Re: Ukweli kuhusu mapinduzi ya zanzibar
Re: Ukweli kuhusu mapinduzi ya zanzibar
Monday, 12 January 2015
KUTOKA JAMIIFORUMS KUHUSU ''MSOMI'' OKELLO
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
activist
Activisty,
Halikupata kuwa suala la woga.
Woga wa kuogopa kitu gani au kumuogopa nani.
Nakueleza kitu ninachokijua.
Mimi ni mwandishi na nimeandika vitabu kadhaa.
Halikadhalika nimekuwa Msaidizi Mtafiti wa Dr. Harith Ghassany wakati anatafiti na kuandika, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru.''
Tumepita kwingi, tumesoma mengi na tumesikilizishwa mengi...
Okello tumemfahamu vyema kabisa...
Okello hakuwa na uwezo wa kuandika kitabu kile.
Badawiy Qullatein alikuwa rafiki yangu na kanieleza mengi
kuhusu Okello.
Naamini unamjua Qullatein...
Ikutoshe tu katika vyeo vya kijeshi alijichagulia cheo cha, ''Field
Marshal.''
Wala Okello hakupatapo kujua nini maana ya ''Field Marshal'' wala
kujua kuwa cheo hicho alikuwanacho Tito wa Yugoslavia na wala
hakupatapo kujua Field Marshal Tito alikipataje cheo hicho.
The Fifth Offensive...Second World War, Partisan Army...
Historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ina vichekesho vya kila aina.
Hiki cha Field Marshal Okello kimefurtu ada.
Labda nikuulize kitu.
Kabla ya kitabu kile wewe umepata kuona chochote alichoandika
Okello?
Kama kuandika kuhusu mapinduzi angeliandika Abdulrahman
Babu siyo Okello.Babu hakuandika hadi anaingia kaburini.
Jiulize kwa nini...
Majibu tunayo.
Okello ni mtu mjinga wale jamaa zake wangelikwenda Nuremburg
Okello ndiye angening'izwa kwa ushahidi wake mwenyewe.
Msome Ghassany anavyoeleza ''blanketi'' alilovishwa Okello na hilo
''blanketi,'' likamwenea khasa...
Wenye shughuli yao wakicheka hadi machozi yanawatoka.
Last edited by Mohamed Said; Today at 22:56.
Introduction Below is a cut and paste from Wikipedia. Please compare and contrast between Ton Ton Macoute of Haiti and Zombies of Zanzi...
No comments:
Post a Comment