Tanzania na
Propaganda za Udini
“Watu wema ni watu wema wawe wa dini yoyote na watu
waovu ni waovu; wawe wa dini yoyote ile. Kama watu wema wenyekupendelea viumbe
wenzao mema hawashikamani, basi waovu wenye kumfuata Shetani watashinda na watatawala.”
Ibrahim Noor Shariff

Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.
Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.
Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.
Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.
Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.

Prof. Ibrahim Noor Shariff
Mwanachuoni wa Chuo Kikuu Cha Rutgers, New Jersey,
Marekani, Ibrahim ni msomi wa Sanaa, Tarikh (Historia) na Fasihi ya Kiswahili.
|
Prof. Ibrahim Noor Shariff ameandika kitabu kipya cha Kiswahili kuhusu "Udini na Ugozi," Tanzania.
Mwandishi kakusudia kuandika kitabu chake kwa Kiswahili ili ukweli uwafikie wale watu wengi ambao kila siku wanatiwa sumu za udini Tanazania.
Inawajibika kitabu hiki kisomwe na kila Mtanzania hasa wakubwa wa serikali, wanasiasa, mapadri na mashekhe.
Makusudio ya kitabu hiki ni kuihifadhi nchi yetu na sumu za chuki za udini zinazopaliliwa kwenye masomo ya vijana wa leo ambao ni viongozi wa kesho.
Inatakiwa kila wenye uwezo wafanye juhudi kuondoa propaganda shuleni mwetu na washikilie kusomeshwa historia ya ukweli.
Kitabu hiki “Tanzania
na Propaganda za Udini” kina milango mitatu na sahifa 152.
- Mlango wa Kwanza unahusu “Taarikh ya Kuwasili Kwa Wabantu, Washirazi na Waarabu Pwani ya Afrikaya Mashariki.” Hapa anaeleza kwa ushahidi wa taarikh usiokatalika kwamba Waarabu wamefika Pwani ya Afrika Mashariki maelfu ya miaka iliopita na Wabantu wamefika pwani hiyo katika karne ya 16 B.K. Makusudio ya mlango huu ni kuonesha kwamba Waarabu si wageni bali ni wenyeji wenye haki hapa sawasasa na wenyeji wengineo.
- Mlango wa Pili unazungumzia “Propaganda za Siasa za Chuki na Athari Zake.”Humo tunaona uovu wa propaganda za udini zilizowatuhumu Waarabu na Waswahili Waislamu peke yao kukamata, kuuza na kumiliki watumwa. Propaganda hizo zimepelekea kuuliwa maelfu ya Waislamu bure bila ya sababu ilipovamiwa Zanzibar, nchi yenye Waislamu wengi, na kumezwa na Tanganyika 1964.
- Katika Mlango wa Tatu “Tanzania na Propaganda za Udini Shuleni“ mwandishi, ambae ni Profesa wa Sanaa, anaonesha ubingwa wake wa kuchambua picha. Anatunakilia picha za kuchorwa kutokana na vitabu vya shule za Tanzania zinazoonesha Waarabu na Waswahili Waislamu wanawakamata, kuwapiga na kuwauwa wanyonge wa Kiafrika ili kuwafanya watumwa. Hapohapo Profesa Ibrahim anaonyesha uzushi wa picha hizo zilizokopiwa na kubadilishwa kutoka picha za wauzaji watumwa wa Kizungu huko Amerika. Pia ameonesha kwamba bila ya shaka picha nyingine zimebuniwa na wachoraji na hazina ukweli. Prof. Ibrahim Noor anakazia katika kitabu chake hiki kuyapitia na kuyatengeneza masomo ya taarikh (historia) katika shule za Tanzania. Anataka masomo haya yajengwe kwenye misingi ya taarikh ya kweli, sio misingi ya uongo wa siasa za udini unaotokana na ukoloni.
Prof. Ibrahim Noor
ana hadharisha Watanzania wote na hatari ya kuendelea kupanda mbegu za chuki dhidi
ya Waarabu, Wahindi na Waswahili na khasa Waislamu katika mipango ya masomo
Tanzania. Hizi chuki za udini zitaleta balaa kubwa kuliko mauwaji ya Zanzibar
ya 1964. Watakaoumia na chuki hizi ni wafuasi wa kila dini na kila kabila nchini
Tanzania. Kitabu hiki kinahitajia kimfikie kila mwenye uwezo wa kubadilisha
mambo Tanzania, kwa mfano:
a)
Wahishimiwa Memba /Wabunge Tanzania
b) Memba wa Baraza
la Wawakilishi Zanzibar
c) Mawaziri wa Serikali
ya Muungano wa Zanzibar
d) Wakubwa wa Makanisa
na Wakubwa wa Vyama vya Kiislamu
e) Wakubwa wa Vyama
vya Siasa
f) Wakubwa wa Magazeti
g) Wakubwa wa TV
na Radio
h) Na kabla ya wote hao waliotangulia
ni mimi na wewe wananchi ambao tunapiga kura kuwachagua viongozi wema
Kitabu kinauzwa:
DAR ES SALAAM
Tanzania Publishing House, Samora Avenue
Tanzania Publishing House, Samora Avenue
Ibn Hazm
Media Centre Msikiti wa Mtoro na Manyema, Phone: 0773 777 707
TAMPRO, Magomeni
Area along Morogoro Road, Adjacent to Kinondoni Municipal, Plot no. 169 Block
R, Kinondoni Dar es Salaam.Phone: 0222172182
KEF “Kalamu
Education Foundation”, Magomeni– Kinondoni District, Dar es Salaam.
ZANZIBAR
Masomo
Bookshop, behind the Central Market, Zanzibar, Phone: 0242 232652
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-historia/823100-kitabu-kipya-tanzania-na-propaganda-za-udini-na-prof-ibrahim-noor.html#post12218146
http://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-historia/823100-kitabu-kipya-tanzania-na-propaganda-za-udini-na-prof-ibrahim-noor.html#post12218146
1 comment:
AHsante Prof. Ibrahim Noor. Kwa hakika vijana wa nchi ndio utajiri mkubwa wa Tanzania. Na kujenga akili na fikra za vijana ni msingi muhimu. Ikiwa dola na serikali inamiliki leo, basi vijana wanamiliki mustakbal wa nchi yetu. Prof. Ibrahim anatuonesha vipi fikra za vijana wa Tanzania zinapotezwa. Pia anatuonesha vipi kutengeneza mambo. Kila Mtanzania anahitajia kusoma kitabu hichi ili kuokoa Tanzania na hatari ya udini.
Post a Comment