Quote By Matola View Post
Mzee MS,

Hapa natumia simu kuna bandiko umesema Nyerere alikuja Dar mji wa waislamu nakupokewa na hao wazee uliowataja,

Mimi nilikuwa sijazaliwa bado na somo la historia shuleni huenda halijakamilika sasa ningependa kujuwa wakati huo mji wa waislamu ulikuwa ni upi na upi na kwa mujibu wa nani? Pia miji ya Wakristo ni ipi na ipi na kwa mujibu wa nani?
Matola,
Mimi nitakujibu Dar es Salaam ya 1950 ambayo mimi nilizaliwa.

Kuhusu miji ya Kikristo sina ujuzi kwa hiyo sitasema lolote:

"Mji wa Dar es Salaam katika miaka ya 1920 ulikuwa umegawanyika katika
sehemu nne: Kariakoo, Gerezani, Kisutu na Misheni Kota.

Sehemu ya ukazi wa asili ilikuwa Kisutu.

Kisutu una msikiti wa zamani kuliko yote katika Dar es Salaam - Msikiti wa
Sheikh Mwinyikheri Akida, unaokaribia takriban miaka mia moja hivi.

Vilembwe wa Sheikh Mwinyikheri hadi leo wangali wakiuhudumia msikiti
wa mzee wao na msikiti huo bado uko chini ya uangalizi wao.

Kariakoo ilikuwa sehemu ya kuandikisha wapagazi wakati wa Vita Kuu vya
Kwanza.

Jina lenyewe, "Karikaoo," linatokana na jina la Kizungu, "Carrier Corps."

Misheni Kota ilikuwa sehemu iliyotengwa makhsusi na Waingereza kwa ajili
ya Wakristo.

Wakati ule Wakristo hawakuwa wengi Dar es Salaam, kwa ajili hii walitengewa
sehemu yao maalum ya kuishi ili wasichanganyike na Waislam.

Misheni Kota ilikawa sehemu ya kuishi Wakristo kiasi ambacho hata mitaa
yake ilipewa majina ya sehemu katika Tanganyika ambako Wamishionari
walikuwa wamejipenyeza na kuweka maskani.

Majina ya mitaa kama Masasi, Likoma, Ndanda, Muhonda Muheza na Magila
imedumu hadi sasa.

Hizi ni sehemu ambazo Ukristo ulishamiri.

Misheni Kota ndiyo sehemu pekee katika Dar es Salaam ambapo wamisionari
walifanikiwa kujenga kanisa.

Wakristo walitengewa katika sehemu hii kuwa makazi yao".
(Kutoka kitabu: "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924-1968)....")