SoNotorious,
Umenita ''ka.''
Nakuwekea hii picha ya ujana wangu uniangalie kama ''ka'' inanienea.
Mimi ni huyo mkono wa kulia.
Nilipokuwa mtoto ''ambition'' yangu ilikuwa nicheze mpira Sunderland (sasa
Simba) kisha nicheze team ya taifa.
Haikuwa.
Niliishia mchangani.
Kidongo Chekundu, Mnazi Mmoja, Jangwani, Uwanja wa Polisi Oyster Bay
na kwengineko.
Wenzangu wengi walikwenda mbele wengine Cosmo, Yanga na Sunderland
hadi timu ya taifa mie nikabaki kuwa ''bookworm,'' na wakinitania kwa hilo la
kupenda ''kusomasoma.''
Wamanyema Allah katupendelea katupa miili mikubwa kiasi Mmanyema tusi lake
kubwa ukimuudhi na wewe si Mmanyema atakuita, ''Kinyangarakata,'' yaani
''Kijitu.''
Mimi si ''ki'' wala si ''ka.''
Kuwa na adab kidogo tu.
Naamini umejielewa.
Una ubavu wa kuweka picha yako?
Hii picha hapo chini nilipokuwa na mwaka mmoja.
Picha hii ilipigwa studio ya
Mzee Shebe Mtaa wa Livingstone na Kipata, 1952/53.
Huyu
Mzee Shebe akajakuwa mpiga picha wa TANU na
Nyerere katika miaka hiyo
ya kupigania uhuru.
SoNotorious,
Hapo chini ndivyo nilivyo hivi sasa.
Picha hii nimepiga New York, Harlem 125th Street.
Hii ndiyo ilikuwa mitaa ya
Malcolm X wakati wa enzi zake katika 1960s.
JF ni mahali pa kubadilishana fikra si mahali pa matusi na ushenzi.
Hapa ni mahali watu mnashindana kwa hoja katika njia za kiustaarabu.
Hapa si mahali pa kuonyeshana nani hodari wa kejeli na mengine yasiyo
na maana.
Naamini wewe na wengine mfano wa wewe mtabadilka na tutakuwa
katika mijadala kwa ustaarabu, adabu na heshima.
No comments:
Post a Comment