Monday, 19 January 2015

MAHAKAMA YA KADHI: BARAZA KUU YAWASILISHA MAPENDEKEZO YA WAISLAM KWA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA


Kushoto Kwenda Kulia: Sheikh Eng. Ali Kilima, Sheikh Amrani Kilemile
na Sheikh Mussa Kundecha

Wajumbe wa Baraza Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam
Wakiwa Masjid Maamur na Picha ya Chini Wakiwa
Mwalimu Nyerere Conference Centre





Wajumbe Wakipanda Ngazi Kuelekea Kwenye Chuma Cha Mkutano

Kushoto Kwenda Kulia Mbele: Sheikh Abdallah Bawazir, Sheikh Mussa Kundecha
Sheikh Amrani Kilemile, Shamim Khan na Jaji Robert Makaramba

Yahya Njama Aliyewasilisha Mapendekezo ya Waislam



Yahya Njama Akihojiwa na Athman Shomari wa TV Imaan Baada ya Kumalizika Kikao







Sheikh Hamid Jongo Aliwakilisha  BAKWATA  Akizungumza na Eng. Sheikh Ali Kilima




Wajumbe wa Baraza Kuu Wakitoka Kwenye Ukumbi wa Mkutano




Sheikh Abdallah Bawazir ametufanyia ihsani ya kutuandikia mukhtasari huo hapo chini:
Waliohudhuria katika mkutano huo jana kwa upande wa Masheikh walikua ni makundi mawili.
1. Bakwata 
2. Kundi la taasisi 11 (Tampro, Baraza Kuu, Hay-at ...) na wengineo. 

Makundi yote yalikua yana masheikh wazuri kwa elimu na amali na lengo lao lilikua ni moja la kutaka Waislam nchini wawe wana Mahakama ya Kadhi rasmi inayokubaliwa na Dola lakini walitofautiana  katika mambo fulani  katika muundo wa Mahakama hiyo. 

Baadhi ya mambo hayo ni: 
1. Ni nani mwenye haki ya kumuaini Kadhi 
2. Nani atagharamia Mahakama hiyo.

Bakwata wanasema kuwa Mufti wao ndie mwenye haki ya kumuaini Kadhi kwa sababu yeye ndiye kiongozi mkuu wa nchi. Aidha Bakwata walimesema kwamba hapana haja ya Mahakama kuagharamiwa na Serikali bali Waislamu wanao uwezo huo. 

Mkutano ulianza kwa Tamko  la  Mhsh. Jaji Robert Makaramba (Mkatoliki mwenye ujuzi mzuri pia wa Sharia ya Kiislaam kiasi chake) . Msemaji wa pili alikua ni upande wa Bakwata ambae ni Sh. Lolila Katibu Mkuu. 

Ama Taasisi 11 (Nahli, Basuta, Dumti, IPC  na nyengine zote) msemaji wao alikua ni Mwanasheria wa Hay-at (Yahya Njama). Baada  ya hapo yalikuja matamko mengine kama tamko la msemaji wa Umoja Wa Wanasheria nchini. 

Katika watu muhimu waliohudhuria ktk Kikao hicho ni Attorney General Mhsh. Masaju na baadhi ya Wabunge wa vyama tofauti. Hoja ambayo haikupata nafasi ktk kikao hicho na wajumbe wengi kuipinga ni kile kifungu kinachotaka Mufti wa Bakwata ndiye mwenye haki ya kumuaini Kadhi. 

Kifungu hicho kilipingwa kwa hoja zifuatazo: 
1. Mufti ni kiongozi wa Bakwata tu. Hana uwezo wa kuaini Kadhi kinyume cha Taasisi nyengine.  2. Tanzania tangu kujitawala leo ni nusu karne ktk kipindi hicho vijana wamesoma dini ktk nchi tofati wakapata elimu ya Sheria ya Kiislam kubwa na shahada. Vijana hao ndiyo muda huo wenye haki ya kuwa makadhi na kuunda bodi itakayokua na uwezo wa kumuaini Kadhi Mkuu na kuweka kanuni za kuendesha mahakama hiyo nchini, vipi Mufti wa Bakwata ataweza kuchukua jukumu hili.  

Mwisho, mapokezi ya wenyeji wa mkutano huo walionyesha upendo na heshima kubwa kwa masheikh wetu  na makaribisho yao yalikua mazuri mwanzo wa shughuli hadi mwisho. 
Walilliahi lhamdu.


No comments: