
By
Ngongo 
Nafahamu unapenda kunukuu kitabu cha Padri John Sivalon lakini nashindwa kukuelewa unapotoa nukuu ambazo wewe binafsi unashindwa kuzitetea.Unaposema bunge linamilikiwa 94% na wakristo ukiambiwa ebu tupatie takwimu kuanzia bunge kipindi cha Mwl Nyerere hadi Kikwete unakimbilia kitabu cha Padri Sivalon wapi na wapi.
Kwa taarifa yako Mwl Nyerere ndio mwanasiasa aliyetengeneza formula inayowaweka mbele waIslam.Tazama bunge la JMT Zanzibar nchi yenye idadi ya watu wasiozidi 2 milioni ambao wengi ni waIslam ina wabunge zaidi ya 60 ambao ni waIslam.Mkoa wa Mwanza una idadi ya watu 2,772,509 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 na idadi ya wabunge wa kuchaguliwa wasiozidi saba ambao majority ni wakristo sasa kama kulikuwa na mpango wa kupendelea wakristo Mwanza yenye idadi idadi kubwa ya wakristo isingetoa wabunge saba huku Zanzibar yenye idadi kubwa ya waislam ikatoa wabunge 70.Unapotoa nukuu ya kitabu cha Padri Sivalon unapaswa kuja mifano yenye mashiko bado sijaenda mkoa wa Kilimanjaro wenye idadi ya watu 1.6 milioni ina wabunge wa kuchaguliwa tisa !.
Nimejaribu kukuonyesha jinsi nukuu yako toka kitabu cha Padri Sivalon inavyopingana na hali halisi ilivyo katika bunge la JMT.Nakuomba na wewe uje na mifano yako itakayoonysha jinsi bunge lilivyotekwa kwa 94% na wakristo ukishindwa kufanya hivyo basi siku nyingine usitumie nukuu za hicho kitabu kwakuwa kinapotosha na si vizuri kwa msomi kama wewe kuendelea kuchota nukuu wakati unajua wazi unadanganya jamii.
No comments:
Post a Comment