Thursday, 1 January 2015

KHITMA YA SHEIKH ALI MZEE COMORIAN MSIKITI NGAZIJA 1ST JANUARI 2015

Msikiti Ngazija ni moja ya misikiti maarufu Dar es Salaam toka enzi na enzi na ni katika misikiti ambayo Mufti Sheikh Hassan bin Amir alipokuwa anatoa darsa zake toka alipohamia Tanganyika mwaka 1940 kutoka Zanzibar. Othman Miraj aliyekuwa mtangazaji maarufu wa Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Ujerumani anakumbuka darsa la Sheikh Hassan bin Amir katika miaka ya 1960 yeye akiwa kati ya wanafunzi vijana. Anasema siku moja ulikatika umeme kati ya Maghrib na Isha na wanafunzi walikuwa wako tayari darsa livunjwe kwa ajili ya kiza. Sheikh Hassan bin Amir akasema darsa lazima liendelee na akamwambia Othman Miraj achukue baskeli aende Kariakoo akalete taa ya kandili. Muda si muda Othman Miraj akawa kesharejea na taa  darsa ikaendelea. Baada ya darsa Sheikh Hassan bin Amir akamwambia Othman Miraj, ''Utakuja kulikumbuka darsa hili miaka mingi baadae.'' Othman Miraj anaendelea kuhadithia anasema hakika miaka mingi sana ikapita na yeye akawa amehamia Ujerumani kama mtangazaji katika Sauti ya Ujerumani Idhaa ya Kiswahili. Ikatokea Sauti ya Ujerumani wakata paweko na kipindi cha dini ya Kiislam. Ikawa tabu kumpata sheikh wa kuendesha kipindi hicho. Othman Miraj ikamjia fikra kuwa kwa nini yeye mwenyewe asikiendeshe kipindi hicho? Ndipo hapo alipomkumbuka Sheikh Hassan bin Amir na darsa la Msikiti Ngazija katika miaka ya 1960 yeye akiwa mwanafunzi. Othman Miraj alikiendesha kipindi kile kwa ufanisi mkubwa sana kiasi kuwa baadae aliweza kuwavuta masheikh wakubwa kuja kuzungumza katika Sauti ya Ujerumani mmojawapo akiwa Said Omar Abdallah (Mwinyibaraka) na Sheikh Aboud Maalim.


Mufti Sheikh Hassan bin Amir, Al Habib Omar bin Ahmed bin Abubakar  bin Sumeit
Nyuma Yake ni Ali Mwinyi Tambwe, Abbas Sykes na Chini ni Sheikh Kassim bin Juma
Aliyevaa Kashda






Sheikh Mzee Ali Comorian Baba Yake Sheikh Ali 




Picha Hii Ya Masheikh Maarufu wa Tanganyika na Zanzibar Ilipigwa Nyumbani kwa
Abbas Sykes Mtaa wa Shaaban Robert Mwaka wa 1962. Katika  Picha Hii Wapo
 Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Sayyid Omar bin Sumeit, Sheikh Mzee Ali Comorian,
Shariff Abdulkadir Juneid, Sheikh Kassim bin Juma, Abbas Sykes, Zuberi Mtemvu,
Ali Mwinyi Tambwe, Sheikh Kassim Juma na Wengine Wengi


Kushoto Kwenda Kulia: Shariff Al Hadi, Zuberi Mtemvu


Msikiti Ngazija








Dk. Hassan Mshinda, Dk. Ghalib Bilal na Balozi Badawy wa Comoro

Salim Ahmed Salim


Sheikh Mohamed Nassor akisoma Qura'an
Sheikh Zubeir Akitoa Wasifu wa Sheikh Ali Comorian Aliyekaa Chini Yake
Kulia ni Sheikh  Ahmed Islam


Dk. Salim Ahmed Salim Kwa Mbali ni Balozi Abbas Sykes
Sheikh Ahmed Islam na Balozi Abbas Sykes 
Kushoto Kwenda Kulia: Wawili wa Mwanzo ni Masoud Adam na Mohamed Nassoro Mabingwa wa Kusoma
Qur'an Kwa Tajwid na Dr. Tamim Bushiri


Baadhi ya Vijana wa Ashab Rasul Wakiimba Baadhi ya Tungo za
Sheikh Ali Mzee Comorian
Dk. Gharib Bilal na Dk. Salim Ahmed Salim

No comments: