Wednesday, 28 January 2015

KUTOKA JF: MAHAKAMA YA KADHI BOBUK AULIZA MASWALI


Quote By Bobuk View Post
Kama suala la mahakama ya kadhi ni suala linalowahusu waislamu tu, na sisi tusio waislamu tukae pembeni, Sasa kwanini?
  1. Mnataka muswaada wa mahakama ya kadhi ujadiliwe ktk Bunge la JMT? au Bunge la JMT limekuwa Baraza la MAULAMAA
  2. Kwanini basi mnataka kodi zetu tusio waislamu zitumike kuendesha hiyo mahakama yenu ya kadhi?



Naomba majibu ya maswali yangu hayo mawili.

Bobuk,

Nataka nikupe mfano ili ujielewe na pengine wengiine nao wenye 

fkra kama wewe na wao wajifahamu.


Katika uchezaji mpira ili uwe mchezaji mzuri na uumudu ule mpira

wenyewe kuna kitu kinaitwa, ''ball control,'' yaani kuumudu mpira 

wenyewe utulie katika miguu ya mchezaji.


Katika hii, ''ball control,'' inaingia upigaji wa danadana.



Ikiwa mchezaji hawezi hata kupiga danadana itakuwa shida sana 

kwake kuwa mchezaji wa maana. 



Ikiwa unajifunza kupiga gitaa ni lazima ujue, ''cromatics,'' yaani 

kutembea katka ''frets,'' bila kwenda, ''off - key.''



Vinginevyo nje ya hapo utakuwa kichekesho.



Ninachokiona hapa na kwa kweli kwa wachangiaji wengi ni kuwa 

hajui historia ya Tanganyika.



Hawajui kuwa Mahakama ya Kadhi zilikuwapo hata wakati wa ule

wa ukoloni.



Vipi na nani aliziondoa hilo ni somo la kujitegemea lenyewe na 

ili ujue kwa nini na nani aliziondoa ni lazima uijue historia ya 

Tanganyika.


Sheikh Said Chaurembo alikuwa akihukumu katika Mahakama 

ya Kariakoo.



Huyu mwaka 1950 alikuwa katika TAA Political Subcommitee 

iliyokuja kuunda TANU mwaka wa 1954.



Si hilo tu kamati hiyo ndiyo iliyoandika hotuba iliyosomwa UNO 

na Nyerere mwaka 1955.



Ndugu yake akiitwa Sheikh Abdallah Chaurembo yeye mwaka 

1955 akiwa na Mwalimu wake Mufti Sheikh Hassan bin Amir na 

Sheikh Nurdin Hussein walikuwepo katika mkutano wa siri ambao
uliweka msimamo wa kuifanya TANU kiwe chama cha kisekula 
ili kupunguza joto la Uislam lililokuwa linazizima
ndani ya chama. 



Je wewe katika umri wako wote umepata kumsikia Sheikh Hassan

bin Amir akihusishwa na historia ya ukombozi wa Tanganyika?



Jiulize kwa nini?



Mahakama ya Kadhi ilikuwa Songea ambapo Sheikh Abdallah 

Simba akihukumu. 



Huyu Sheikh Abdallah Simba alikuwa rafiki mkubwa wa babu 

yangu Salum Abdallah mmoja wa waasisi wa TANU Tabora na 

muasisi wa Tanganyika Railway African Union mwaka 1955 yeye 
akiwa rais muasisi katibu wake akiwa Christopher Kassanga 
Tumbo.



Kulikuwa na Mahakama ya Kadhi Moshi Bomani na Liwali Mussa 

Minjanga alikuwa hakimu.



Huyu Liwali Mussa Minjanga akifahamiana vyema na baba yangu.



Tabora alikuwapo Liwali Bilal Mshorwa akihukumu mahakamani 

na yeye pia akifahamiana vyema na babu yangu kwa kuwa wote 

ndiyo walikuwa wazee wana wa mji.


Mahakama hizi ndizo zilizokuwa zikihukumu kesi sote za ndoa, 

talaka na mirathi na hapakuwa na tatizo lolote na zilidumu hadi 

1963.


Shida ilikuja pale ukoloni ulipoanguka na Kanisa likaweka mikakati

ya kuitawala Tanganyika na kuvunja nguvu ya Uislam.



Ndiyo maana leo unaona hata historia ya kweli ya uhuru wa nchi

yetu Tanganyika haitakiwi.

Ikiwa unapenda kusoma historia hii soma kitabu changu,''The 

Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968 Struggle) 

The Untold Story of the Muslim Struggle Against British 
Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press, London,1998.



Bobuk,
Naamini unajua kuwa Serikali inatoa bilioni 91 kila mwaka kwa


Makanisa ili yaendeleze shughuli zake.

Niwie radhi kwa kukuchanganyia habari nyingi mahali pamoja.

Nimefanya hivi makusudi ili kwanza uelewe kuwa baadhi yetu

tumekuwa na historia hii kwa hiyo tunaujua ukweli.


Kanisa limejipenyeza miaka hii baada ya uhuru na ndiyo unaona

hii chuki iliyojengeka.



Kabla ya hapo nchi yetu Waislam na Wakristo walikuwa wamoja.

Soma historia itakueleza.



Mwalimu Nyerere angelikuwa hai tungemuomba awaeleze nduguze 

nani walimpokea Dar es Salaam na nani waliomuweka katika uongozi

wa Tanganyika.


Hatujachelewa Mama Maria yu hai.
Last edited by Mohamed Said; Today at 12:08.
Edit / Delete

No comments: