
By
Ngongo 
Ha ha ha ha ha Sheikh
Mohamed Said kitabu chako cha kichochezi si miongoni mwa vitabu rejea chuo kikuu cha Dar jiulize kwanini ?.Ikiwa wewe unadai umeandika kitabu cha historia ya kundwa TANU ni kwanini kitabu chako hakisomeshwi mashuleni hapa nina maana kuanzia darasa la kwanza hadi A Level ?.Ni kwanini si rejea katika vyuo vikuu ?.Kitabu chako kinaweza kusomeshwa labda chuo kikuu cha Morogoro.
Ngongo,
Hiyo si hoja.
Labda nami nikuulize.
Kwa nini kitabu changu hakisomeshwi Chuo Kikuu cha St. Augustine lakini
kinasomeshwa vyuo vyote Marekani na Ulaya?
Sasa wewe si wa kutoa jibu.
Jibu wacha litolewe na Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mbona hujagusa matawi ninayokalia?
Yanakutisha?
Hivi unajua kama mimi nimo kwenye list ya Dictionary of African Biography?
Hivi unajua huu mradi ulikuwa wa Harvard na Oxford University Press,
New York?
Ikiwa hawa huwajui uliza utaambiwa hawa ni nani katika duru za kisomi na
uchapaji.
Wewe uko kwenye s...list.
Hahahahahahahahahahahah!Jamani mbavu zangu.
Ngongo,
Niangalie hapa chini:
Unapajua hapo?
Hapo ni BBC.
Siyo BBC London, Bush House.
Hapana.
Hapo ni BBC Glasgow.
Unajua nafanya nini?
Nafanya kipindi cha historia ya Afrika.
Unajua ni lini?
1991.
Si unaona nilikuwa mdogo.
Kufa kwa roho yako mbaya ya choyo na wivu.
Ati mbona kitabu changu hakisomeshwi Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.
My foot!
Usithubutu kurudi na utumbo wako hapa jamvini.
Ndiyo nitakumaliza kabisa.
Ngongo,
Hunijui.
Nataka leo unijue.
Si tu "The Life and Times of Abdulwaid Sykes..." kimepigwa pande
hakisomeshwi hapa nchini.
Nina kitabu kingine kilichochapwa na mabingwa wa uchapaji nacho
vilevile kimekataliwa hakisomeshwi.
Lakini kitabu hiki kinasomeshwa shule zote Kenya na Uganda.
Kitabu hiki kipo katika mradi wa kusomesha Kiingereza shule za
msingi lakini hapo hapo watoto wajifunze na historia za nchi zao.
Kitabu hiki kinaitwa, "TheTorch on Kilimanjaro," Oxford University Press,
Nairobi, 2006.
Mimi siyo bongolala kama wewe.
Ubongo wangu unafanyakazi.

Mohamed Seif Khatib Akizindua Kitabu Changu Mbele ya Viongozi wa Wizara ya Elimu Kempisky Hotel Mwaka 2006
No comments:
Post a Comment