Thursday, 4 September 2014

KUTOKA JF: KITABU CHA ABDULWAHID SYKES

e: Kitabu cha Historia ya harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika kimewasili nchini

Quote By bona View Post

the problem woth this guy is making this to look as if ni issue ya waislam, si ni kitabu tu au? kwenda kukipeleka misikitin ni kuonyesha nn? weka maeneo mengi tukisome alafu uje tukupe challenge! eti untold story kweli kuna untold story???

Bona,
Nimeweka historia ya kitabu hiki na usambazaji wake kwa ufupi katika post
yangu kabla ya hii.

Naamini umeiona, umeisoma na umeelewa.

Kitabu hiki hakika kinauzika sana Kariakoo labda kwa sababu ni kwetu
na wajukuu wa wengi waliokuwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika
ni wakazi wa Kariakoo na bado wanaishi hapo.

Lakini juu ya kuuzika Kariakoo kitabu hiki kimeuzika sana katika maduka
ya WH Smith ambayo yapo katika miji mingi Uingereza - London, Leeds,
Liverpool, Cardiff, Glasgow nk.

Kila chuo nilichopita Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya kitabu hiki kipo
maktaba na kinasomeshwa.

Bona,
Jitulize na taadab.

Wewe huna uwezo wa kupambana na mimi.

Waliodhaniwa wana uwezo wa kupambana na mimi huu mwaka wa
16 wako kimya wameshindwa hata kukifanya pitio kitabu changu.

Kitabu changu kimefanyiwa pitio na miamba wa African History - John
Iliffe
, Jonathon Glassman na Jim Brenan kutoka vyuo vikuu Uingereza
na Marekani.

Sasa tuje kwenye, ''untold story...''

Naam ni untold story kwa kuwa kabla ya mie kuandika mengi niliyoandika
hayakuwa yanajulikana.

Ikiwa ulikuwa unayajua uwanja uko wazi na wanajamvi wanakusubiri
kukusikiliza.

Karibu.

Mimi nimeingizwa katika Cambridge Journal of African History.
Sasa mimi nakupa wewe ''challenge,'' kama unavyoita wewe.

Tafuta wangapi katika hao unaowaamini wewe wameandika kitabu na
kikatiwa katika hilo journal la Chuo Kikuu cha Cambridge.


Quote By lukindo View Post
Kwa hiyo hiki kitabu kimeandikwa kwa ajili ya watu wote wanaopenda kujua historia ya Tanganyika au ni kwa hawa wenye access na haya maeneo uliyoyataja tu!?

Reply With Quote

Lukindo,
Nipe ruhusa nikueleza kwa mukhtasari historia ya kitabu hiki na usambazwaji
wake.

Hiki kitabu kilitoka kwa mara ya kwanza 1998 na kilichapwa London.
Uingereza kilikuwa kinapatikana Africa House, WH Smith na kwengineko pamoja
na Amazon.

Hapa nyumbani kikiuzwa Ibn Hazm Mtoro na Manyema na duka moja Mtaa wa
Kipata karibu na Msikiti wa Kipata.

Kitabu hiki kikakuzwa Tanzania Publishing House, Slip Way Bookshop hapa
Dar es Salaam, Kase Bookshop Arusha na maduka mengine siyakumbuki.

Hii ilikuwa nakala ya Kiingereza na toleo la kwanza.

Mwaka 2002 kitabu kikachapwa Nairobi kwa Kiswahili na kikauzwa katika hayo
maduka niliyotaja hapo juu.

Hili lilikuwa ndilo toleo la kwanza la Kiswahili.
Toleo la pili likachapwa 2008 na vitabu vikauzwa katika maduka hayo hayo.

Mwaka huu 2014 toleo la pili la Kiingereza limetoka pamoja na toleo la tatu
la Kiswahili.

Kwa kuwa kitabu ndiyo kwanza kimefika maduka yanayouza kitabu hiki ni
Ibn Hazm Mtoro na Manyema lakini wako wauzaji wadogo wadogo wanachukua
na kuuza mitaani mikononi nakala tatu, tano saba zikisha wanarudi dukani
wanachukua vingine.

Hivi sasa kitabu kinapatikana Soma Cafe Bookshop, Mikocheni na nadhani baada
ya wauza vitabu kujua kuwa kitabu kipo mjini wataagiza ili wauze madukani
kwao.

Hiki kitabu kimeingia dukani Jumatano iliyopita leo ni kiasi siku ya nane.
Tuvute subra vitapatikana kwingi tu ikiwa wauzaji vitabu watapenda kukiuza
kitabu cha Abdul Sykes.

Kwa kumalizia ningependa kuufahamisha ukumbi kuwa kitabu kinakwenda kama
maandazi ya moto.

No comments: