Sunday, 8 June 2014

KUTOKA JF: HISTORIA YA TANU MCHANGIAJI ADAI NYERERE ALIKUWA NA ''KITU ADIMU''

234
Default Re: Tanganyika(TANU) imetoka mbali waasisi wake wengi wao wametangulia mbele ya haki

Kituko,
Ingawa umetaka mnakasha khasa katika nukta yako tumalizie hapa
mimi binafsi naomba nieleze machache na naamni ni katika kujenga.

Labda ungetaja hvyo ''vitu adimu'' vya Nyerere tungeweza kufanya
uchambuzi wa pamoja.

Mimi naamini unakusudia Masters Degree yake na ikiwa nimekosea
basi bila shaka utanifahamisha.

Katika TAA pale New Street 1950s mwanzoni kulikuwa na vichwa
vitatu vikali.

Kulikuwa na Abdul Sykes ''A'' student toka darasa la kwanza na
alikuwa anaingia Makerere 1942 Waingereza wakamtia katika jeshi
la KAR na safari ya Kampala ikafa akaelekea Lower Kabete, Kenya
kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi.

Hivi juzi juzi tu ndiyo tumekuja pata taarifa kuwa alikuwa aingie
Princeton University, Marekani 1953 na huko nako hakwenda.

Huyu wa kwanza.

Alikuwapo Hamza Kibwana Mwapachu yeye alianza na Medicine
wakati uleni kozi ya Medical Officer.

Hii ni sayansi.

Alipomaliza akenda Makerere na alipotoka Makerere ndiyo akenda
University of Wales, Cardiff.

Mtu wa tatu ni Nyerere na sifa zake sote tunazijua.

Kulikuwa na madaktari watano katika TAA - Dk. Luciano Tsere,
Dk. Michael Lugazia, Dk. Joseph Mutahangarwa, Dk. Vedasto
Kyaruzi
, na Dk. WBK Mwanjisi.

Huyu Dk. Mwanjisi yeye alitaka kuacha uganga aende Uingereza
kusoma social science.

Kuna kisa cha kusisimua sana kati yake na Nyerere kuhusu yeye
kuondoka kwenda Uingereza.

Hakwenda Uingereza baada ya kutokea msuguano kati yake na
Nyerere.

Kulikuwa na Chief Abdallah Said Fundikira mhitimu wa Oxford
University na kulikuwa na Chief Kidaha Makwaia wote wahitimu
wa vyuo vya Uingereza.


Chief Abdallah Said Fundikira

Hao wote niliokutajia hapo walikuwa hawapungui nyumbani kwa
Abdul Sykes kwani pale ndipo ilipokuwa barza yao ya siasa.

Msome Judith Listowel katika kitabu cheke ''The Making of
Tangayika,'' ana sura nzima kaipa jina ''Makerere Intellectuals.''

Katika sura hiyo anawaeleza hawa wasomi wa nyakati zile waliotoka
Makerere.

Tuje kwa Nyerere.

Kitu kimoja ambacho yeye mwenyewe hakupatapo kusema na wengi
kwa hiyo hawakijui na ndiyo sasa inaleta shida ya kuelewa ukweli ni
kuwa yeye Nyerere alipoachiwa TAA na Abdul Sykes mwaka 1953
chama kilikufa.

Nadhani mpaka hapa kwa wale ambao bado hawakuwa wanajua TAA
ilikuwa na watu wa uwezo upi angalau wamepata picha.

Sasa ukitaka kujua vipi Nyerere aliweza kufanya hayo yote katika
TANU hadi uhuru ukapatikana ndiyo hapo inabidi tuachane na historia
ya sampuli ya Kivukoni ya ''vitu adimu,'' tuingie kwenye ulkweli wa
mambo.

Tuwatafute wafadhili wa harakati, askari wa miguu, watu wa zile
propaganda.

Hapa ndipo utakutana na Abdul Sykes na ile timu yake ya akina
Dossa
 ''The Bank,'' Aziz na Rupia kwa Dar es Salaam.

Kanda ya Ziwa akina BomaniSuedi Kagasheki, Aikaeli Mbowe
huko Moshi kuwataja wachache tu.

Watu wa propaganda - akina Sisso, Bakis, Nujum Azhar, Saniyyat
Hubbi, vyama vya akina mama vya lelemama, mama yangu Hawa
bint Maftah 
kwa Dar es Salaam na mama yetu Bi. Dharura bint
Abdularhaman 
kule Tabora na Bi. Shariffa bint Mzee Lindi nk.
nk.

Akina Rashid Heri Baghdeleh, Robert Makange, Ramadhani
Mashado Plantan, 
hawa watu wa magazeti.

Kulikuwa hadi na watu wa ''seth habar.''
Akina Mwalimu Bakari na Sheikh Issa Nassir wa Bagamoyo.

Vituko,
Naitafuta ile picha ya Nyerere kabeba bango lina maneno:
''Independence 1961,'' Insha Allah nikiitia mkononi nitaileta jamvini.

Nyerere kabebwawa juu.
Tazama angalia kakalia mabega ya akina nani.

''Tazama angalia kwa chini kuna mtu nyie mnawaita kwa dharau
wavaa, ''barghashia.''

Huyu bwana mkubwa kavaa koti la ras na kanzu ya darzi.

Unamjua yule nani?
Na kwa nini kawekwa pale karibu ya Nyerere kwa siku ile adhim?

Historia ya Illife, Kimambo, Kivukoni hawajui na hawatajua
historia hii hata siku moja.

Nyerere kwa hiyo ''kitu adimu,'' asingefika hata Ilala Quarter.

Inatosha.
Last edited by Mohamed Said; Today at 18:19.

No comments: