[QUOTE=SoNotorious;11639824]Tatizo ni kuwa ukweli wa mapinduzi anaujua Mohamed Said na Harith watu wengine wote walikuwa wajinga na vipofu wakati mapinduzi yanatokea
[video=youtube;7uPi3vh2hGE]https://www.youtube.com/watch?v=7uPi3vh2hGE[/video][/QUOTE]
SoNotorious,
Unatukebehi.
Hii si dalili nzuri kwako.
Inaonyesha kushindwa na hoja zangu.
Mimi huwa sizungumzi kile nisichokijua naogopa kufedheheka.
Tungejuaje historia ya mapinduzi kama wale walioshiriki hasa
wasingetukalisha chini na kutusomesha?
Tungeliyakuaje ya Kipumbwi na Sakura kama Victor Mkello na
Mzee Mkwawa wasingetufungulia milango ya siri ile nzito ya
mamluki wa Kipumbwi?
Dr. Ghassany alifanya utafiti wa miaka.
Kapita maktaba nyingi Amerika na Uingereza hadi nyumbani kwa
Mzee Mkwawa Makorola Tanga na Nguvumali.
![]() |
Mohamed Omari Mkwawa |
Huko hakuonyeshwa nyaraka.
Kule alielezwa kuhusu kambi ya askari mamluki wa Kimakonde
wakata mkonge kutoka shamba la Sakura waliokuwa wakifanya
mazoezi ya kuvamia Zanzibar porini.
Regional Commissioner Jumanne Abdallah na Area Commissioner
Ali Mwinyi Tambwe wote wakisimamia mpango ule.
Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mmoja wa watu ambao hawakutaka
ijulikane kuwa alihusika katika mapinduzi.
Ali Mwinyi Tambwe alikataa kuzungumza na marehemu Prof.
Haroub Othman alipomgusia habari ya mapinduzi.
Nafsi yake iliingia hofu kubwa alipokujajua watu waliouliwa katika
mapinduzi yale.
Dr. Ghassany hakuyakuta haya ya Sakura, Kipumbwi na mamluki
wa Kimakonde katika utafiti wake Library of Congress Washington
wala Rhodes House Oxford.
Haya kaja elezwa Tanga Makorola na Nguvumali na watu ambao
hakuna aliyekuwa anajua mchango wao.
Hakika kwa kiasi chetu tunaijua historia ya mapinduzi.
Ilimchukua miaka mitatu kwa Dr. Ghassany kuweza kumshawishi
Victor Mkello kumuamini kuwa likuwa ni mtafiti wa kweli na wala
hatoki International Criminal Court (ICC) Hague ndipo alipokubali
kuongea.
Mimi nilikuwapo katika mahojiano yote ya miaka mitatu ya nyuma
isipokuwa huu wa mwisho alipofunguka na kueleza ukweli wa yale
waliyofanya katika kuivamia Zanzibar kutoka Kipumbwi.
Mimi nilibaki nje nimeegesha gari yangu msikitini.
Nilijua kuwa hii ndiyo ile kubwa yake nilitaka Dr. awe na ''one on
one,'' na Mzee Mkello.
Baadae Dr Ghassany aliniambia kuwa mama yetu mkewe Mzee
Mkello alikuwapo katika mazungumzo yale na sababu yake ni kuwa
Mzee Mkello alitaka ili akikosea au kusahau jambo amkumbushe.
Soma ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,'' umsikilize nini Mkello
alisema.
Baada ya Dr. Ghassany kueleza yale yaliyopitika Kipumbwi kati
ya 1961 na 1964 kwa watu kuvushwa kutoka Tanganyika kwenda
kuipigia kura ASP Uchaguzi wa 1961 na kufanya mapinduzi mwaka
wa 1964 watafiti wengi wa nje wakataka kuja Tanga kufanya utafiti
wa uthibitisho.
Picha hiyo hapo chini mmoja wa watafiti kutoka Marekani akimhoji
Mama Mkello nyumbani kwake Nguvumali, Tanga. Kipindi hiki
mumewe tayari alikuwa keshafariki.

Philomon Mikael,
Nakuomba hebu linganisha maelezo uliyobandika na jibu langu kwa
SoNotorious.
Naamini utaona mpishano uliokuwapo.
Mapinduzi ya Okello ni mapinduzi ya kuzuka usiku mmoja.
Mapinduzi niliyoeleza mimi kwa kumnukuu Dr. Harith Ghassany ni
mapinduziyaliyopangwa na kuratibiwa na wajuzi wa mipango -
Abdullah Kassim Hanga,Oscar Kambona juu kwenye kinara.
Chini yao kwenye ''Zone of Operation,'' kuna maofisa wa serikali ya
Tanganyika-Jumanne Abdallah na Ali Mwinyi Tambwe.
Chini ya hawa kuna Mohamed Omar Mkwawa na Victor Mkello.
Hawa ndiyo walikuwa wakiwasiliana na mamluki wa Sakura na
Kipumbwi.
Nadhani hii ''Chain of Command,'' unaiona.
Nani anawajibika kwa nani na kwa kipi.
Mzee Mkwawa anasema hata siku moja Kambona wala si Hanga
walifika kambini Kipumbwi kuzungumza na ''askari.''
Simlazimishi mtu kuamini yale aliyoeleza Dr. Ghassany kwenye
kitabu chake, ''Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru'' lakini Waswahili
tuna msemo, "Penye ukweli uongo hujitenga.''
kufanya yote aliyofanya na kusababisha mauaji ya maelfu ya watu.
No comments:
Post a Comment