Quote By Ritz View Post
Sheikh Mohamed Said

Niwe radhi kiduchu kwa swali langu kwako.

Ni bayana gani iliyokusisimua kwenye kitabu cha "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri uhuru".

Pamoja kuwa kuna mkono wako ndani ya kitabu hicho.
Ritz,
Kwanza ningependa nikusahihishe kidogo.

Katika kitabu hiki hakuna mkono wangu.
Watu wengi wanadhani kuwa kitabu kina mkono wangu.

Mimi nilikuwa msaidizi wa Dr. Ghassany kwa kummwendesha na kumpeleka
huku na huko.

Labda na kupiga picha ''stills,'' na ''video,'' na kufanya ''narration,'' katika
video.

Mimi siwezi kuwa na sauti mbele ya msomi huyu wa Chuo Kikuu Cha Michigan
na Harvard.

Katika moja ya vitu ambavyo kwa kweli vilinishtua katika kitabu hiki ni suala la
Nyerere na Uislam katika Zanzibar.

Hapa ningependa kusema kuwa yapo mengi yaliyonistua kwa kweli kabisa lakini
hili lilinitisha sana.

Nakuwekea hapa chini kipande hicho nilichosoma ambacho kilinifungua macho
na kunisaidia kuyaelewa Mapinduzi ya Zanzibar.

Hebu soma hapo chini:

''Pia alisema Kambona, kuwa, wacha mambo ya kupinduwa, tangu ilipokuwa
mambo ya uchaguzi, anasema ilikuwepo kamati maalumu ya kupeleka watu
Zanzibar, toka wakti wa uchaguzi mpaka katika masala ya mapinduzi.
Kanielezea kuwa walipeleka watu wengi kutoka bara, kutoka Tanganyika.
Aliniambia watu wametoka kwetu. Alitumia neno hilo. Alisema madam Zanzibar
Serikali atakuwa yuko Mfalme ndani yake wanaona kwao wao hautokuwa
mlingano mzuri baina ya jirani kwa jirani. Mimi nikamwambia kwamba, hilo tu
au kuna suala la dini limo ndani yake?

Hiyo khabari ya ufalme tu au na dini ilikuwa ndani yake Nyerere anayo?
Akanambia Kambona kuwa Nyerere alisema tujaribu kama tutakavoweza
kupunguza nguvu za Uislamu katika Zanzibar. Na ikiwa hatutokuwa na
serikali Zanzibar hatutomudu kulifanya hilo. Yeye akanijibu, na dini ipo
ndani yake. Hilo ndo jibu lake yeye. 
Hilo pia kanizungumzia. Katika hizo plan zao.''

Anaeeleza habari hizi ni Aman Thani Fairoz aliyekuwa secretary general wa
Zanzibar Nationalist Party (ZNP)

(''Kwaheri Ukoloni...'' Mlango wa Kumi na Saba uk. 278 toleo la kwanza 2010).

Nillibahatika kukutana na Mzee Aman Thani nyumbani kwake Rashidiyya, Dubai
mwaka 1999 na tulizungumza mengi.

Amam Thani ni mwandishi wa kitabu ''Ukweli ni Huu,'' kinachozungumzia historia
ya Zanzibar na mapinduzi.

Sasa ile dhana ya kuwa si kama mapinduzi yalisababishwa na hizo sababu
mashuhuri zinazoelezwa kila siku bali kuwa nia ilikuwa ni kuupiga vita Uislam
na kwa hakika Nyerere alifanikiwa Zanzibar kwa kiasi.

Tunaweza tukaenda mbali zaidi kutaka kujua kuhusu hii njama lakini kwa sasa
na tumalizie hapa.

Si ajabu kwa William Lukuvi kusema serikali tatu Zanzibar itaimarisha Uislam.
Ni muendelezo ule ule wa mwaka 1964.