Wewe tapeli chakubimbi mwanakijiji umtishe nani banah??
Vitabu vyako vya ngano za mapenz hadi leo vinadoda pale mliman city sembuse historia uiwezee wapi wewe??
Wewe utabakia kutapeli tuh humu jf na huko facebook na kwenye magazeti uchwara tuh.
Mohamed said siyo size yako hata chembe.
We fani yako si kuhubir mihadhara ya injili na kuongopea watu ushibe kwa pesa za sadaka za wanakondoo??
Unadhan hatulijui profile lako??
Teh teh teh.
Kuna malofa humu ndan unaowaongopea ongopea basi wanakuona wa maaana kumbe njaa kali tu mkimbizi wa nchi.
Teh teh teh.
cathedral bookshop unayoisemea yenyewe wamejikita zaidi kwenye uuzaji wa vitabu ya dini kupitia waandishi mbalimbali na zaidi ni vitabu vya kikatoliki...
Sasa ikiwa lengo la kitabu chako nikueleza historia ya kweli ya uhuru wetu kwanini kitabu kiuzwe MANYEMA na MTORO tu??? uhisi kuwanyima haki ya kuujua ukweli ndugu zangu wa Musoma, Njombe, Bunda n.k???
au unataka watu nchi nzima waende hapo MANYEMA na MTORO??
Sasa ikiwa lengo la kitabu chako nikueleza historia ya kweli ya uhuru wetu kwanini kitabu kiuzwe MANYEMA na MTORO tu??? uhisi kuwanyima haki ya kuujua ukweli ndugu zangu wa Musoma, Njombe, Bunda n.k???
au unataka watu nchi nzima waende hapo MANYEMA na MTORO??
Remote,
Huwezi kumpa mwenye duka kitu auze kama hataki.
Maduka yaliyotaka kuuza kitabu hiki wamekiuza.
Labda nikufahamishe kuhusu aina ya vitabu ambavyo mimi nimenunua Cathedral
Bookshop - ''Religion and Development in Tanzania,'' cha Van Bergen na kitabu
maarufu cha Sivalon.
''Catalogue'' ya vitabu hivi havina tofauti na kitabu changu.
KASE Bookshop Arusha wameuza kitabu changu nakala nyingi sana.
TPH wameuza vilevile kitabu changu.
Book Cafe wameuza kitabu changu.
Ikiwa wauza vitabu wa Bunda na Tandahimba watakitaka bila shaka
watakipata kama walivyopata wauzaji wengine.
Vuta subra tuone.
Kitabu ndiyo kwanza kimewasili na maduka ya vitabu wanataarifa bila
shaka wataviuza.
Re: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini
Chuma.
Ungefanya jambo la maana sana kama ungekuja na historia yako ya ukweli uliyoandika wanaukumbi tupate kuisoma mkuu.
Re: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini
Mohamed Said mwenyewe ni "Mcongo", tena wa kujisifia.
Mohamed Said, naku-challenge ukanushe hili!
Hakika mimi ni Mmanyema na asili ya babu yangu mkuu ni Congo.
Pale Kipata nilipozaliwa mimi pana historia ya kipekee.
Mtaa wa Kipata na Congo kulikuwa na nyumba ya Ibrahim Hamisi. Huyu alikuwa Mnubi kutoka Dafur ndiko ilipokuwa asili ya baba yake.Ibrahim Hamisi alikuwa muasisi wa African Association.
Mtaa wa Kipata na Swahili na mbele Mtaa wa Sikukuu alikuwapo Hassan Machakaomo, huyu alikuwa Mzulu baba yake alikuwa na Von Wissman.
Mtaa wa Kipata na Livingstone na mbele yake New Street alikuwapo Salum Abdallah. Huyu ndiye babu yangu na yeye baba yake alikuwa Mmanyema kutoka Congo.
Hapo hapo alikuwapo Kleist Sykes huyu Mzulu na baba yake alitoka Mozambique, alikuja na Wissman.
Vitukuu vya Kleist, Machakaomo, Salum Abdallah, Ibrahim Hamisi wapo nchini hadi sasa na hawa ni vizazi vya tano.
Sawaka,
Huwezi kumpa mwenye duka kitu auze kama hataki.
Maduka yaliyotaka kuuza kitabu hiki wamekiuza.
KASE Bookshop Arusha wameuza kitabu changu nakala nyingi sana.
TPH, Da es Salaam wameuza vilevile kitabu changu.
Book Cafe, Dar es Salaam wameuza kitabu changu.
Kitabu hiki kinapendwa sana na kinanunuliwa sana.
Kitabu ndiyo kwanza kimewasili na maduka ya vitabu wanataarifa bila
shaka wataviuza katika maduka yao.
Lakini cha kuzingatia kwako ni kuwa hiki kitabu hakiuzwi msikitini.
Ibn Hazm Media Centre maduka yake mawili moja liko Mtaa wa Mahiwa karibu na Msikiti wa Mtoro na lingine lipo Mtaa wa Mafia karibu na Msikiti wa Manyema.
Unapotaka kumuelekeza mtu maduka haya yalipo kwa wepesi afike unamwambia nenda Msikiti wa Manyema au Mtoro.
Lakini ikiwa mtu kwa kupenda kuifurahisha nafsi yake akasema kuwa hayo maduka ya vitabu yako ndani ya msikiti ni vigumu kwangu kumzuia.
Mtu ana haki ya kuamini apendacho.
Hii ni nchi huru.
Angalia picha hii nimepiga jana tarehe 27 August 3014 katika duka la Ibn Hazm Media Centre.
Je hapo ni msikitini?
Yesterday 23:09#209Join Date : 16th August 2013Posts : 150Rep Power : 384- Likes Received
- 29
- Likes Given
- 2
Re: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini
Tukiendelea kuwachekea hawa wahuni kama kina Mohamed Said
taifa litasambaratika hili,kule kenya hupigwa risasi mapema.
Aliyeandika haya anaitwa ''Ududu.''
No comments:
Post a Comment