Re: Masheikh wapiga kambi Bungeni kushinikiza Mahakama ya Kadhi kupita
999,
Kuna kitu kimoja umekisema cha kweli kabisa nacho ni kuwa
Waislam na Wakristo hawana ugomvi na haya tunayoshuhudia
sasa ni matokeo ya wanasiasa.
Lakini huwezi kuyajua haya ikiwa huijui historia ya kweli ya
Tanganyika kuanzia wakati wa ukoloni miaka ya mwanzo ya 1900
uje miaka ya kati wakati Waafrika wanaanza harakati za kudai
uhuru hadi kufikia uhuru wa Tanganyika mwaka 1961.
Ukiijua historia hii ya Julius Nyerere anafika Dar es Salaam mji
wa Waislam anapokelewa na Abdulwahid Sykes na wenzake
katika TAA, Nyerere anakutanishwa na Mufti Sheikh Hassan bin
Amir na wazee wengine...
TANU inaundwa, Nyerere anasafiri na Ali Mwinyi Tambwe katibu
wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Muslim Union of Tanganyika)
na Dossa Aziz, Jimbo la Kusini mwaka 1955 kwenye ngome ya
Ukatoliki kuitangaza TANU kufikisha mwito wa uhuru...hapo Lindi
akipokelewa na Sheikh Mohamed Yusuf Badi, Salum Mpunga na
Yusuf Chembera...
Ikumbukwe kuwa wakati huo mapadri walikuwa wakiwakataza waumini
wasijiunge na TANU.
Sheikh Hassan bin Amir anaiongoza TANU katika misingi ya kupiga
vita udini alipohisi TANU inaweza ikaathirika na hilo...na kwa kweli
mwaka 1958 kikaundwa chama cha Waislam All Muslim National
Union (AMNUT)... Waislam wakakikataa...
Nimetaja kwa uchache tu hawa mashujaa wa uhuru wa Tanganyika...
Hawa wazee wetu walionyesha upendo mkubwa na kukita misingi
ya umoja.
Kitu gani kimetokea hii leo hali imegeuka imekuwa ya uhasama?
Inawezekana hii ni laana ya hawa wazee kwa kuwa tumeifuta
historia yao?
Nani amesababisha uadui huu?
Wanajamvi tunaweza kujadili haya?
Kutoka Kushoto:Iddi Faiz Mafongo (Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na TANU), Sheikh Mohamed Ramia (Khalifa wa Qadiriyya), Julius Nyerere, Saadani Abdu Kandoro na Haruna Taratibu. Picha imepigwa Dodoma Railway Station 1956 wakati wapigania uhuru hawa wakitembea nchi nzima kufikisha ujumbe wa TANU kwa wananchi kuwa kutawaliwa ni fedheha.
Last edited by Mohamed Said; Today at 06:55.
No comments:
Post a Comment