Jana baada ya sala ya Isha Waislam wa Masjid Nur Magomeni Mapipa walifanya kisomo cha kumrehemu Sheikh Ali Mzee Comorian kama picha inavyoonyesha hapo chini. Kisomo kiliongozwa na Iman Mkuu wa Masjid Nur Sheikh Nassor Bin Abdulrahman wa Jongo (aliyeko kibla picha ya pili) na katika waliohudhuria alikuwa Sheikh Hamisi Mataka mmoja wa wanazuoni wakubwa (mwenye kofia ya njano).
Radio Kheri usiku walirusha mubashara Kipindi Maalum Cha Maisha ya Sheikh Ali Mzee Comorian ambacho wasikilizaji walipiga simu kuchangia. Kipindi hiki cha saa moja kilajaa simanzi kubwa. Mwandishi alieleza maisha ya Sheikh Ali Comorian toka walipokuwa watoto wadogo wakiwa pamoja katika mitaa ya Kariakoo ya miaka ya 1960/70 hadi kufikia walipokuwa sasa watu wazima katika miaka ya 1980/90. Mwandishi aliwaeleza wasikilizaji wake historia ya wazazi wake Sheikh Mzee Ali Comoria na mkewe Bi, Maalim Bahia aliyekuwa mwalimu wa chuo akisomesha Qur'an. Halikadhalika wasikilizaji walielezwa historia ya masheikh wakubwa ambao kwa hakika ndiyo walimjenga Sheikh Ali Comorian katika dini, kama Sheikh Said Omar Abdallah (Mwinyibaraka) na masheikh wengine waliokuwa na baba yake kama Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Abdallah Idd Chaurembo, Sheikh Digila, Sheikh Ramadhani Abbas na wengineo. Wasikilizaji waliwekewa kasda ambazo Sheikh Ali Comorian alizutunga katika kumsifu Mtume SAW kiasi hata jina la Ashab Rasul likamwenea hadi kifo chake...
Kilichokwenda Hewani Mubashar
Kipindi Maalum Cha Maisha ya Sheikh Ali Mzee Comorian
|
No comments:
Post a Comment