Tuesday, 3 June 2014

KUTOKA JF: DK. WBK MWANJISI, CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA JK NYERERE


*      Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia
*      mbele ya haki
Quote By Gagnija View Post
Alikuwa kipenzi cha wa-Tanganyika. Picha uliyoiweka ni ya Zanzibar kwenye
mazishi ya Karume aliyeuwawa kwa risasi, ulitegemea aende huko kama anakwenda
harusini? Labda kama alivyosema Jaji Werema, sisi wengine mambo ya huko hatuyajui
na hayatuhusu. Tuwaachie wenyewe.

Turudi kwenye mada, wale wazee waliompokea Nyerere Dar walisukumwa na kitu gani
hasa hadi kumchagua kuwaongoza mtu toka kijijini bara asiyejua hata kula chapati?

Gagnija,

Nakuomba upunguze hamaki.

Maswali unayouliza ni mazuri na yanaweza kunogesha sana mnakasha huu
ukawa wenye tija na vilevile kustarehesha wasikilizaji na wachangiaji ila
kwa sharti kuwa tuondoe hamaki zetu.

Tujiepushe na lugha, kwa kutumia lugha ya Bunge la Tanzania, tujiepushe
na lugha za ''maudhi.''

Vyakula kama chapati huendana na utamaduni wa watu.
Mie binafsi nikipata tabu sana na wenzangu tukisafiri.

Wanataka tukale chakula kwenye baa na wanaagiza pombe, ugali na nyama
ya kuchoma.

Nikitaabika sana la kwanza huo ugali na kisha kula chakula baa.

Lakini ndiyo maisha kila mtu ana mazoea aliyotokanayo kwao kwa hiyo kwa
sasa tuachane na hayo masuala ya ''chapati.''

Turudi kwenye mada.
Ukweli ni kuwa TAA ilikuwa imefika mahali haiendei mbele wala hairudi nyuma.

Walikuwa hawajaitisha ''delegates conference'' kwa miaka 4 toka ule uchaguzi
wa 1950 uliomtia madarakani Abdul Sykes na Dk. Vedasto Kyaruzi.

Lakini katika hii miaka 4 TAA ilikuwa imefanya mambo makubwa katika uwanja
wa siasa kiasi cha serikali kutoa onyo kupitia Government Circular No. 5 na 6
ya 1953.

Sasa haya ninayoeleza hapa chini ni katika mazungumzo yangu na Tewa Said 
Tewa tulikyokuwa tukifanya mara kwa mara.

Tewa anasema Abdul ndiye aliyekuwa akizuia kuitishwa kwa hiyo ''delegates
conference,'' na mimi natumia neno lilelile alilokuwa akipenda kutumia Mzee 
Tewa, ''delegates conference.''

Nilimuuliza Mzee Tewa, ''Vipi mtu mmoja anaweza kuzuia msiitishe mkutano
kwa miaka 4?''

Jibu alonipa lilikuwa, ‘’TAA ilikuwa haina fedha zake yenyewe na sisi katika
masuala ya fedha tukimtegemea sana Abdul.''

Katika majibu haya mimi nikafanya, ''deduction,'' kutoka taarifa nyingine
ambazo nilizokuwanazo kuhusu siasa katika kipindi kile.

Kipindi hiki cha 1950 - 1953 ndicho kipindi ambacho Abdul alikuwa na vikao
visivyokwisha nyumbani kwake na Chief David Kidaha Makwaia wa Shinyanga
kuhusu yeye kujitoa kwa Waingereza na kuja kuongoza TAA ili waunde TANU.

Wakati ule Chief Kidaha alikuwa katika Legico.



Mzee Tewa hili la kumleta Chief Kidaha TAA akilijua na alinieleza lakini yeye
hakuunganisha kama moja ya sababu ya Abdul kuchelewesha kuitisha kwa
wakati ''delegates conference,'' kwa kumsubiri Chief Kidaha.

Kwa nini Abdul alihangaika sana na Chief Kidaha?
Hili swali ni mojawapo ya maswali ambayo mie binafsi yakinitaabisha sana.

Jibu nililipata katika Nyaraka za Sykes.

Katika nyaraka hizi nimmesoma Dk. Wilbard Mwanjisi akiandika mwaka 1951
akisema maneno hayo hapo chini katika italics:

The conflict between TAGSA and the government was not to end there.
In his inaugural speech to TAGSA members upon his election as president,
Dr Mwanjisi attacked the British and called them ‘uncivilised’, emphasizing
in his speech the fact that human intelligence has nothing to do with race
or skin pigmentation; and that all human beings were born equal and therefore
subject to the same limitations.

Dr Mwanjisi called upon the government to allow civil servants to take part
in politics with the following words:

‘’In recent session of the Legico, Honorable Chief Kidaha Makwaia, advised
the Government to consider the question of allowing civil servants to take
part in open politics, I completely and fully support that young chief, the
greatest African politician of our day in this territory. There are many great
brains of his calibre but sorry, they are being wasted just because they are
civil servants.’’ [1] (
‘Doctor Mwanjisi Speaks to TAGSA’ 22 nd December, 
1951. Sykes' Papers).

Chief Kidaha alipowakatalia TAA ndiyo sasa 1952 hapo akatokea Nyerere na
kisomo cha hali ya juu pamoja na Hamza Mwapachu kumueleza Abdul bila
kuuma maneno kuwa yeye anamjua vyema Nyerere na anaweza akakisaidia
chama pakubwa.

Kwa ufahamu wangu hali ilikuwa hivi na ndivyo Nyerere alivyoingia TAA pale
Makao Makuu ya TAA, New Street.

Ilikuwa baada ya hapa na Nyerere kuchukua uongozi kama rais wa TAA 1953
ndipo sasa alipojulishwa kwa Sheikh Hassan bin Amir na kwa wazee wengine.

Tatizo linalowakumba wengi ni huku kutojua hali halisi ya siasa za wakati ule
na ‘’advantage,’’ kubwa niliyokuwanayo mie dhidi ya wengi hapa jamvini ni
kuwa mimi ninazo taarifa ambazo hata hawa viongozi wa leo katika CCM
hawana na waliokuwanazo weshatangulia mbele ya haki

Bila ya taarifa hizi mtu atakuwa anapigiapigia pembeni tu hana mbele wala
nyuma.

Kilichojenga TANU si ule mkutano wa Julai 7, 1954.
Historia ya TANU ilijengwa kabla ya saba saba.

Kwa kumalizia na katika mojawapo ya maswali ambayo sijapata majibu hadi
hii leo ni kuwa Dk. Mwanjisi na Chief Kidaha walikuja kuwa maadui wakubwa
na Nyerere baada ya uhuru na wote wawili wakakimbia nchi na kwenda kuishi
Kenya.




No comments: