Msikiti wa Makonde umesoma khitma kumrehemu marehemu Sheikh Ali bin Sheikh bin Mzee Comorian. Katika mambo yaliyostaajabisha na kufurahisha ni kuona jinsi silsila ilivyoshika nafasi yake katika hafla ile. Angalia picha juu huyo anaeingia kibla kusalisha sala ya Isha kabla ya kisomo ni Sheikh Mahdi bin Sheikh Muharam bin Sheikh Saleh Kitembe ambae baba yake Sheikh Muharam bin Saleh alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir. Tusimame hapa kidogo. Sheikh Saleh Kitembe ndiye aliyekuwa Imam wa Msikiti wa Mwinyi Kheri Akida ulioko Kisutu katika miaka ya 1950/60. Msikiti wa Mwinyi Kheri Akida una zaidi ya miaka 100 na ndiyo msikiti mkongwe kupita yote Kariakoo. Sheikh Mahdi ni mmoja wa maimamu wa Msikiti wa Kisutu akifata nyayo za wazee wake. Huyo aliyevaa kanzu ya njano ni Sheikh Abbas bin Sheikh Ramadhani Abbas. Baba yake na baba yake Sheikh Mahdi, Sheikh Muharam Saleh wote walikuwa wanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir. Sheikh Ramadhani Abbas ndiye aliyesimamia mazishi ya Sheikh Mzee bin Ali Comorian. Sheikh Mzee Ali Comorian alipofariki mtoto wa Sheikh Ramadhani Abbas, Sheikh Abbas bin Sheikh Ramadhan Abbas ndiye huyu hii leo aliyesimamia mazishi ya Sheikh Ali Comorian. Kama hii haitoshi. Sheikh Zubeir Yahya Imam wa Msikiti wa Mtoro ndiye aliyetoa wasifu wa Sheikh Ali Comorian. Sheikh Zubeir ni mwanafunzi wa Sheikh Ramadhani Abbas. Aliyesoma dua ya mwisho alikuwa Sheikh Uwesu na yeye na Sheikh Zubeir wote walikuwa wanafunzi wa Sheikh Ramadhani Abbas na hawa wote hivi leo wako katika vyuo wakisomesha watoto Qur'an. Hawa masheikh zetu wameondoka lakini wameacha nyuma watoto na wanafunzi wema wanaoipigania dini ya Allah.
Imam wa Msikiti wa Mtoro Mwinyi Mangara Sheikh Zubeir Yahya MMoja wa Wanafunzi wa Sheikh Ramadhani Abbas |
Sheikh Mohamed Dedes |
Sheikh Mohamed Iddi |
Sheikh Uwesu Akisoma Dua Kushotoni ni Sheikh Abbas Ramadhani |
Balozi wa Comoro Akiwa Pembeni mwa Dr. Gharib Bilal, Sheikh Khamis na Balozi wa Iran |
Sheikh Ali Basaleh Aliyesimama Mbele Aliyevaa Kanzu ya Hudhurungi ni Mubarak Ghulum wa Radio Kheri Akisimamia Urushaji wa Matangazo Mubashara |
Add caption |
Kushoto Kwenda Ku lia: Mubarak Ghulam, Sheikh Katungunya na Abdallah Ubaya Ghulum na Ubaya Kutoka Radio Kheri Walikuwapo katika Hitma Kurusha Matangazo |
Rais Khalfani Jakaya Mrisho Kikwete nyumbani kwa Sheikh Ali Mzee Comorian Mtaa wa Kariakoo Picha ya Chini Sheikh Abdallah Miraj Akiomba Dua |
1 comment:
Kwake tumetoka na Kwake ni marejeo yetu...
Post a Comment