Wednesday, 27 August 2014

KITABU CHA MAISHA YA ABDULWAHID SYKES NAKALA YA KIINGEREZA NA KISWAHILI KINAUZWA IBN HAZM MEDIA CENTRE MSIKITI WA MTORO NA MSIKITI WA MANYEMA

Mwandishi akimkabidhi Sheikh Ali Hassan Mwinyi kitabu cha Abdul Sykes

Mwandishi Akiwa Ndani ya Duka la Vitabu la Ibn Hazm Media Centre
Kitabu hiki, ''The Life and Times of Abdulwahis Sykes (1924 - 1968) the Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika,''  kilichochapwa kwa Kiingereza London mwaka 1998 kisha kikafanyiwa tafasiri ya Kiswahili na kuchpapwa Nairobi mwaka 2002 si kitabu kigeni kwa kusikika na wengi. Maudhui ya kitabu hiki yalishtua wengi kitabu kilipotoka na kwa muda mrefu kimesababisha mjadala mkali katika Jamii Forums. Kwa kipindi kirefu kitabu hiki hakikuwa kinapatikana na ikawa mara kwa mara wasomaji wanakiuliza vipi watakipata.

Kitabu sasa kinapatikana katika maduka ya vitabu ya Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema.




No comments: