In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu wanahabari,
Jumuiya ya Wataaluma Waislamu Tanzania (Tanzania Muslim Professionals
Association) huwa tunatumia fursa kama hii ya kuukaribisha Mwezi wa Mtukufu wa
Ramadhani kuwakutanisha wanataaluma wa fani na kada mbali mbali kutoka hapa
nchini na nje ya nchi ili kuzungumza na kujadili masuala mbalimbali ya kijamii na
kidini ya hapa nchini kwetu na pia kimataifa.
Akiongea na wahandishi wa Habari Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Ndugu Mussa
Mziya Alisema, “Kongomano la Kukaribisha Ramadhani hufanyika kila mwaka
katika Jumapili ya mwisho ya mwezi wa Shaaban na kwa kipindi cha miaka sita
mfululizo na limefanikiwa kujadili na kupata majawabu ya masuala mbali mbali ya
kijamii na kidini. Tumekuwa na kauli-mbiu mbalimbali kila mwaka kutokana na
jambo mahsusi tunalotaka kulijadili kwa jamii – kwa mfano tumekuwa na kauli-mbiu
kama “Kufuta Umasikini kupitia Zakah na Sadaqah”, “Nafasi ya Elimu katika Kuleta
Maendeleo ya Jamii”, “Athari za Vyombo vya Habari Katika Jamii” na “Mifumo ya
Benki za Kiislam”, “Wanawake, Ngozo Kuu ya Maendeleo ya Jamii”.
Ndugu Mziya Aliongeza Kuwa “Vijana Wetu, Hazina Yetu” au kwa Kiingereza
“Our Youth, Our Future” ndio kauli mbiu ya WELCOMING RAMADHAN
CONFERENCE ya Mwaka huu 2014 (1435H). Vijana hawa wanaokua hivi leo bila
shaka wao ndio umma wa kesho.
Katika kongamano la mwaka huu tumekusudia kuzungumzia VIJANA na
changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku
hususan maisha yao ya kidini na kiuchumi; Na kwa maana hiyo basi, tumechagua
anuani ya Kongamano la mwaka huu kuwa “Vijana Wetu, Hazina Yetu”. Ni lengo
la Kongamano la mwaka huu kuhamasisha Umoja na Mshikamano miongoni mwa
Wanataaluma wa Kiislamu na Waislamu wote kwa ujumla hususan Vijana na
kuona kuwa Vijana kama kundi kubwa na muhimu katika jamii yetu kuwa wanapata
malezi, nafasi na elimu sahihi ya mazingira na ya kidini ili kumudu kuendesha
harakati za kiuchumi na kidini kwa maana ya kuiweka jamii katika mustakbali wa
maisha kama ilivyoamrishwa na dini yao.
In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful
Mziya Alisema “Kwa kutambua kuwa hali ya Vijana kwa sasa imekuwa na
changamoto nyingi katika nyanja mbali mbali zikiwemo za uchumi, kijamii na
kiteknolojia imepelekea kuona umuhimu wa Waislam hasa wanataaluma kama
sehemu ya jamii kukaa, kujadili ili kuona namna ya kuwasaidia vijana hasa kwenye
njanja za uchumi kama vile ajira, ujasiriamali na uwekezaji, pia nyanja za Kijamii
hasa Kiimani ili kupata raia wema na waadilifu”.
Kipindi cha ujana ni muhimu sana kwa sababu ndicho upeo wa mustakbali wa
umma na mustakbali wa kutokana na sababu hii ndio mafundisho bayana ya dini
yetu yanatilia mkazo sana kukizingatia kipindi hiki kutokana na umuhimu wake,
kama hadith ya Mtume Muhammad SAW aliposema: "Hakika nyayo za mja
hazitaweza kunyanyuka katika siku ya Kiyama hadi aulizwe ameumaliza umri wake
katika njia gani na ameutumia ujana wake katika nini."
Mussa Mziya alisema kuwa “Kongamano hili la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani pia linakusudia kuiomba Serikali kuweka mikakati mahsusi ya
kuwasaidia vijana kiuchumi kwa kuwa na sera zitakazowezesha kuongeza ajira
kwa vijana na fursa mbalimbali za ujasiriamali. Taifa linaelekea kufika mahali
ambapo baadhi ya watu wanaotuongoza wamekuwa wanajali maslahi binafsi au
watu wa kikundi fulani, wasio na Imani na maadili mema ambayo yanaathiri mfumo
mzima wa maendeleo ya Jamii, Kisiasa na Kiuchumi. Inawezekana kabisa
mporomoko unaotokea sasa wa maadili ni athari za jamii ikiwemo ya Kiislam yenye
muongozo bora kama mfumo wa maisha ya binaadamu kutomuhusisha vyema
kijana katika sera na mipango ya kimaendeleo au kusahau majukumu makuu ya
malezi kwa vijana katika kujenga Jamii Imara na yenye taaluma na Maadili mema
kama dini yetu ya Kiislam inavyotufundisha. Mziya alisisitiza kuwa “Wazazi wa leo
tumekuwa tukijishughulisha sana kutafuta Mali kwa ajiri ya Maendeleo ya Vitu
(Materials) na kusahau familia zetu hasa vijana na tunapostuka tunakuta vijana
tayari ameshaharibika katika Umalaya, Madawa ya Kulevya, Ufisadi, na mambo
mbali mbali ya Hatari”.
Pia Bwana Mziya Alisema, “Kongamano hili la Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani pia linategemea kuiomba Serikali, Vyombo vya Habari Pamoja na
wanaharakati mbali mbali kujishughurisha zaidi na shida za vijana wa leo hasa
kimaadili na kuhakikisha hazina hii ya vijana kweli inakuwa hazina ya Taifa hili sasa
hivi na huko mbele. Kufutwa kwa mifumo inayoonekana kuwabagua vijana wetu
kwa imani zao hasa katika masuala ya ibada mashuleni, Vyombo vya habari
kuacha kurusha habari ambazo zinaendelea kuporomosha maadili kama vile
Kuonyesha vijana wa Kiume wamevaa kama wanawake katika Television,
wanaharakati kushabikia mambo ambayo yanawafanya vijana wahamaki na kuwa
wenye kulalamika kila siku badala ya kuwafanya waone fursa zinazowanzunguka
au kutetea mavazi ya baadhi ya vijana ambayo yanaonyesha wazi kuwa
yanahamasisha masuala ya ngono”
Pia Mwenyekiti huyo wa wanataaluma Waislam, Mussa Mziya alisisitiza kuwa,
Kongamano hili linategemea kuwa kama ukumbusho kwa Wataaluma na
wanazuoni wote wa kiislamu juu ya kuendelea kumuhimalisha Kijana Kimalezi ya In The Name of Allah, the Magnificent, the Merciful
Kimaadili na Kumuendeleza ili kujenga jamii bora ya Kiislamu inayofuata maadili
bora na sahihi ambayo italeta athari kwa maendeleo ya Taifa pia litakuwa ni
chachu kuwakumbusha kutosahau kutekeleza majukumu yao ya Kiimani katika
kipindi chao chote cha maisha na kushirikiana na wanazuoni wetu ambao muda
mwingi wanakuwa katika wakati mgumu kuendeleza jamii kiroho.
Napenda kuwashukuru wanahabari wote kwa kuhudhuria katika Kongamano la
Kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani leo tarehe 22.06.2014 na pia
kushukuru uhusiano ambao umekuwa ukikuwa kila mwaka kwa kuielewa jamii ya
Kiislam kwa Ujumla kwa mambo mema na kuendelea kuelezea picha nzuri juu ya
Uislam na Waislam ili kudumisha mshikamano na Umoja wa Taifa.
In ShaaAllah Mwenyezi awafanyie wepesi katika kusukuma Mbele Nchi yetu
Tanzania.
Ahsanteni kwa kunisikiliza, Mwenyezi Mungu atujaalie kufika Mwezi Mtukufu wa
Ramadhan, Amiin na karibuni nyote katika Kongamano la Kukaribisha Mwezi
Mtukufu wa Ramadhani.
Mussa Mziya
Mwenyekiti
Umoja wa Wanataaluma wa Kiislamu Tanzania –
Tanzania Muslim Professionals Association (TAMPRO)
+255 754 261 600
Ukumbini: Julius Nyerere International Conference Centre |
Khalid Mtwangi Akizungumza na Dk. Badamana wa Chuo Kikuu Cha Nairobi |
Dk. Salha Akizungumza Kuhusu Ulezi wa Yatima |
Mwenyekiti wa TAMPRO Mussa Mzia na Dr. Badamana |
Dr. Badamana Akihojiwa na Vyombo vya Habari |
Ukumbini |
Mohamed Kamilagwa |
Ali Masoud aka Kipanya Akitoa Mada Kuhusu Vijana |
Dr. Badamana na Sheikh (Eng) Ali Kilima |
Washiriki Wanajitayarisha kwa Sala ya Dhuhr |
No comments:
Post a Comment