Sunday, 3 August 2014

KITABU MAARUFU ''KWAHERI UKOLONI KWAHERI UHURU'' KINACHOELEZA HISTORIA YA KWELI YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR KIMEWASILI NCHINI


Mohamed Omar Mkwawa mmoja wa wanamapinduzi wa Zanzibar
aliyekuwa na kazi ya kuvusha wakata mkonge kutoka mashamba ya
mkonge ya Kipumbwi  na Sakura kuingia Zanzibar kuiangusha serikali ya
 Mohamed Shamte  akiwa amekishikilia kitabu, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri
Uhuru.''

Tundu Lissu aliposimama katika Bunge la Katiba na bila ya kutafuna maneno akataka serikali ieleze kifo cha Abdallah Kassim Hanga na wanamapinduzi wengine, ukumbi mzima ulizizima. 

Ukumbi ulizizima si kwa kuwa haikuwa ikijulikana kuwa Kassim Hanga aliuawa. la hasha.

Ukumbi ulilizizima kwa kuwa siku zote watu wakimuona mfalme akitembea uchi lakini hakuna aliyekuwa na ujasiri wa kumueleza mfalme kuwa yuko uchi na arejee nyumbani kwake akavae. 

Tundu Lissu alikuwa kayasema hayo ya kuuwawa kwa Hanga huku amekishika kitabu cha Dr. Harith Ghassany, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru, '' kama ushahidi wa yale aliyolkuwa akiyaeleza pale Bungeni. 

Baada ya Tundu Lissu kusema hayo wengi waliingiwa na hamu na shauku ya kutaka kujua khasa nini kilitokea katika historia ile hadi Hanga na wenzake wakakamatwa na kuuliwa. 

Kwa bahati mbaya kitabu hakikuwa madukani.

''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' sasa kinapatikana duka la vitabu Ibn Hazim Media Centre, Msikiti wa Mtoro, Kariakoo.

Ndugu msomaji kipate kitabu hicho usome historia ya kweli ya Mapinduzi ya Zanzibar.




Siku Nyerere Alipomuadhiri Hanga Viwanja Vya Mnazi Mmoja
Mbele ya Kibarua Bar Nyuma ya  Ukumbi  wa Arnatouglo
Hanga Alitolewa Jela Ukonga Kuletwa Pale Makhsusi kwa Shughuli Hiyo
Baada ya Siku Hii Hanga Hakuoenekana Tena

No comments: