Tuesday, 17 March 2015

KUTOKA JF: MAJEMADARI WA VITA VYA MAJI MAJI - SULTAN SONGEA BIN RAUF NA SHEIKH SULTAN MATAKA BIN HAMIS MASSANINGA

  1. #89   Report Post    
    Pascal Ndege's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 24th November 2012
    Posts : 833
    Rep Power : 587

    Likes Received
    134

    Likes Given
    25

    Default Re: Ukweli wa Vita vya MajiMaji

    Ahaaah ndio maana songea kuna mabomu sasa
    MZEE MKUDA




  2. #90   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 6,370
    Rep Power : 339995

    Likes Received
    5490

    Likes Given
    268

    Default Re: Ukweli wa Vita vya MajiMaji

    Quote By Pascal Ndege View Post
    Ahaaah ndio maana songea kuna mabomu sasa
    Pascal Ndege,
    Soma hii hapo chini kama inavyoandikwa sasa na wanahistoria wetu:

    "Anasema hali hiyo ilitokea kwa sababu Chifu Songea Mbano alikuwa ndiyo Jemedari Mkuu wa Jeshi la Wangoni na alikuwa ni hodari sana asiyeogopa lolote kwa hiyo Wajerumani walitaka abakie ili wamtumie kwa malengo yao."

    Sasa soma kama nilivyobadili mimi:

    "Anasema hali hiyo ilitokea kwa sababu Sultan Songea Bin Ruuf alikuwa ndiyo Jemedari Mkuu wa Jeshi la Wangoni na alikuwa ni hodari sana asiyeogopa lolote kwa hiyo Wajerumani walitaka aba
    kie ili wamtumie kwa malengo yao."(Jina lake khasa ni Sultan Songea Bin Rauf siyo "Ruuf."
    Hii "Rauf" ni katika majina 99 ya Mwenyezi Mungu).

    Jina hili kwa ukamilifu na sahihi lilitakiwa liandikwe hivi: Sultan Songea Bin Abdirauf kwa kuwa Rauf ni jina katika majina ya Allah yeye anatakiwa kuitwa "Abdirauf," yaani Mtumishi wa Allah."

    Sasa usisahahu huyu Sultan Songea bin Rauf anamwandikia Sheikh Sultan Mataka Bin Hamis Massaninga

    Wakati huu walikuwa katikati ya dimbwi la vita na Wajerumani.

    Ukitafiti historia ya Tanganyika kwa umakini wake unaotakiwa vitu kama hivi ni vingi sana.
    Ni wajibu wetu sasa kuiweka sawa historia hii.

    Haya ni makosa yanayotakiwa kusahihishwa.

    Pascal Ndege,
    Umehusisha Vita Vya Maji Maji na "mabomu Songea," kwa kuwa majemadari wake walikuwa akina Sultan Songea Bin Rauf na Sheikh na Sultan Mataka Bin Hamis Massaninga.

    Sipendi kuwachosha watazamaji wetu hapa,
    In Sha Allah nitakupa jibu la katika "post," yangu ijayo.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 13:22.
  3. #91   Report Post    
    Mohamed Said's Avatar
    JF Senior Expert MemberArray
    Join Date : 2nd November 2008
    Posts : 6,370
    Rep Power : 339995

    Likes Received
    5490

    Likes Given
    268

    Default Re: Ukweli wa Vita vya MajiMaji

    Quote By Pascal Ndege View Post
    Ahaaah ndio maana songea kuna mabomu sasa

    Pascal Ndege,

    Ungetafakari kwanza na uisome historia kabla hujasema hayo uliyosema.
    Umefanya haraka kuhusisha Vita Vya Maji Maji na "mabomu."

    Historia ya mashujaa wale waliouliwa katika vita ile pamoja na makamanda
    wao karibu ya 70 walionyongwa na Wajerumani si kitu cha kufanyiwa mzaha,
    kejeli nk.

    Vita Vya Maji Maji athari yake ilikuja kuonekana wakati TANU ishaundwa
    Dar es Salaam mwaka 1954.

    TANU Southern Province iliundwa na Suleiman Masoud Mnonji, Salum
    Mpunga 
    na Yusuf Chembera na baadae Sheikh Mohamed Yusuf Badi
    (kuwataja wachache) ambae ndiye alikuwa sheikh maarufu Lindi alijiunga
    na harakati hizo za kudai uhuru.

    Katika kundi hili alikuwapo Bi. Sharifa Biti Mzee mwanamke shujaa katika
    TANU.

    TANU ilipata nguvu sehemu zilezile walizotoka makamanda wa Vita Vya Maji
    Maji na sehemu hizi wakazi wake wengi walikuwa Waislamu.

    Kanisa likawa linawakataza waumini wake kujiunga na TANU na harakati za
    kudai uhuru.

    Pascal Ndege,
    Najua historia hii ni ngeni kabisa kwako hujapatapo kusomeshwa wala kuisikia
    popote na ndiyo maana akili yako kwa haraka ikaruka miaka na miaka ya
    historia ya kweli ya Tanganyika ukaja leo miaka hii ya 2014/15 ukaleta mambo
    ya "mabomu," tena kwa kebehi.

    Waswahili tuna msemo: "Asiyekujua hakuthamini."

    Nina mengi katika historia na athari ya Vita Vya Maji Maji kwa wazee wetu.
    Ukipenda nitaileta hapa majlis.
    Last edited by Mohamed Said; Today at 16:28.
    Edit / Delete

No comments: