea. Kama inabidi basi hatuna budi kusema;
Ahsante Al Alama Mohamed Said, AlhamduliLlahi, tumefyonza ilm kedekede. Tunakupa "ruksa" kwa shingo upande na kwa sharti moja "duchu", utuandalie darsa jingine siku za karibuni.
Tunamshukuru Allah aliyekupatia wasaa kutupa hizi ilm zilokuchukuwa muda mrefu kuzi "compile".
Amma kwa hakika, leo hii umetufanya tujivune na tujivunie wazee wetu kwa umahiri wao na muono wao. Tumefarijika sana uwepo wako muda mwingi humu, inataka moyo na ujasiri mkubwa. Kwa uhakika na bila shaka, twathubutu kusema moyo wako ulojawa na hamasa na ujasiri uso na kifani tumeushuhudia.
Haijapatapo kutokea Tanzania hii, Mwandishi yeyote wa maandiko ya ki akademia akatokeza kwenye mijadala kama hii kuelezea, kufafanua na kutetea hoja na maandiko yake kama ufanyavyo wewe kwa muda mrefu sana humu JF.
Sisi tuwachie wataokuja na masuala yao humu tuta "deal" nao, na ukiona inabidi uingile basi twakuomba usisite kufanya hivyo.
Wa bi Llahi Tawafiq.
Ahsante kwa maneno mazuri yaliyonifariji na kunipa nguvu.
Allah akujaze kheri.
Umenisomesha mengi sana dada yangu.
Sina maneno ya kukushukuru wewe wala wanajamvi wengine wote hata wale
waliokuwa tukipingana.
Tuesday, 10 June 2014
KUTOKA JF: ATHARI YA KUJARIBU KUIBADILI HISTORIA YA TANU NA YA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
Ahsante kwa maneno mazuri yaliyonifariji na kunipa nguvu.
Allah akujaze kheri.
Umenisomesha mengi sana dada yangu.
Sina maneno ya kukushukuru wewe wala wanajamvi wengine wote hata wale
waliokuwa tukipingana.
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment