 |
Jeneza la Sheikh Ali Comorian Likielekea Makaburi ya Wangazija Huku Manyunyu
Yaliyofuatiwa na Mvua Kubwa Yakidondoka |
Sheikh Ali Mzee Comorian amezikwa leo tarehe 29 Desemba 2014 sawa na tarehe 6 Mfungo Sita 2015 Makaburi ya Wangazija Mtaa wa Bibi Titi Mohamed. Sheikh Ali Comorian amezikwa pembeni kwa baba yake Sheikh Mzee Comorian. Kabla ya maiti kupelekwa Msikti wa Makonde kwa ajili ya Sala ya Jeneza na baada ya kusomwa khitma, ulisomwa mlangowa nne wa Barzanj kama alivyousia mwenyewe marehemu na hivi ndivyo ilivyokuwa pia katika mazishi ya baba yake Sheikh Mzee Comorian. Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi alikuwa mmoja wa waombolezaji. Sheikh Ali Hassan Mwinyi alikuwa karibu sana na Sheikh Ali Comorian wakati wa uhai wake. Balozi wa Comoro Tanzania alitoa rambirambi maalum kutoka kwa Rais wa Comoro. Mara tu baada ya kumaliza sala ya jeneza na wakati masafara unaanza kuondoka hapo msikitini ukiongozwa na magari ya polisi mvua kubwa sana ilianza kunyesha na ikafanya msafara uende taratibu sana na kwa watu kurowa. Kwa kipindi cha karibu saa mbili kulikuwa na na msongamano wa magari kuingia Mtaa wa Msimbazi kuelekea Morogoro Road kwenye makaburi ya Wangazija.
1 comment:
DAR ES SALAAM
Waislamu jijini Dar es Ssalaam leo wamemsindikiza katika makao yake ya mwisho mwanachuoni maarufu nchini Tanzania Marhem Sheikh Aliy Mzee Komorian baada ya kufariki dunia hapo jana.
Marhem Mzee Ali Komoria ameswaliwa katika msikiti wa Makonde, na kuzikwa katika makaburi ya Kazija jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi mbal;imbali wa dini na serikali akiwemo Raisi mstaafu Alhaj Aliy Hassan Mwinyi, Mufti wa Tanzania, Sheikh Issa Shaaban samba, Sheikh wa Mkoa wa dar es Salaam Alhad Salum, Mwenyekiti wa Umoja wa wanazuoni Tanzania, HAY IATUL ULAMAA, Sheikh Amran Kilemile, pamoja na maelfu ya waislamu wa jiji la Dar es Salaam.
Muda mfupi kabla ya kuswaliwa Marhem Komoria, Muhadhir kutoka chuo kikuu cha Waislamu Morogoro, Sheikh Mohammed Dedes amesema kazi kubwa iliyofanywa na Almarhoom sheikh Komoria ni kumuenzi Mtume (SAW).
Kwa upande wake, Sheikh wa mkoa wa Dar es salaam, Alhad Mussa Salum amesema, miongoni mwa watu walioweza kumnusuru vyema Mtume (SAW) katika zama hizi nimarhem Sheikh Komoria.
Naye mwenyekiti wa Umoja wa wanazuoni Tanzania HAY ATUL ULAMAA Sheikh Kilemile amesema katika kumuenzi Bwana mtume (SAW) Sheikh Komoria ni miongoni mwa watu walioweka mfano na kiigizo kikubwa katika kumuenzi Bwana Mtume (SAW)
Post a Comment