Re: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini
masopakyindi
Wanaukumbi,
Inaelekea mnakasha ushatoka katika reli na sasa ni matusi, kejeli na lugha
zisizopendeza.
Wakati mwingine ghadhabu zimepanda kwa wachangiaji wengine kuzungumza
''kunipiga kiberiti.''
Hapa yameingizwa mambo ya ugaidi nk.
Kwa kweli kilicho jamvini ni kitabu cha Abdul Sykes na nini kitabu hiki kinasema.
Nina jambo moja tu ningependa kuufahaisha ukumbi.
Kitabu hiki kilipochapwa Uingereza kwa Kiingereza mwaka 1998, publishers
Minerva Press walikitangaza kwenye vyuo vyote vinavyosomesha African History.
Baada ya kutangazwa huku ndiko wasomi wa Historia ya Afrika wakakisoma
na wengine wakakifanyia ''review.''
Kitabu kikafanyiwa review na John Iliffe na ''review'' ikachapwa katika Cambridge
Journal of Africa History.
Kitabu kikafanyiwa ''review'' na Jonathon Glassman wa Northwestern University.
Kitabu kikafanyiwa ''review'' na James Brenan wakati huo anasomesha SOAS.
Hawa ni mabingwa katika historia ya Afrika na hasa Tanzania.
Hata mmoja katika hawa hakuna aliyesema kitabu kinatukana Ukristo, cha kigaidi
au kinamdhihaki Nyerere.
Mwaka 2011 nilialikwa Marekani na nimezungumza kuhusu kitabu hiki mbele ya
Brenan na tukapingana kama ilivyo kawaida yetu mimi na yeye.
Mnakasha ule ulinoga sana na niliposhuka jukwaani Jonathon Glassma akaniomba
niende chuoni kwake Northwestern University tufanye mnakasha mwingine.
Nadhani ndugu zangu sasa mnayo picha ya kitabu hiki.
Kitabu hiki kimepata hadhi kwa kuwa kimekuja na habari mpya ambayo kabla
haikuwa ikifahamika.
Hiki ndicho kitu kilichokipa hadhi kitabu changu.
Niliporudi Marekani nikaalikwa Ujerumani kwa masuala haya haya kwenye
taasisi ijulikanayo kama Zentrum Moderner Orient (ZMO) iliyoko Berlin.
Hii ni taasisi ya utafiti katika historia kama hizi za kwetu.
Kwa kumaliza ningependa kuufahamisha ukumbi kuwa kitabu hiki kimenipekeka
kwingi na kimenipa kazi nyingi kufanya pamoja na watafiti wengi kutoka nje.
Hapa nyumbani hakuna mwanahistoria hata mmoja aliyekifanyia kitabu changu
''review.''
| James Brenan |
Mtazamo,
Unajitisha bure.
Hakuna yoyote anaechochochea vurugu za kidini wala hakuna wa kusimama
mahakamani kwa kuandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika.
Kitabu cha Abdul Sykes sasa ni mwaka wa 16 toka kilipochapwa na hivi sasa
tunakwenda toleo la nne na haijatokea hata mtu mmoja kuchanjwa na wembe
kwa ajili ya kitabu hiki.
Kitabu kinaingia kutoka nje kinapita ngazi zote za uchunguzi na forodha na
kinauzwa kote nchini watu wanakisoma.
Mtazamo,
Usijitishe wewe wala kuwatisha watu wengine ati kutakuwa na ''umwagaji
wa damu,'' kisa watu wanajadili mustkbali wa nchi yao.
kama nilivosema awali kuwa siwezi kupoteza muda wangu kusoma kitabu chako pamoja na kwamba unanishawishi nikisome, najiuliza kwanini nipoteze muda wangu kusoma kitu ambacho katu hakiwezi kuishawishi akili yangu ila naamini kama nisingekuwa najua hoja zako kupitia humu jf labda ningeweza kukinunua na kukisoma! Licha ya kuwa waingereza wanasema " do not judge a book by it's cover" lakini mimi nasema you can judge it through the attitude of it's author! Kuhusu kitendawili chako cha "boya" sijui ulitaka nikueleweje zaidi ya dhana ya ugaidi na roho ya kinyama!
Mpingauonevu,
Niliandika kitabu cha Abdu Sykes baada ya kuona kuwa historia
iliyoandikwa kuhusu TANU na harakati za uhuru ilikuwa na upungufu
mkubwa kwa kuwa mchango wa Waislam ulifutwa kwa makusudi.
Kitabu cha Abdul Sykes kimebadili hali hii.
Hili nimelieleza katika kitabu kwa kirefu na kuonyesha ushahidi.
Wewe si mtu wa kwanza kuhangaishwa na historia hii niliyoandika.
Fr. Smith amepata kuhoji na nikampatia jibu sawia. (Angalia See
Fr. Peter Smith, ‘Christian and Islam in Tanzania Development
and Relationships’ in Islamochristiana, 16 (1990) pp. 171-182.
Also Smith, ‘Some Elements for Understanding Muslim-Christian
Relations in Tanzania’. 1993 (seminar paper presented in Dakar,
Senegal, ‘Islam in Africa South of Sahara.’
Rejea hii yake na nyingi nyingine utaziona katika kitabu changu.
Huyu Fr. Pater Smith alinitafuta hadi akaonana na mimi uso kwa
macho na aliniuliza mengi na mimi nilijitahidi kwa kadr ya uwezo
wangu kumueleza yale yote niliyokuwa nayajua.
Fr. Peter Smith alikuwa akifanya kazi pale St. Joseph na ofisi yake
ilikuwa Atuman House.
Nimeshindwa kukujibu kila kitu kwa kuwa umechanganya mambo
mengi lakini nadhani haya niliyokuandikia yanatosheleza.
Join Date : 29th April 2011
Location : VIRGINIA
Posts : 2,864
Rep Power :
1368133
- Likes Received
- 836
- Likes Given
- 2286
Re: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini
Shame on you Moderators of this forum. Kama kweli hamna agenda za siri kwa nini mmefuta posts zangu ambazo nili nukuu posts zilizo anza kumtukana Mohamed Said kabla hata ya Mimi MZIMU, Ritz, kahtaan na Boko Haram hatuja kuja kujibu Mashambulizi. Matusi ambayo hayana uhusiano kabisa na Maudhui ya thread. Nili nukuu posts kadhaa na nikaziweka rangi nyekundu. Hizo posts kwa nini zimeondolewa na kubakisha zinazo leta dharau kwa Mohamed Said.
Sasa huo tuite ujanja au Ujinga?. Kama mnauona ukweli, kwanini sasa mnakataa kuufuata. Kinyume chake mungewacha kila mtu aone.
Nafsi zenu zina wasuta. Na sikatika hili tu, bali ni mambo mengi sana. Sasa kwanini mnakua watumwa wa Mawazo. Kama akili zenu ni huru, follow the truth.
Acheni hizo nyinyi jikomboeni kifikra.
No comments:
Post a Comment