Sunday, 8 June 2014

KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU - DK. VEDASTO KYARUZI, KASELLA BANTU NA JULIUS NYERERE


1.      Mohamed Said is online now 
Today 06:30
#1406   Report Post    
Mohamed Said's Avatar
JF Senior Expert Memberhttp://www.jamiiforums.com/images/verified.pngArray
Join Date : 2nd November 2008
Posts : 5,679
Rep Power : 66189
Likes Received
4252
Likes Given
234
Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki
Quote By Mohamed Said View Post
Pondamali,
Hilo usemalo wala halina wasiwasi umesema kweli.

Abdul Sykes alikuwa katibu na kaimu rais wa TAA toka Dk. Kyaruzi alipopewa
uhamisho.

Wala sina haja ya kuweka sawa ninayoandika hilo mie nikilijua siku zote.
Kwani pamezuka nini?

Vipi kuhusu habari za Mzee Kasella Bantu.

Ungependa nikuwekee hapa habari zake zaidi au umetosheka basi na zile za
mwanzo?

Pondamali,
Historia Abdul Sykes inakuhangaisha wewe kama ilivyowahangaisha
wengi kabla yako.

Kwa mara ya kwanza nilipoandika habari zake katika gazeti la Africa
Events lililokuwa linachapwa London, toleo zima lilikusanywa likapigwa
moto.

Jiulize amri ya kuyakusanya magazeti yale ilitoka wapi na nini sababu
yake?

Huenda usiamini lakini ndivyo ilivyokuwa.
Kwa yale machache ambayo yaliwafikia watu habari ile ilikuwa gumzo
kubwa.

Watu wengi walivurugikiwa akili kama wewe hii leo akili yako
inavyovurugika.

Unajiuliza,''Hii kweli au ni uongo na porojo za Mohamed Said?''

Watu wengi hapa jamvini husema naandika porojo.
Wengi walikuwa hawajamsikia Abdul Sykes kuwa ndiye aliyeunda
TANU.

Sasa gazeti lile lilikuwa na makala,‘'In Praise of Ancestors’' Africa
Events,
 London, March/April 1988, (uk. 37-41) nilitaja mchango wa
Waislam na nikamtaja Abdul Sykes.

Kwa wengi historia hii ilikuwa ngeni kabisa.

Pondamali sasa nakurudisha kwa Dk. Kyaruzi na dhana kuwa yeye
ndiye aliyemwachia chama Nyerere.

Nakuambia kwa kinywa kipana kabisa.
Huo ni uongo.

Haya ninayoweka hapo chini nimetoa katika kitabu changu kuhusu:

''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold 
Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London 1998.
''In June, TAA headquarters announced its executive committee
with J.K. Nyerere, President; Abdulwahid Sykes, Vice-President;
J.P. Kasella Bantu, General Secretary; 
Alexander M. Tobias and
Waziri Dossa Aziz, Joint Minuting Secretary; John Rupia, Treasurer
and Ally K. Sykes as Assistant Treasurer. Committee members were
Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said, Denis Phombeah, Z.
James, Dome Okochi, C. Ongalo and Patrick Aoko.[1] The composition
of the TAA leadership showed East African solidarity that existed
during the struggle for independence. Kenyan patriots were elected
as office bearers side by side with Tanganyikans. It is said that it
was about that time, in the last months of 1953, that Abdulwahid
talked to Nyerere seriously about forming an open political party to
replace TAA.''




[1]Tanganyika Standard, 19 th June 1953.

Pondamali,

Nimekuwekea hapa juu uongozi wa TAA wa 1953 na gazeti ambalo
lilitaarifu habari hiyo.

Umeomuona 
Mzee Kasella Bantu katika mabadiliko hayo ya kihistoria?

Uongozi huu mpya ulitokea baada ya uchaguzi wa tarehe 17 Aprili
katika Ukumbi wa Arnautoglo ambako Nyerere alichaguliwa kuwa rais
wa TAA na Abdul Sykes makamu wake.

Katika hali kama hii vipi Dr. Kyaruzi iwe kamuachia chama Nyerere?

Achilia 
mbali kuwa yeye alipata uhamisho kwenda Kingolwira na kisha
Nzega mwaka 1951.

Mimi nawapeni sana pole kwa kuwa kwa kweli mnaziviza akili zenu
pasi na sababu ya maana.

Hakuna mwanahistoria ambae ataweza kuandika historia ya 
TANU
au ya Nyerere bila ya kwenda kwenye Nyaraka za Sykes.

Hii ni hazina ya kipekee kabisa.
Ukiwa hujaridhika rejea tena na maswali mengine.

Insha Allah utanikuta mie bado nabariz hapa jamvini nakusubiri.

Tuagane kwa swali hili langu moja.

Pondamali,

Mzee Kasella Bantu hakupata kukuhadithia ile ''drama,'' siku ile
ya uchaguzi kati ya mwalimu wa shule Nyerere ambae hakuna
aliyekuwa anamfahamu na Abdul Sykes kijana maarufu wa mjini?

Mimi ''movie'' nzima ninayo kanihadithia Dossa Aziz nyumbani kwake
Mlandizi.

Mzee Kasella Bantu hakupata kukuhadithia kwa nini yeye na
Nyerere walikuwa maadui wakubwa kufikia Kasella Bantu kutoroka
nchi kwenda Ujerumani hali kapitishwa uwanja wa ndege kavaa
mavazi ya kipadri?



Joseph Kasella Bantu 

Last edited by Mohamed Said; Today at 12:15.

No comments: