| Sheikh Ali Mzee Comorian Akizungungumza Katika Khitma Saigon Club Tarehe 24 Juni 2012 |
| Sheikh Ali Mzee Comorian |
Sheikh Ali Mzee Comorian
amefariki hii leo tarehe 28 Desemba 2014 sawa na tarehe 5 Rabbi Awal au Mfungo
Sita 1436. Binafsi habari zimenifikia kabla ya sala ya Dhuhr. Siwezi kusema ni lini nimemjua Ali Mzee Comorian au ni lini kwa mara
ya kwanza nilifahamiananae na kumtia machoni. Siwezi kusema hayo kwa kuwa Ali
Mzee tumekuwa na kucheza pamoja katika mitaa ya Dar es Salaam ya 1960. Leo
nikiangalia nyuma naona kama vile ni jana tu kushinda leo. Nawakumbuka marafiki
zake wakubwa marehemu Ahmada Digila (mtoto wa Sheikh Digila mmoja wa wanafunzi
wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir) na Said Mohamed Marjebi. Ali Mzee Comorian ni mtoto
wa Sheikh Mzee Comorian (mshairi bingwa wa kutunga mashairi ya kumsifu Bwana
Mtume SAW na yeye pia alikuwa mwanafunzi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir). Mama yake Ali Mzee Comorian ni Maalim Bahia, mama maarufu Dar es Salaam na mwalimu wa
Qur'an katika madras yake mashuhuri ya Maalim Bahia iliyoko Mtaa wa Kariakoo. Hawa ndiyo wazazi wake Ali Mzee Comorian.
Mara tu baada ya kifo cha Sheikh Ali Comorian kufahamika ujumbe ulianzwa kutumwa katika mitandao yote taarifa zikipishana ikiingia hii inakuja nyingine kukupa taarifa ileile na ya msiba ule ule. Sheikh Ali Comoria alikuwa mtoto wa mjini, mtu wa watu na sheikh maarufu katika masheikh wa mji kiasi watu wakawa wanamwita ''Sheikh wa Dar es Salaam.'' Katika hafla yoyote Sheikh Ali kama hataitwa kuzungumza basi ataombwa mwisho atoe dua na hapo ndipo Sheikh Ali alipokuwa akiwapeleka wazee masheikh wa Dar es Salaam akiwarudisha nyuma enzi za baba yake Sheikh Ali, Sheikh Mzee Comorian kwa sababu Sheikh Ali Comorian alisoma dua za mashairi alizotunga marehemu baba yake. Haya yalikuwa mashairi aliyotunga Sheikh Mzee Comorian zaidi ya miaka 50 iliyopita na yalichapwa kwenye kitabu. Jina la kitabu limenitoka lakini nakumbuka kitabu kilikuwa na picha yake kavaa joho na kafunga kilemba. Nimewahi mara nyingi kumuuliza Sheikh Ali kuhusu kukichapa kitabu kile ili watu wa hivi sasa wanufaikenayo. Bahati mbaya hadi leo kitabu kile hakijachapwa.
Mimi binafsi ingawa umri wetu ulikuwa sawa na mchezo wetu ulikuwa mmoja mimi siku zote nikimpa heshima Sheikh Ali kwa ajili ya elimu yake ya dini. Sheikh Ali Comorian baada ya kumaliza elimu ya sekondari Kinondoni Muslim School wao wakiwa wanafunzi wa mwanzo kabisa. Sheikh Ali Comorian alisoma Shule ya Kinondoni darasa moja na mwanamuziki maarufu marehemu Marijani Rajab. Katika mazishi ya Marijanoi Rajab Ali Mzee Comorian ndiye aliyeongoza shughuli ile na na akatoa taazia nyumbani kwa marehemu na kusoma dua makaburi ya Kisutu. Nakumbuka shule ya Kinondoni ilijengwa na East African Muslim Welfare Society na ilimalizika mwaka wa 1967 na wanafunzi wa mwanzo walianza kusoma katika madarasa ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika Mtaa wa Lumumba na shule ya Kinondoni ilipomalizika ndiyo wakahamishiwa huko. Hili nalikumbuka vyema kwa kuwa rafiki yangu Juma Hassan Heri alikuwa mmoja wa wanafunzi walioanzisha Shule ya Kinondoni nami nilikuwa nikimfuata pale Al Jamiatul Islamiyya Muslim School mimi nikiwa bado niko shule ya msingi. Juma Heri alikuwa na kipaji cha hali ya juu sana katika mpira. Hiki ndicho kitu kilichotuunganisha. Wakati huo tukicheza club yetu tuliyoipa jina Everton na tukivaa jezi za bluu kama Everton yenyewe ya Uingereza. Hii Everton ndiyo baadae ikajabadilisha jina na kuwa Saigon.
Ali Mzee Comorian hakuwa katika kundi lile la akina Juma Heri nadhani yeye aliingia mwaka uliofuatia mwaka 1968. Rafiki yangu Juma Heri baada ya kupoteana miaka mingi nikaja kusikia kuwa alihamia Marekani na huko amefariki miaka michache iliyopita Baada ya elimu ya sekondari Ali Comorian alijikita zaidi katika elimu ya dini na kwa ajili hii akaingia katika orodha ya masheikh vijana katika mji wetu. Wakati mimi na akina Hassan Heri tukiwa tumeshughulishwa na kucheza mpira viwanja vya Mnazi Mmoja na Jangwani pamoja na sahib kipenzi wa Ali Comorian, marehemu Ahmada Digila ambae na yeye alikuwa mtoto wa sheikh maarufu, Sheikh Digila, Ali Comorian yeye alikuwa katika Msikiti wa Badawy ambako Sheikh Hassan bin Amir akitoa darsa. Hapo Ali Comorian akiwa na umri wa kiasi cha miaka 14 hakuwa mbali na jicho la baba yake ambae alikuwa katika darsa alilokuwa akisomesha Mufti Sheikh Hassan bin Amir. Ali Mzee Comorian alikuwa katika makuzi ya namna hii. Hili utaliona kwa Sheikh Ali Comorian jinsi alivyokuwa anazijua kasda na nyuradi nyingi zilizokuwa zikisomwa pale Badawy. Hivi sasa Badawy inaitwa Masjid Rawdha.
Sheikh Ali Comorian alikuwa akimpenda sana Sheikh Said Omar Abdallah kwa jina lingine Mwinyibaraka. Kila Mwinyibaraka akija Dar es Salaam kutoka Ngazija yeye alikuwa ubavuni kwa sheikh Mwinyibaraka. Mwinyibaraka alikuwa katika marafiki wakubwa wa baba yake. Katika miaka ya mwishoni 1970 kuelekea 1980 Mwinyibaraka alikuwa akipenda kuja Dar es Salaam akitokea Ngazija na kutoa darsa zake Mtaa wa Pemba nyumbani kwa Mama Nuru. Kwa kawaida Mwinyibaraka alikuwa akija kuzungumza Msikiti wa Manyema ambako pale alikuwapo Sheikh Aboud Maalim. Lakini akiwa katika mapuziko nyumbani kwa Mama Nuru Mwinyibaraka alikuwa anapenda kufanya darsa na vijana wa mtaani. Huu ulikuwa uradi wa Mwinyibaraka hadi anafariki. Sheikh Ali Comorian alikuwa mmoja wa wanadarsa hili na alisaidia sana kulistawisha kwani alilitangaza kwingi kwa vijana wenzake na wengi walipendezewa na yale ambayo waliwakuwa wakiyasikia kutoka kwa Ali Mzee Comorian kwa hivyo walivutiwa na wao wakaja katika darsa. Ali Mzee Comorian alichukuliwa sana na Mwinyibaraka kiasi ikawa anamuiga hata uzungumzaji wake na uwasilishaji wake wa mada. Marehemu Sheikh Kassim Juma na masheikh wengine wa kizazi kipya walijaribu sana kumuiga Mwinyibaraka lakini katika watu waliokuwa wanampatia sana Mwinyibaraka ni Sheikh Ali Mzee Comorian labda hii ni kwa kuwa Ali Mzee akijua vyema Kiingereza na Mwinyibaraka, msomi wa Chuo Kikuu Cha Oxford Uingereza kwake yeye haikuwa tabu kufanya rejea kutoka vitabu vya Kiingereza kwa lugha ya Kiingereza kisha ndipo akafanya tafsiri. Basi kwa kuwa Ali Mzee alikuwa na kipaji cha kuzungumza na akifuata nyayo za ''mentor'' wake Mwinyibaraka kwa hakika Ali Mzee Comorian akizungumza utapenda aendelee kuzungumzana hutochoka kumsikiliza sikwambii akiwa anasoma dua kwa mashairi. Mwinyibaraka alimpa Ali Mzee Comorian ijaza ya kusimamia ile zawiyya nyumbani kwa Mama Nuru na hapo pakawa kituo cha watu wa kheri kwa miaka mingi hadi Mama Nuru alipohama hapo na zawiyya ikahamia Mission Quarters nyumbani kwa kijana mwingine mwanadarsa Sheikh Abdulswamad.
Sheikh Ali Comorian alianzisha kundi lililo maarufu katika shughuli za Kiislam na alilipa jina Ashab Rasul - Wapenzi wa Mtume SAW. Sheikh Ali Comorian ndiyo mtunzi wa kasda maarufu ambayo inasomwa na karibu vyuo vyote Dar wa Salaam. Kasda hii inaitwa ''Haya Tumpendeni Mtume Rasul,'' Sheikh Ali Comorian katunga kasda nyingi sana ambazo leo ni maarufu katika radio za Kiislam na katika masikio ya wengi na zote hizo mashairi yake yalikuwa katika kumsifu Mtume SAW.
Rafiki yangu, ndugu yangu Farouk "Encyclopedia'' Hussein kaniletea ujumbe wa Whatsapp akisema kwa masikitiko, "Abu Faraj, Dar es Salaam imeondokewa..."
Hakika kwa kifo cha Sheikh Ali Mzee Comorian Dar es Salaam imepungukiwa katika hesabu zake.
Sheikh Ali Comorian amefariki katika mwezi huu wa Mfungo Sita ambao sehemu nyingi hasa hapa Dar es Salaam maulid husomwa kusherehekea mazazi ya Mtume SAW Waislam watakaohudhuria hafla hizo bila shaka watamkumbuka Kipenzi cha Mtume Sheikh Ali Comorian kwa kuwa hivyo ndivyo vilikuwa viwanja vyake na zaidi watakapoisikia kasda yake, "Haya Tumpende Mtume Rasul.''
Hakika Kwake tumetoka na Kwake ni marejeo yetu.
Allah amghufirie ndugu yetu Sheikh Ali Mzee Comorian dhambi zake na amtie peponi.
Amin.

No comments:
Post a Comment