Quote By 1701 View Post
Kwani kiswahili ni lugha ngumu?ipo siku wewe unayejitoa ufaham bwana said,na wapumbavu wote wanasiasa hasa hawa manyang'ao wa sasa,ipo siku kwa mtutu wa bunduki ntawaua mimi mwenyewe
1707,
Umeghadhibika.
Ukiwa na hasira fikra hazikai sawia.

Hii ni hatari.

Kumtishia mtu kumuua ni kosa la jinai lakini mimi nalichukulia kuwa hujakusudia
ila hamaki ndiyo zimekupeleka huko.

Nakueleza haya kwa kuwa ingekuwa kweli wewe ni shujaa na unaweza kuniua
kwanza ungeonyesha ushujaa katika mambo madogo.

Ungeonyesha ujasiri wako kwa kuingia JF bila ya kujificha nyuma ya hili pazia
jembamba.

Naliita pazia la JF jembamba kwa kuwa nikitaka kukujua wewe ni nani ni
rahisi sana.

Lakini pia hapa naliona tatizo la kisaikolojia ulilonalo.

Unapotoa vitisho hadharani vya kuniua mimi ujue hapo hapo unahatarisha
maisha yako mwenyewe.

Waulize polisi katika somo hili watakupa mifano hai mingi inayotisha.

Watu hawauani kwa kuwa wamekutana katika barza na wakapingana hoja.
Jitulize.

Unaweza mikiki na vishindo vya JF bakia jamvini.

La una moyo wa kuku huhimili vishindo jitoe kabisa lakini hili la kunitishia
kuniua halifai.

Utajiponza.
Vitisho kama hivi vitakuangamiza.

Jibu langu kwako na vitisho vyako nimeviweka katika blog yangu.
Nitaweka link hapa JF.